Kilimo cha alizeti

zeeble

Member
Jan 4, 2022
34
30
Ndugu zangu habari zenu jamani, mimi kijana Nina miaka 23 naishi Morogoro. Katika harakati za kuhangaikia maisha nimekuja kugundua kijana kama mimi ili niweze kufanikiwa kwa haraka zaidi kilimo ni njia pekee inayoweza kutusaidia kutusua kimaisha. Najua zipo shughuli nyingi za kutuingizia kipato ukiachana na kilimo.

Lakini Kwa upande wangu nimeamua kujikita na kilimo. Kwa Sasa Nina uzoefu wa kilimo Cha mpunga kwasababu maeneo ninayoishi ndiyo shughuli kuu. Ukiachana na hayo nimevutiwa na kilimo Cha ALIZETI kimenivutia Kwa sababu naona trends sokoni ni kubwa yaani inahitajika sana (MAFUTA).

Hivyo basi ningeomba kama Kuna uwezekano wa kupata eneo au maeneo(SHAMBA) nijue gharama Kwa kukodi na pia namna ya kuandaa SHAMBA na baada ya muda gani mavuno yanafanyika.

AHSANTENI SANA
 
Hongera.

Jiandae vyema..tafuta nyuzi za kilimo cha alizeti ziko nyingi humu.

Chamsingi kuwa well informed.

#MaendeleoHayanaChama
 
Ulimaanisha hizi si ndio?
20220329_144312.jpg
 
Nipo mpwapwa Dom, moja kati ya kilimo kinacholimwa sana huku. Mvua za mwezi wa 12, wa 1 hata wa pili unaweza ukapanda kimsingi ni zao linalovumilia ukame haliitaji mvua nyingi. Kukodi shamba huku ni elf 30 na kulima (wanatumia ng'ombe au powertiller) 25 - 30k kupalilia per acre 30k.

Ni kilimo flan hv hakina mambo mengi sn sabab wenyej wa huku hawatumii mbolea ardhi kwa sehem kubwa ina rutuba. Hakuna matumizi ya viwatilifu (japo magonjwa au wadudu yanaweza kutokea). Mavuno baada ya miez 3-4. Makadirio unaweza pata gunia 3-4 kwa eka. Palizi hata ukipalilia mara moja unaweza kuvuna.
 
Kilimo Cha kupata gunia 3-4 kw hekar skushaur maana utabaki kulima kilimo Cha kupata pesa y kununua vocha na kuinglia kweny vibanda umiza cku mzee wa kutetema anafanya yake! Alzet ili irudshe gharama z uendeshaj upate walau gunia 10+ kwa hekar,
 
Kilimo Cha kupata gunia 3-4 kw hekar skushaur maana utabaki kulima kilimo Cha kupata pesa y kununua vocha na kuinglia kweny vibanda umiza cku mzee wa kutetema anafanya yake! Alzet ili irudshe gharama z uendeshaj upate walau gunia 10+ kwa hekar,
Hivi hata huko Ukraine na wao wanapata gunia 3-5 kama sisi au inakuaje?
 
Kule naskia heka moja unavuna gunia 50 na kuendlea nko na mshikaj Wang tumelima heka 60 tunajiandaa kwenda kuvuna,
 
Kule naskia heka moja unavuna gunia 50 na kuendlea nko na mshikaj Wang tumelima heka 60 tunajiandaa kwenda kuvuna,
Pia mkuu ....
Ivi unaweza kulima alizeti mikoa kama Songea, Njombe ....kwenye mvuà nyingi na ukapata mavuno mazuri?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom