Kilimanjaro: Ateketeza nyumba baada mkewe kuchelewa kumfungulia

miss zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
2,768
2,000
MWENYEKITI wa Kitongoji cha Ituunyi, Kata ya Masama Mashariki, Wilaya ya Hai, Wariading’u Anasa, ameiteketeza nyumba yake kwa moto wa mafuta ya petroli, baada ya mkewe kuchelewa kumfungulia mlango.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro (ACP), Koka Moita, alisema mwenyekiti huyo aliamua kuchukua mafuta ya petroli yaliyokuwa kwenye pikipiki yake na kuichoma nyumba hiyo kwa hasira kwa kile alichodai mkewe alionyesha dharau.

“Kwa bahati nzuri hakuna vifo wala madhara kwa binadamu yaliyotokea, lakini huyu Mwenyekiti baada ya kufanya tukio hilo alifanikiwa kutoroka, Jeshi la Polisi lilifanikiwa kumkamata katika Kijiji cha Uswaa nje kidogo ya Kijiji cha Sawe akiwa amejificha,” alisema Moita.

Inadaiwa kuwa chanzo cha tukio hilo ni ulevi uliopindukia wa mtuhumiwa na wakati anatekeleza kusudio lake alikuwa amelewa na kumlalamikia mke wake kuwa alichelewa kumfungulia mlango.

Tukio hilo limetokea juzi majira ya saa 6:00 usiku katika Kijiji cha Sawe, Kata ya Masama Mashariki, Tarafa ya Masama, Wilaya ya Hai.

Wakati huo huo, Shaban Juma, amefariki dunia jana, baada ya kuangukiwa na mtungi wa zege katika jengo la ghorofa 11 linalojengwa na kumilikiwa na mfanyabiashara, Fredrick Shoo.

Mtungi huo ulianguka na kusababisha kifo, baada waya ngumu inayotumika kupandishia mtungi huo juu ya ghorofa kukatika katika ghorofa ya nane.

Jengo hilo refu kuliko yote katika mji wa Moshi, linajengwa na Kampuni ya Wachina katika Barabara ya Market Road.

Chanzo; IPPmedia
 
majoto

JF-Expert Member
Jul 19, 2013
2,040
2,000
Ana pepo la wivu. Kwa wivu wake alihisi kuna linalofanyika ndani. Bila kufikiria, hasira plus wivu akachoma nyumba.

Hilo ni pepo na ndio linasababisha mauaji ya mapenzi
 
Mkwawe

JF-Expert Member
Jun 10, 2016
1,769
2,000
Kuna wakati nahisi wanaume tuna matatizo sana kuliko tunavyowachukulia wanawake

sijawahi kusikia wanawake wakishiriki kufanya matukio ya ajabu kama haya
 
CaptainDunga

JF-Expert Member
Jul 17, 2009
1,550
2,000
Hakuna cha ulevi wala kufanyiwa dharau hapo ni mawazo mabaya ya WIVU tu ndo yalikuwa yana msumbua........sasa atakula alipopeleka MBOGA....dadeki.
 
Akili Unazo!

JF-Expert Member
Feb 18, 2009
3,450
2,000
MWENYEKITI wa Kitongoji cha Ituunyi, Kata ya Masama Mashariki, Wilaya ya Hai, Wariading’u Anasa, ameiteketeza nyumba yake kwa moto wa mafuta ya petroli, baada ya mkewe kuchelewa kumfungulia mlango.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro (ACP), Koka Moita, alisema mwenyekiti huyo aliamua kuchukua mafuta ya petroli yaliyokuwa kwenye pikipiki yake na kuichoma nyumba hiyo kwa hasira kwa kile alichodai mkewe alionyesha dharau.

“Kwa bahati nzuri hakuna vifo wala madhara kwa binadamu yaliyotokea, lakini huyu Mwenyekiti baada ya kufanya tukio hilo alifanikiwa kutoroka, Jeshi la Polisi lilifanikiwa kumkamata katika Kijiji cha Uswaa nje kidogo ya Kijiji cha Sawe akiwa amejificha,” alisema Moita.

Inadaiwa kuwa chanzo cha tukio hilo ni ulevi uliopindukia wa mtuhumiwa na wakati anatekeleza kusudio lake alikuwa amelewa na kumlalamikia mke wake kuwa alichelewa kumfungulia mlango.

Tukio hilo limetokea juzi majira ya saa 6:00 usiku katika Kijiji cha Sawe, Kata ya Masama Mashariki, Tarafa ya Masama, Wilaya ya Hai.

Wakati huo huo, Shaban Juma, amefariki dunia jana, baada ya kuangukiwa na mtungi wa zege katika jengo la ghorofa 11 linalojengwa na kumilikiwa na mfanyabiashara, Fredrick Shoo.

Mtungi huo ulianguka na kusababisha kifo, baada waya ngumu inayotumika kupandishia mtungi huo juu ya ghorofa kukatika katika ghorofa ya nane.

Jengo hilo refu kuliko yote katika mji wa Moshi, linajengwa na Kampuni ya Wachina katika Barabara ya Market Road.

Chanzo; IPPmedia

Haki ya Mungu Huko Moshi kila Jinsi ni Shida kuwa na uvumilivu
 
Sakayo

JF-Expert Member
Sep 10, 2015
56,561
2,000
Wasisingizie pombe bhana, kilichomfanya akimbie ni nini!!!! Angesubiri sasa kama ni pombe kweli, mjinga kabisa alikuwa wapi mpaka akute familia imelala....
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom