Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,502
- 9,282
Bangi mbaya. Jamaa alidhani anachoma migodi ya AcaciaHasira nyingine ni hasara
Saa sita usiku jua Kali hivyo. Kweli Moshi ni Mji wa kitalii
Tukio hilo limetokea juzi majira ya saa 6:00 usiku katika Kijiji cha Sawe, Kata ya Masama Mashariki, Tarafa ya Masama, Wilaya ya Hai.
Labda familia yake ile yeye serikali imempa ifadh kituo cha policeHASIRA HASARA SASA HIVI ANALALA KWA MAJIRANI
Miss Natafuta unacheka Mungu anakuona ujueahahaaaa
hahaha mkuuLabda familia yake ile yeye serikali imempa ifadh kituo cha police
umeona picha ya saa sita usiku moshi?Daah kwelo pombe sio chai
Saa sita usiku jua Kali hivyo. Kweli Moshi ni Mji wa kitalii
MWENYEKITI wa Kitongoji cha Ituunyi, Kata ya Masama Mashariki, Wilaya ya Hai, Wariading’u Anasa, ameiteketeza nyumba yake kwa moto wa mafuta ya petroli, baada ya mkewe kuchelewa kumfungulia mlango.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro (ACP), Koka Moita, alisema mwenyekiti huyo aliamua kuchukua mafuta ya petroli yaliyokuwa kwenye pikipiki yake na kuichoma nyumba hiyo kwa hasira kwa kile alichodai mkewe alionyesha dharau.
“Kwa bahati nzuri hakuna vifo wala madhara kwa binadamu yaliyotokea, lakini huyu Mwenyekiti baada ya kufanya tukio hilo alifanikiwa kutoroka, Jeshi la Polisi lilifanikiwa kumkamata katika Kijiji cha Uswaa nje kidogo ya Kijiji cha Sawe akiwa amejificha,” alisema Moita.
Inadaiwa kuwa chanzo cha tukio hilo ni ulevi uliopindukia wa mtuhumiwa na wakati anatekeleza kusudio lake alikuwa amelewa na kumlalamikia mke wake kuwa alichelewa kumfungulia mlango.
Tukio hilo limetokea juzi majira ya saa 6:00 usiku katika Kijiji cha Sawe, Kata ya Masama Mashariki, Tarafa ya Masama, Wilaya ya Hai.
Wakati huo huo, Shaban Juma, amefariki dunia jana, baada ya kuangukiwa na mtungi wa zege katika jengo la ghorofa 11 linalojengwa na kumilikiwa na mfanyabiashara, Fredrick Shoo.
Mtungi huo ulianguka na kusababisha kifo, baada waya ngumu inayotumika kupandishia mtungi huo juu ya ghorofa kukatika katika ghorofa ya nane.
Jengo hilo refu kuliko yote katika mji wa Moshi, linajengwa na Kampuni ya Wachina katika Barabara ya Market Road.
Chanzo; IPPmedia