Kilimo cha miwa (Elimu, masoko na faida ya kilimo)

Abbyarico

Member
Aug 5, 2021
50
42
Habari za kutwa wapendwa ndugu na jamaa. Napenda kuchukua wasaha huu kwa kuweza kujoin kwa pamoja na wana JF wenzangu na waalimu wazuri wa kilimo.

Lengo la kuuandaa chapisho hili ni kutaka msaada kwa wataalamu wa kilimo cha miwa.

1 Jinsi ya uandaaji wa shamba
2-Jinsi ya uandaaji wa mbegu
3-Jinsi ya kupanda
4-Mbolea na madawa mazuri ya kutumia ili
Mmea uweze kuwa na afya nzuri
5-Muda wa mavuno
6- Ushauri wa mwalimu au mshiriki yeyote
Kwenye chapisho hili juu ya kilimo hiki
Cha miwa
7-Masoko, faida na hasara ya kilimo hiki

Karibuni sana ndugu zangu kwa msaada; kilimo ni ajira tukomboeni vijana kwa elimu kama hizi kusudi tuachane na mambo ya kulalamikia ajira mitandaoni.

Karibu sanaaa kwa msaada [mention]CHASHA FARMING [/mention] [mention]kilimo biashara [/mention] [mention]Kilimo na Ufugaji Bora [/mention] [mention]kilimo kwz [/mention] uwanja ni wa kwenu sasa
 
Miwa ni zao linalohitaji ardhi bora yenye rutuba na maji ya uhakika japo huvumilia ukame kama imeshaota sio rahisi kufa ni vema ukapanda kwenye udongo ambao sio kichanga kwa sababu kichanga hakitunzi unyevu kwa muda mrefu miwa yaweza kufa au kudhoofu sana kwenye kiangazi

Yafaa shamba liandaliwe mapema kwa kulima walau mara mbili baadae ukapiga harow japo sio lazima kisha upige mifereji ukisubiri mvua zinyeshe

Yafaa ulime kabla mvua za vuli hazijaanza yaani mwezi wa 9 kuendelea kusudi mvua zikinyesha tu upande Mapema. Miwa ikipandwa na unyevu ukiwepo inaota kwa kasi mbaka mvua za vuli zinaisha unahangaika na palizi na miwa itakuwa mikubwa

Zikianza mvua za masika mwezi wa 3 miwa itakuwa mikubwa unaweza piga palizi moja au mbili unaweka mbolea ya kukuzia hapo utafurahia show mapema mwezi june ni mavuno subiri mvua ya mahela kutoka kiwandani

Mbegu ya miwa ni miwa yenyewe unaenda mwa mwenzako ambaye muwa wake ni mpya bado haujavunwa ndo unakata kwake unapanda shambani kwako wakulima wengi nguvu zao nyembamba hawamudu mbolea ya kupandia kama ww unaweza unaweka lkn sio lazima

Umakini unahitajika sana hasa ktk kupanda ukipata wavuta bangi bila kuwasimamia wanafukia miwa empty mm ishantokea na hela unawapa tegemea uwezo wako wengine wanapanda miwa miwili pamoja wengine wanweka mmoja mmoja vyovyite vile inaota vizuri tu

Gharama ni kubwa mwamzoni tu ukishavuniwa mwaka wa 2 gharama ni palizi tu na mbolea ya kukuzia ikitojea kuna magepu mua haujaota vizuri unapanda na kipato utakita kinaongezeka kuliko awali

Tegemea na kiwanda ulichopo kilombero nasikia wanalipa pesa nzuri sana sijui kagera na tpc wakulima wanalipwaje kwa tani ya miwa mm niko mtibwa malipo yao ni kama mshahara wa kampuni ya wahindi kiduchu mno ila hvo hvo tunajikaza

Sina uzoefu sana ktk hii biashara kama nimekosea nrekebishwe sina ubaya
 
Cha kwanza muwa kabla hujalima inabidi utafute eneo ambalo ni lazima liwe karibu na kampuni utakayouzia na pia liwe linafikika kwa urahisi hasa nyakati za mvua.
Pili, chagua mbegu, miwa nayo ina mbegu zake kwahiyo inabidi uchunguze kampuni utakayouzia wanahitaji miwa gani na yenye sifa ipi, ndiyo maana nikakwambia uonane na field officer au mabwana shamba wa makampuni.
Tatu, lima shamba mapema kipindi cha kiangazi na uoteshe kabla mvua hazijaanza kunyesha hususani mvua za msimu wa mwezi wa 10/11 .
Yapo mambo mengi sana kwenye hichi kilimo hususani kwenye uandaaji wa shamba, viuatilifu, mbolea, palizi, umwagiliaji n.k
Uliza maswali zaidi kwa ufafanuzi zaidi au waweza kuja pm kwa mawasiliano zaidi ili nikupe mwongozo na usimamizi kutoka unapopanda hadi unavuna.
Kumbuka kilimo ni hatua hivyo inakupasa umhusishe mtaalamu toka unaandaa shamba mpaka unavuna, na kilimo hakina reverse kwamba ushakosea kwenye kuchagua mbegu hapo tayari ushaumia hamna tiba ya hilo, au hujatumia mbolea miwa imedumaa hapo hamna namna tena ya kuirudisha kwenye hali yake ya kawaida.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na unataka ulime miwa kwaajili ya sukari au ya kula?

