Vugu-Vugu
JF-Expert Member
- Feb 24, 2017
- 1,381
- 1,593
Wanajamii amani iwe kwenu!
Katika hali isiyo ya kawaida jana nilimshuhudia Raisi wa Tanzania Dk John Joseph Pombe Magufuli
akiwa na furaha iliyopitiliza, Akiongea kwa bashasha na kujiamini Raisi Magufuli anasema hajawahi kuona umati mkubwa wa watu kama ule uliokuwapo kwenye viwanja vya Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjoro, Mkoa mbao wakati tunapata Uhuru ulikuwa na watu 300,000 tu
Itakumbukwa kuwa mkoa wa K`njaro unawakazi takribani mil 1.6 huku ukiwa na shule za sekondari zaidi 279, Ukifuatiwa na mkoa wa Dar-es salaam wenye watu mil 5 ukiwa na shule za sekondari 230 pekee na kisha mkoa wa Mwanza wenye watu 2.7 huku kukiwa kuna shule za sekondary 218 achilia mbali Mbeya kabla ya kuwanywa iliyokuwa na shule za sekondari 270.
Kama ilivyokawaida ya wanasiasa wote duniani kote hupenda sana kuongea/kuhutubia watu wengi na hicho wao hukiona kama kipimo cha kukubalika kwao."all politician are adicted to mass cogregations" yaani wanasiasa wote wana-uraibu wa kupenda kuhutubia watu wengi eg Mwenyekiti wa CHADEMA Mh Freeman Aikael Mbowe huyu bwana yuko radhi akodi hata Helkopta ili tu akusanye watu wengi wa kumsikiliza bili kujali mass quality wao huangalia Mass quantity tu na ndio faraja yao.
Jambo hili limemtokea jana Raisi wa Tanzania wa awamu ya Tano Mh Dk John Joseph Pombe Magufuli katika viwanja vya chuo cha biashara Ushirika Moshi (MoCU) baada ya watu kwenda kumpokea kwa lazima kwa mujibu wa sheria na kanuni za uendeshaji wa serikari,Watu hawa hawakuja wote kwa mapenzi yao.
Kama tunashule za sekondari 279 na kila shule ikaleta wastani wa watu 50 tu, Basi jana tulikuwa na wadau toka shule za sekondari 13,950 bila kuhesabu shule za msingi ambazo ni zaidi ya 500,Nyuma ya viwanja vya ushirika kipo chuo cha Biashara cha Ushirika ( MoCU) chenye wanafunzi zaidi 1,000 nao walikuwepo kwa lazima, Ukivuka barabara ni chuo cha cha polisi CCP nao walikuwepo kwa lazima, Juu kidogo chuo cha KCMC nao walikuwepo kwa lazima, Mbele kidogo ni chuo cha Mwenge University collage nao walikuwepo kwa lazima.
Uongozi wa mkoa wa Kilimanjoro nawapongeza kwa kumuhadaa mwanasiasa huyu mwenye adiction ya mass quantity badala ya mass quality,Siamini wala sioni kama ni busara Raisi wa inchi nzima kujisifia mkusanyiko wa watu wether ni wengi au wachache Raisi anapashwa kujikita kwenye Maendeleo tu. Waje 20 waje 20,000 wewe fanya kwa kadiri unavyoweza usichanganwe na wingi au uchache wa watu, Ipo siku utaenda mahali utakosa watu utakasirika Raisi wangu, Huu si muda wa kampeni hata kama uko kwenye kampeni mbona unapambana na usiyemjua?
Hongera sana wanafunzi wote wa mkoa wa K` njaro kwa kumpatia Mh Rais furaha ya Moyo wake ila ninyi wafanyakazi na wananchi wa Moshi Mungu anawaona.
Mwafwaaaaaaaaaaaaaaa.
Msemakweli Mpenzi wa Mungu
Mungu ibariki Tanzania na Watanzania.