Kilimo kwanza iliishaje mpaka ije Matokeo makubwa sasa?

Kilimo kwanza iliishaje mpaka ije Matokeo makubwa sasa?

clasi

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2013
Posts
379
Reaction score
726
Salamu wanaJF.

Hhivi karibuni kumeibuka mpango wa serikali wa MATOKEO MAKUBWA SASA (BIG RESULT NOW) swali langu hivi serikali huwa inafanyaga tathmini ya mipango yake kweli hapa kati tena kiliundwa kitengo cha PRESIDENTIAL DELIVERY UNIT/BUREAU.

Hivi kweli hivi vitengo vina ulazima mbona sioni mabadiliko?
 
Viongozi wa Tanzania ni mabingwa wa kupanga mipango ambayo kwa kweli haina utekelezaji wowote na kama inatekelezwa siyo kwa mafanikio. Katika elimu tulikuwa na mpango wa MMEM & MMES, nani anaweza kutueleza mafanikio ya mipango hii? Kwa hiyo hata huu mpango wa "BIG RESULTS NOW" utapita kama ilivyopita mipango mingine. TUSUBIRI TUONE WAKATI UTATOA MAJIBU.
 
Kwahiyo ulitegemea saa hii tungeongelea UVUNAJI MKUBWA SASA.
 
kuna mipango ilikuwepo inaitwa KILIMO CHA KUFA NA KUPONA, SIASA NI KILIMO etc. sijui iliishia wapi hiv na SUKITA nayo sijui ilifia wapi
 
Hi itakuwa ni njia ya kupiga hela kwa hizi semina kila wizara watu wanatengeneza mbinu za kuchota hela.
 
kuna kitengo kipya kinaanzishwa ikulu kitasimamia mageuzi ya kilimo nafkiri ndo mwendelezo wa kilimo kwanza kwa maana ya big results now
 
kuna kitengo kipya
kinaanzishwa ikulu kitasimamia mageuzi ya kilimo nafkiri ndo mwendelezo
wa kilimo kwanza kwa maana ya big results now

Mkitaka kuamini watu wanapanga mbinu za kuchota pesa fatilia hata wanaoteuliwa kuwa viongozi wa Big result na mchunguze mtapata majibu, ni ndugu zao tu.
 
Naipongeza kwa mikakati yake kuleta maboresho ya Sekta ya Elimu nchini. Ushauri wangu ni kwamba Serikal ni lazima ihakikishe mazingira bora ya Mwalimu, mazingira mazur ya mwanafunzi kujifunzap+BIG SALARIES to teacherz this will results to BIG RESULTS
 
Viongozi wa Tanzania ni mabingwa wa kupanga mipango ambayo kwa kweli haina utekelezaji wowote na kama inatekelezwa siyo kwa mafanikio. Katika elimu tulikuwa na mpango wa MMEM & MMES, nani anaweza kutueleza mafanikio ya mipango hii? Kwa hiyo hata huu mpango wa "BIG RESULTS NOW" utapita kama ilivyopita mipango mingine. TUSUBIRI TUONE WAKATI UTATOA MAJIBU.

Ni nguvu ya soda. They have no staying power. Mipango yao mingi ni changa la macho tu. Pole sana kama ulidhani walitaka kweli kutekeleza hiyo mipango.

Kuna wakati Waziri Mkuu (wakati huo) Edward Lowasa alitangaza mpango kabambe wa kutengeneza mvua kwa kutumia ndege. Ni vizuri kwamba lilikuwa changa la macho. Inatisha kuona watu kama hawa wanataka kununua Urais.
 
Kulikuwa na mipango ya chakula ni uhai, siasa ni kilimo. Mipango hii ilikufa bila tija. Wamalasia wameamuwa kutupa pesa tukafuta mipango yote iliyoanzishwa!
 
Nchi ya kitu kidogo
Nchi ya watu wadogo

Zote ni namna mbaya za matumizi ya pesa
ya Umma yasiyoweza kuleta matokeo
wanayosema kila uchao ni kama miradi ya
umwagiliaji inavyowapa pesa watu.
 
MKUKUTA,MKURABITA,KILIMO KWANZA,TATIZO LA MAJI KUWA HISTORIA,BIG RESULTS ni code za kisiasa kufanikisha mission za wanasiasa!
 
tunapaswa kufanya tathmini kwa miradi iliyopita kabla hatujaingia kwenye miradi mipya jameni pesa hizi za walipa kodi tutakuja kudaiwa wandugu
 
Kama bunge lina wabunge vilaza ishu kama hizi hawakumbuki...
 
Serikal dhaifu kaz kulimbikiza kauli mbiu tu utekelezaj f
 
Viongozi wa Tanzania ni mabingwa wa kupanga mipango ambayo kwa kweli haina utekelezaji wowote na kama inatekelezwa siyo kwa mafanikio. Katika elimu tulikuwa na mpango wa MMEM & MMES, nani anaweza kutueleza mafanikio ya mipango hii? Kwa hiyo hata huu mpango wa "BIG RESULTS NOW" utapita kama ilivyopita mipango mingine. TUSUBIRI TUONE WAKATI UTATOA MAJIBU.

Mkuu upo sahihi!,Viongozi wetu kwa mipango tu hawajambo!,yaani laiti km Mipango inayopangwa ingekuwa inaendana na maendeleo basi Tz ingekuwa juu zaidi ya South Afrika.
 
Back
Top Bottom