Kilimo: Kuongeza Thamani Yako Kama Mkulima(Agro-Value Spec)

TechTania

Member
Jul 31, 2018
91
225
Kilimo ni Sekta ambayo imekuwa ikitambulisha bara la Africa kwenye Dunia inayo tuzunguka. Kitu cha ajabu ni kuwa watu wachache sana Hupata thamani halisi ya Sekta hii pana na yenye faida.

Kwanza kabisa mimi ni Blogger na E-Com Entreprenur....Ila bado ni mkilima Pia! Sawa naweza kuwa siendi Shamba kushika jembe ila bado ni mmiliki wa shamba hivyo bado ni mkulima.

Kilimo ni Kitu amnacho tumerithi kwa karnenkadhaa kutoka kwa wazazi wetu maana kimekuwa kikitupatia Chakula na baadae kuibuka kuwa biashara pia baada ya Mkoloni kuleta mazao ya Biashara.

Kitu kinacho zidi kukera ni kwamba kati ya watu wanao dharauliwa na kuonwa wa kawaida ni mkulima. Hii ni kwa kuwa thamani yake imefichwa, na hajali maana anachukulia hiyo kama Sehemu ya maisha.

Wapo wakulima wengi tu, amabo wanatambua kuwa mkulima inamaanisha nini kwa Familia, Majirani, Watu wa Mijini, Viwanda na hata taifa kwa ujumla; Na kwa kufahamu hivyo wanafurahia kilimo kuliko baadhi ya waajiriwa wa serikali.

Ili linaweza kuwa swali la kitoto ila, Je, uliwahi kujiuliza nini kingetokea endapo wakulima wangeacha kuuza mazao yao?

Wangepata chakula cha kutosha kwa ajili ya familia zao. Ila kwa upande wa pili, Viwanda vingekosa raw materials hivyo kuanza kupata raw materials nje, Hiyo ingesababisha bei ya bidhaa kupanda hivyo watu mjini kushindwa kumudu mahitaji na hivyo Ukwepaji wa Kodi ungeongezeka...hivyo taifa zima kurudi nyuma kimaendeleo kwa asilimia kubwa

Hii yote ni kwa sababu ya mkulima na ndo thamani yake. Na ndo maana serikali itafanya vyovyote iwezavyo kuhakikisha mkulima analima....kwa kumpa motisha iwe hasi au chanya.

Ukifahamu kuwa huku kwenye 2nd na 3rd World Countries kilimo ndo kinabeba mataifa, Ndipo utajua.mkulima sio mtu wa kawaida.

Ila kama umefuatilia kiumakini...baada ya kufahamu hayo yote bado hujafahamu thamani halisi na jinsi ya kuitumia kufanikiwa na ninataka kukuonesha kitu hicho.....

Jinsi ya Kutumia Thamani Yako Kama Mkulima Kama Fursa

Kiufupi mi ni mfanya biashara(Namiliki E-Commerce Store Tatu), Ni mkulima na pia ni Blogger.

Nyingine humu zinaonekana kama sio kazi...Ila mimi nazichukulia Serious na zimebadili maisha yangu.

Kati ya hizo Model tatu...Kilimo ni moja ya kitu ambacho nakipenda na naelewa thamani yake. na nikisema thamani namaanisha;

1.Umoja ni Nguvu, Utengano ni Udhaifu

Ili kufanikiwa, Haupaswi kufanikiwa kivyako vyako ili uyaite hayo mafanikio.Kuna hawa jamaa huwa wanakuja wakati wa mavuno( Kipindi Tukianza Kuuza) wanaanza kuja na bei zao,Ukiwagomea wataenda kwa sababu sio wewe mkulima pekee wa zao husika.Ukigomea bei yake ataenda kwa jirani na jirani hawezi kugoma...Akigoma ataenda kwa mwingine. Ila piga picha kuwa kwenye kijiji chenu/wilaya mnafahamika kwa zao fulani. mkakutana na mkajiwekea bei kuendana na hali fulan..Mteja akija nanbei yake kwako ukagomea ukamwambia ni bei fulani, akaenda kwa jirani ikawa hivyo na jirani mwingine, atafika hatua akubaliane na bei yenu.Na hapo mtaonesha mnaheshimu kazi yenu na mnaitambua thamani.

2. Wewe Ndiye Mwenye Kuchagua Bei Sio Mteja

Kama nilivyosema, Utasikia.kuna mashirika ya mazao fulani na ni mengi kibao. Mashirika haya hujipangia bei kuendana na matakwa yao ...na wakilenga faida kuanzia kwao na watakayemuuzia.....Ila sio wewe.

Shida zisikufanye ukubali kushushiwa thamani na kila mkulima kwenye Wilaya yenu akikubaliana na bei kadhaa..Na wilaya nyinginwe zikafanya hivyo kikawepo chama hadi cha Manispaa..Thamani haitashuka tena.Na kila.Mka wakifanya Hivi...Faida itaomgezeka.kwa wakulima.na Serikali kupitia Kodi na Pia wanunuzi watazoa bei ow ulivyokuwa ukizoeleshwa

3.Fikiria Zaidi ya Mipaka

Mkitumia hizo njia za kwanza wateja wanaweza kupungua...Na saa nyinhine kupanga vikao vyao kujifanya hawatonunua ili mradi mpunguze bei.

Hili jambo lilitokea Mwaka jana, Kagera; Nilisaidia kuunda kikundi cha wakulima wa Maharage (Frozen) na wanunuaji wakagoma.

Tulichokifanya ni kwamba tuli Mpa Offer yule Mmiliki wa kampuni wale wanunuaji walio kuwa wanauzia..Tukapunguza 15% na akaanza kununua mazao bila shida maana bei yetu ilikuwa cheap kuliko ya wale jamaa.

Na hali ikitokea kama hii mtabidi mtumie.mbinu hii kuhakikisha Thamani yenu haishuki. mnaweza kuwa wakulima hata 20 tu.Mkapunguza bei na kumuuzia yule End User ambao wateja wenu wnamuuzia.Mtapata Faida kubwa.mno!

Extra Bonus!

Nina mpango wa kuanzisha Network ya wakulima amabako wanaweza wakakutana na Kushare Mazao yao na ambako wataweza kukubaliana Bei watakayo iweka kwenye zao Husika kwenye msimu Husika.Baada ya hapo kuwakutanisha na Wanunuaji Wa Kuaminika Kutoka Nje/Ndani ya Nchi.

Nakaribisha Maswali na Maoni, Pia Mawazo Yenu kuhusu Idea Hii

Nimeitengenezea Hati Miliki, Kwa hiyo Usifikirie Kuitumia


Ahsante! Kama makala hii imekufungua soma nyingine kwenye kitengo cha Ujasiliamali!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom