Kilimanjaro Express

ceekay

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2011
Posts
413
Reaction score
156
Mimi ninasafiri sana kati ya Dar - Moshi - Arusha kwa basi tajwa hapo juu. Leo tarehe 20 December 2016, mimekuta mfumo mpya kwenye ofisi yao ya Moshi, unalipa Tshs 3,000 na kukatiwa tiketi ya Arusha (Hakuna kulipa ndani ya basi kwa konda). Mfumo huu ni mziri (tena sana).

Kitu kilichonifanya kuandika uzi huu, ni pale basi ilipofika. Kondakta na dereva wa basi lilipofika wakasema "Hakuna nafasi!!! Nafasi zimejaa!!!". Hilo jambo likasababisha abiria kuanza kusukumana tukiwa hatuamini kinachoendelea. Dereva alipoona hilo na yeye akaja kuanza kusukuma abiria ili wasiingie. Nikajiuliza maswali kadhaa:
1 - Kilimanjaro Express ninayoijua mimi ndio kuna utaratibu mbovu hivi? Je ni kwa kuwa ni kipindi cha sikukuu wakiwa wanaamini kuwa watapata tu abiria?
2 - Kwanini ofisi ilikatisha tiketi kuzidi nafasi zilizopo kwenye gari husika?
3 - Haki ya abiria iko wapi hapa?

It's very [HASHTAG]#sad[/HASHTAG], Kilimanjaro Express badilikeni
 
Tulishasema hapa mara nyingi hapa kwamba Kilimanjaro na Dar Express ni moja ya mabasi yenye ubabaishaji mkubwa lakini watu bado wanakuwa vichwa vigumu hawaelewi, badala yake wanakuja hapa kulialia.


Acha wawapigeni tu maana hakuna namna sasa,...
 
Nyokooo WA nyokoo sswaya
 
Tulishasema hapa mara nyingi hapa kwamba Kilimanjaro na Dar Express ni moja ya mabasi yenye ubabaishaji mkubwa lakini watu bado wanakuwa vichwa vigumu hawaelewi, badala yake wanakuja hapa kulialia.


Acha wawapigeni tu maana hakuna namna sasa,...
Leta bombadier basiii
 
Ungewasiliana na RTO wa Kilimanjaro, ni kosa kisheria kuja abiria kupita kiasi. Ikitokea ajali ni balaa
 
just report to Sumatra
 
Andika namba ya gari hapa nilifanyie kazi...

Fujo zilikuwa kubwa sana nikasahau kufanya hivyo. Ila nikiliona tena nitazileta hapa namba za gari kwa sababu nawakumbuka dereva na konda wake pia.
 
UMETOZWA NAULI KUBWA KWENYE BASI KULIKO UMBALI UNAOKWENDA?
Ni rahisi tu, fanya yafuatayo:
1. Bishia nauli uliyotozwa kuwa si halali. mfano kama unakokwenda ni Dar-Mafinga, nauli inapaswa kuwa 20,000 wewe ukatozwa Dar-Njombe 25,000, bishia. Kondakta akikataa lipa, ingia kwenye gari.
2. Atakupa tiketi imeandikwa Dar-Mafinga 25,000 au atakupa tiketi imeandikwa Dar-Njombe 30,000. Pokea
3. Ipige picha hiyo tiketi, au iscan kisha itume kwenda nambari 0682 887722(kwa whatsapp,telegram au wechat) ukielezea kuwa umetozwa nauli kubwa kuliko umbali wa safari au umepandishwa bus ordinary wakati wewe ulitozwa nauli ya luxury. Na kwamba kondakta amekataa kukuandikia tiketi ya unakokwenda badala yake akakuandikia tiketi inayoonesha kituo ambacho basi linaishia. Au Tuma ujumbe au piga simu kwenda 0800 110 019 au 0800 110 020 (bure). Namba hizi tumia hata pale gari inapokatisha ruti au kuwatelekeza njiani baada ya kuharibika.
4. Basi litasimamishwa kituo cha mbele, utarudishiwa nauli yako. Kama limekamatwa na askari polisi basi dereva au kondakta atarudisha nauli na 30,000 itamhusu. Akikamatwa na SUMATRA basi atarudisha nauli na faini ya sh.250,000 itamhusu.
5. SAMBAZA UJUMBE HUU KADIRI UWEZAVYO, MUELIMISHE MWENZIO
KWA HISANI YA RSA TANZANIA,
USALAMA BARABARANI JUKUMU LETU SOTE
 
ww jamaa m'mbeya sana inaelekea maana habar haielewek na hakuna hata ushaid wa ku suport usemayo....

1. Uliza swali pale ambapo haijaeleweka
2. Ulitaka ushahidi wa namna gani mfano?
 
Tulishasema hapa mara nyingi hapa kwamba Kilimanjaro na Dar Express ni moja ya mabasi yenye ubabaishaji mkubwa lakini watu bado wanakuwa vichwa vigumu hawaelewi, badala yake wanakuja hapa kulialia.


Acha wawapigeni tu maana hakuna namna sasa,...

Nimeanza kuamini hii kitu, hzo kampuni zimeanza kushiba hela. Tatizo letu tunajisahau sana when it comes to customer care.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…