Biashara zipo nyingi tu ambazo waweza fanya bila kupigwa lakini hizi za miti acha kuwaingiza watu mkenge, naongea ukweliambao nimeona kwa macho yangu labda uhamie huko huko....! nd yale yale ya wakulima wa Mbozi, mtu anakopesha fedha na pembejeo kwa wakulima halafu wakati wa mazao kuvunwa wakulima wanatakiwa kulipa ile mikopo cha ajabu na kushangaza wanamua yule mtu anayewadai na aliyewakopesha kwa nia nzuri tu. Tuwe makini wapendwa mavuno ya miaka 10 si mchezo!
Teh teh! naona swali la mkuu Malila limemuingiza jamaa mitini.
Lakini hujataja hata biashara moja ambayo mtu anaweza kufanya bila kupata changamoto ktk dunia ya leo na hasa Tz yetu. Nitajie moja tu, usiseme ziko nyingi.
Futa kauli hiyo.Kwa hiyo hoja yako ni ipi hapo, kutapeliwa ama miaka 10 ni mingi.
Yaonekana bado kuwa watu hawajitambui ama bado watoto wa shule humu.
Ina mana hujawahi kununua shamba ama kiwanja? Na je taratibu za kuuziwa mali isiyohamishika hauijui? Ama wataka tukupe elimu kwanza taratibu za kufuata katika ununuaji wa mali zisizohamishika?
Upande wa muda sio tatizo kwa mwekezaji mwenye muono wa mbali kama uwezo wako ni wa kuwekeza upate mia mbili baada ya siku mbili, ni juu yako. Ila kwa mwenye malengo ya badae msiwakatishe tamaa, wapeni moyo kama wana nia na sio lazima kupitia kwangu bali hata kama wewe wafahamu kuhusu kitu waweza mshauri pia ama ukampa direction ya uwekezaji bt, unapoponda na kuwatisha halafu huwapi mawazo wafanye nini mbadala unakuwa hujakamilika.
Tupo kwa ajili ya kubadilishana mawazo ya kimaendeleo sio kupondana wala kutishana ndugu.
NB: Unapotoa angalizo ama walakini wa jambo fulani jaribu kutoa na wazo mbadala ili mawazo yako yakamilike.
Asante kwa kuchangia,
Watz wenzangu ni vizuri tukijenga tabia ya kusema ukweli hata kama unauma. Kwa kuwa na maelezo nusu nusu tunaumizana sana. Kama angekuwa na uhakika na anacho kisema angeweka hadharani kama mimi nilivyofanya, jf na hasa jukwaa la uchumi ni sehemu ya ukombozi, tusaidiane. Igeleke na Kibengu kuna ardhi ya hatari ndugu zangu. Niko ktk vijiji hivyo mwaka wa saba sasa. Igeleke manpower ni tatizo pia.
Tuokoe muda, kama una nia ya kuwasaidia wenzako wapande miti basi watafutie ardhi Kipanga, Lulanda,Ibwanzi na Ukami. Huko ardhi ipo na nzuri pamoja na manpower. Igeleke wanunue wenyeji kwa sababu za kiusalama.