figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,720
- 55,859
Polisi wa Kutuliza Ghasisi (FFU) mkoani Kilimanjaro wametumia mabomu kuwatawanya wananchi wa eneo la Tarakea wilayani Rombo, waliokusanyika kutaka kuwekewa matuta,mwendesha pikipiki kugongwa na lori la kubeba magogo na kufa papo hapo, wananchi walianza kuhamasishana na kufunga barabara.
Kamanda wa Polisi Mkoa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa hakupatikana kuelezea tukio, lakini Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Lembris Kipuyo alithibitisha kutokea kwa vurugu hizo.
“Tumetumia busara zote kuhakikisha barabara hiyo inafunguliwa lakini ikashindikana, hivyo polisi na Serikali tukalazimika kutumia nguvu,” alisema Kipuyo