Sent using Jamii Forums mobile app

Somo zuri sana mkuuu nimekuelewa sana but kwa kuwa nipo mbali na viwanda vya sukari nilitizama kwa kina sana kwa sababu watu wengi sana wanakula miwa lakini mm nilitaka nilime na kuweza kuwauzia wale wauzaji wa masoko makubwa kwa mbeya na dsm mkuu unanishaurije. Hapo
 
Miwa ni zao linalohitaji ardhi bora yenye rutuba na maji ya uhakika japo huvumilia ukame kama imeshaota sio rahisi kufa ni vema ukapanda kwenye udongo ambao sio kichanga kwa sababu kichanga hakitunzi unyevu kwa muda mrefu miwa yaweza kufa au kudhoofu sana kwenye kiangazi

Yafaa shamba liandaliwe mapema kwa kulima walau mara mbili baadae ukapiga harow japo sio lazima kisha upige mifereji ukisubiri mvua zinyeshe

Yafaa ulime kabla mvua za vuli hazijaanza yaani mwezi wa 9 kuendelea kusudi mvua zikinyesha tu upande Mapema. Miwa ikipandwa na unyevu ukiwepo inaota kwa kasi mbaka mvua za vuli zinaisha unahangaika na palizi na miwa itakuwa mikubwa

Zikianza mvua za masika mwezi wa 3 miwa itakuwa mikubwa unaweza piga palizi moja au mbili unaweka mbolea ya kukuzia hapo utafurahia show mapema mwezi june ni mavuno subiri mvua ya mahela kutoka kiwandani

Mbegu ya miwa ni miwa yenyewe unaenda mwa mwenzako ambaye muwa wake ni mpya bado haujavunwa ndo unakata kwake unapanda shambani kwako wakulima wengi nguvu zao nyembamba hawamudu mbolea ya kupandia kama ww unaweza unaweka lkn sio lazima

Umakini unahitajika sana hasa ktk kupanda ukipata wavuta bangi bila kuwasimamia wanafukia miwa empty mm ishantokea na hela unawapa tegemea uwezo wako wengine wanapanda miwa miwili pamoja wengine wanweka mmoja mmoja vyovyite vile inaota vizuri tu

Gharama ni kubwa mwamzoni tu ukishavuniwa mwaka wa 2 gharama ni palizi tu na mbolea ya kukuzia ikitojea kuna magepu mua haujaota vizuri unapanda na kipato utakita kinaongezeka kuliko awali

Tegemea na kiwanda ulichopo kilombero nasikia wanalipa pesa nzuri sana sijui kagera na tpc wakulima wanalipwaje kwa tani ya miwa mm niko mtibwa malipo yao ni kama mshahara wa kampuni ya wahindi kiduchu mno ila hvo hvo tunajikaza

Sina uzoefu sana ktk hii biashara kama nimekosea nrekebishwe sina ubaya

Somo kubwa sana mkuu barikiwa mno
 
Somo zuri sana mkuuu nimekuelewa sana but kwa kuwa nipo mbali na viwanda vya sukari nilitizama kwa kina sana kwa sababu watu wengi sana wanakula miwa lakini mm nilitaka nilime na kuweza kuwauzia wale wauzaji wa masoko makubwa kwa mbeya na dsm mkuu unanishaurije. Hapo
Ok kama unataka ulime kwaajili ya kula, mbegu zake ni tofauti na za sukari ila ulimaji ni sawa jaribu kuongea kwanza na wakulima wa eneo ulilopo maana kila eneo lina miwa yake inayoota vizuri eneo hilo ila kwa ushauri miwa inahitaji sana maji na rutuba/ mbolea jitahidi kuzingatia hilo
 
Ahsante sana kwa mwongozo mkuu
 
Inachukua mda gani muwa kukomaa Toka kupandwa had mvuno wa kwanza?

Na pia utaendelea kuvuna kwa mda gani au Mara ngapi Hadi kusafisha shamba na kupanda upya
 
Mojawapo ya miwa inayotumika kwa kula Tanzania
FB_IMG_1649045735549.jpg
images%20(47).jpg
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom