Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,445
- 7,813
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salam imeamuru kampuni ya Kilimanjaro Truck Company Limited, inayomiliki mabasi ya Kilimanjaro Express kulipa fidia ya Sh300 milioni kutokana na moja ya mabasi yake kugonga gari dogo lililokuwa linatumiwa na familia na kusababisha kifo cha mmoja wa wanafamilia.
Amri hiyo imetolewa leo Jumatano Desemba 21, 2022 na Jaji Leila Mgonya katika hukumu ya kesi ya madai iliyofunguliwa na mfanyabiashara Leonard Paul Kisenha dhidi ya kampuni hiyo, Roland Sawaya (mkurugenzi mtendaji na mmiliki wa kampuni hiyo) na dereva wa basi hilo, Mjahid Mohamed.
Ajali hiyo ilitokea Desemba 24, 2021 eneo la Kerege wilayani Bagamoyo mkoani Pwani, wakati Kisena alipokuwa akisafiri na familia yake kuelekea kwao Kilimanjaro, akitumia gari lake binafsi.
Katika ajali hiyo, basi la Kilimanjaro aina ya Scania liliacha njia na kuliparamia gari la Kisena aina ya Toyota Landcruiser.
Mtoto wake mmoja wa kike aliyekuwa na umri wa miaka 16 alifariki dunia na Kisena, mkewe na mtoto wao mwingine wa kiume walinisurika japo walipata majeraha.