Kilimanjaro: Diwani atoweka baada ya fumanizi

Linguistic

JF-Expert Member
Mar 16, 2021
3,671
8,237
Na Gaudence Msuya, Hai

DIWANI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Kata ya Lundugai wilayani hapa, Azizi Simbano anadaiwa kutoweka kwa kinachoelezwa kuwa ni kukimbia fumanizi la mke wa kiongozi wa chama hicho.

Aidha, CCM wilaya imetangaza msako dhidi ya diwani huyo aliyefumaniwa kwa nadhiri kwamba, apatikane asipatikane lazima hatua kali za kinidhamu zichukuliwe dhidi yake.

Kwa mujibu wa taarifa ya tukio hilo lililothibitishwa pia na Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Hai, Waguba Madanda, diwani huyo ametoweka na hata simu yake haipatikani.

Madanda alisema diwani huyo alitoweka baada ya chama hicho kumdhamini kwa tuhuma za fumanizi la mke wa Katibu wa Siasa na Uenezi wa Kata ya Lundugai, Zebedayo Makalla na kuahidi kumlipa mwenye mke shilingi milioni 2.5 za ugoni.

Alisema tangu atoe ahadi hiyo ni mwezi sasa hajaonekana na namba yake ya simu ikipigwa haipokelewi, hali inayoonesha kuwa amekimbia tuhuma hizo.

Madanda alisema wao kama chama wanaendelea na hatua stahiki baada ya zile za awali kukwama.

Makalla alikitaka chama hicho kuhakikisha diwani huyo analipa pesa zake ili akatafute mke mwingine kwa kuwa aliamua kumwachia tangu siku ya tukio, hivyo kwa kuwa chama kilibeba dhamana kwa kiongozi huyo, basi kisimamie haki itendeke.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Lundugai, Charles Kondema alisema matukio ya diwani huyo yamewachosha kwa kuwa, hana maadili mema na haitendei haki nafasi hiyo kwa matendo yake.

Gazetibla RAIAMWEMA Toleo la Jumanne Machi 29, 2022, Ukurasa wa 3
 
CCM mbona ni jadi yao hiyo nenda dodod kwenye mkutano mkuu uone
Na Mbowe akaiga akawa anawabandua wabunge viti maalumu mpaka wakamzarau wakaingia bungeni kwa nguvu alipotqkawasiende sasa hivi anahaha kuwatoa bungeni mwisho wake atajifanya anahekia atasema amewasamehe kumbe hakuna kitu wamemshinda nguvu
 
Na Gaudence Msuya, Hai

DIWANI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Kata ya Lundugai wilayani hapa, Azizi Simbano anadaiwa kutoweka kwa kinachoelezwa kuwa ni kukimbia fumanizi la mke wa kiongozi wa chama hicho.

Aidha, CCM wilaya imetangaza msako dhidi ya diwani huyo aliyefumaniwa kwa nadhiri kwamba, apatikane asipatikane lazima hatua kali za kinidhamu zichukuliwe dhidi yake.

Kwa mujibu wa taarifa ya tukio hilo lililothibitishwa pia na Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Hai, Waguba Madanda, diwani huyo ametoweka na hata simu yake haipatikani.

Madanda alisema diwani huyo alitoweka baada ya chama hicho kumdhamini kwa tuhuma za fumanizi la mke wa Katibu wa Siasa na Uenezi wa Kata ya Lundugai, Zebedayo Makalla na kuahidi kumlipa mwenye mke shilingi milioni 2.5 za ugoni.

Alisema tangu atoe ahadi hiyo ni mwezi sasa hajaonekana na namba yake ya simu ikipigwa haipokelewi, hali inayoonesha kuwa amekimbia tuhuma hizo.

Madanda alisema wao kama chama wanaendelea na hatua stahiki baada ya zile za awali kukwama.

Makalla alikitaka chama hicho kuhakikisha diwani huyo analipa pesa zake ili akatafute mke mwingine kwa kuwa aliamua kumwachia tangu siku ya tukio, hivyo kwa kuwa chama kilibeba dhamana kwa kiongozi huyo, basi kisimamie haki itendeke.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Lundugai, Charles Kondema alisema matukio ya diwani huyo yamewachosha kwa kuwa, hana maadili mema na haitendei haki nafasi hiyo kwa matendo yake.

Gazetibla RAIAMWEMA Toleo la Jumanne Machi 29, 2022, Ukurasa wa 3

Kazi iendelee:

IMG_20220329_110130_732.jpg
 
Chama chetu kinapakwa matope sana sijui tufanyeje, lakini nadhani kuna tatizo mahali, kuna waimbaji toka Ruvuma wameimba hivi majuzi na mbele yao alikuwepo mwanachama mwenzetu
 
Kwa mujibu wa taarifa ya tukio hilo lililothibitishwa pia na Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Hai, Waguba Madanda, diwani huyo ametoweka na hata simu yake haipatikani.
Sasa hili ni suala binafsi naona chama kisijiingize huko
 
Na Gaudence Msuya, Hai

DIWANI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Kata ya Lundugai wilayani hapa, Azizi Simbano anadaiwa kutoweka kwa kinachoelezwa kuwa ni kukimbia fumanizi la mke wa kiongozi wa chama hicho.

Aidha, CCM wilaya imetangaza msako dhidi ya diwani huyo aliyefumaniwa kwa nadhiri kwamba, apatikane asipatikane lazima hatua kali za kinidhamu zichukuliwe dhidi yake.

Kwa mujibu wa taarifa ya tukio hilo lililothibitishwa pia na Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Hai, Waguba Madanda, diwani huyo ametoweka na hata simu yake haipatikani.

Madanda alisema diwani huyo alitoweka baada ya chama hicho kumdhamini kwa tuhuma za fumanizi la mke wa Katibu wa Siasa na Uenezi wa Kata ya Lundugai, Zebedayo Makalla na kuahidi kumlipa mwenye mke shilingi milioni 2.5 za ugoni.

Alisema tangu atoe ahadi hiyo ni mwezi sasa hajaonekana na namba yake ya simu ikipigwa haipokelewi, hali inayoonesha kuwa amekimbia tuhuma hizo.

Madanda alisema wao kama chama wanaendelea na hatua stahiki baada ya zile za awali kukwama.

Makalla alikitaka chama hicho kuhakikisha diwani huyo analipa pesa zake ili akatafute mke mwingine kwa kuwa aliamua kumwachia tangu siku ya tukio, hivyo kwa kuwa chama kilibeba dhamana kwa kiongozi huyo, basi kisimamie haki itendeke.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Lundugai, Charles Kondema alisema matukio ya diwani huyo yamewachosha kwa kuwa, hana maadili mema na haitendei haki nafasi hiyo kwa matendo yake.

Gazetibla RAIAMWEMA Toleo la Jumanne Machi 29, 2022, Ukurasa wa 3
Akamatwe akafungwee huyo na uongozi Avuliwe,. tumechoka.
 
Back
Top Bottom