Mimi niliwahi kulima kilimo hicho ambacho ni mashuhuri sana mkoa wa Dodoma ila nilipumzika kukilima kutokana na sababu nyingi ikiwemo ya kupungua kwa soko lake baada ya kuja kilimo cha ufuta. mara ya mwisho nililima ekari mia moja na kuvuna gunia za maganda zaidi ya 1200. Kwa ujumla nilikuwa nalima kwa trekta au ng'ombe na kuwapa wenyeji wanipandie kienyeji.
Changamoto nilizokutana nazo ni kama;-
1, Bei , wakati wa mavuno bei inakuwa chini sana mpaka usubiria mpaka mwezi wa 12 au january.
2. karanga zinahitaji palizi hata mara tatu kama kuna mvua nyingi na palizi yake ni ghali kutokana na kuwa karibukaribu sana.
3. Kuvuna unatakiwa kung'oa wakati kuna mvua ili kurahisisha kazi . Hapo napo kuna tatizo kubwa la karanga kuota kama mvua itaendele, hata ugeuze juu chini kama kuna mvua nyingi zitaota. tu
4.Kupungua, gunia nne za maganda unapata gunia moja la kichere.
5. Gharama za uzalishaji ni kubwa kwani unahitaji, kulima , kupalilia hadi mara tatu, kung'oa , kuchambua ( yaani kutoa kwenye mashina), usafiri wa kurudisha nyumbani, magunia au mahali pa kuhifadhi, kukoboa kwa mashine ili kupata kichere na kuchangua vichwa na vipande ndipo usafirishe kwenda kuuza na huko kuna madalali.
Ndiyo huo uzoefu wangu kwenu , nawatakia kila la heri.