Kilichowaliza Tizeba na Kimei kinawaliza wangapi?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
25,838
Reaction score
50,543
Dr. Charles Tizeba na Dr. Charles Kimei ni watu wawili tofauti wenye Majina yanayofanana na ni wabobevu kwenye fani wanazozitumikia. Lakini kwenye siku za hivi karibuni wote wawili wamemwaga chozi hadharani.

Tizeba na Kimei wote wamelizwa na hali ya kuona wana wajibu fulani wa kutimiza lakini wanakwamishwa na ukata wa fedha. Watu wazima kama kina Tizeba kulia hadharani si jambo dogo hata kidogo.

Tizeba na Kimei ni watu maarufu na ndiyo maana habari zao za kulia zimesikika sana nchini mwetu. Jee ni watanzania wangapi wanalizwa na hali kama waliyoiona kina Tizeba na Kimei?
 
Mkuu kwa hali ilivyo sasa.

Hakuna Mtanzania wa kawaida ambae halii hivi sasa kwa machungu ya madhila yanayosababishwa na hali halisi ya maisha yaliyoletwa na Utawala huu wa awamu ya 5..

Sikuwahi kusikia Kiongozi wa level ya Tizeba au Kimei akilia kwenye awamu zilizopita.
 
Utasikia wanakwambia 'tatizo ni Tundu Lissu na Chadema' wanashirikiana na Mabeberu kuhujumu serikali ya ccm.

Baada ya hapo serikali ya ccm inaenda kutembeza bakuri kwa Mabeberu haohao!!
 
Watu wanalia siyo kwa sababu hawana chakula bali wanalilia kwa kujiuliza ni nini tulichofanya hadi kustahili uongozi wa namna hii! Uongozi ambao kazi yake kubwa ni kuua uchumi na kusababisha mateso kwa raia wa sasa na vizazi vijavyo?

Taifa letu lilikuwa kwenye ukungu, tukiamini siku moja tutakuwa kwenye mwanga mwangavu, cha ajabu limeingia kwenye giza totoro.
 
wanaua uchumi eti wale wasiowapenda wasifaidi akili za mwafrika hizo
 
Kinana ka-step down akihofia kuja kulia hadharani kama Tizeba na Kimei. Siku Jiwe litakapokaa pembeni, ni lazima liburuzwe the Hague.
 
Mkuu kwa hali ilivyo sasa.

Hakuna Mtanzania wa kawaida ambae halii hivi sasa kwa machungu ya madhila yanayosababishwa na hali halisi ya maisha yaliyoletwa na Utawala huu wa awamu ya 5..

Sikuwahi kusikia Kiongozi wa level ya Tizeba au Kimei akilia kwenye awamu zilizopita.
Niwe mkweli ktk tawala zoote zilizopita sikuwahi kuishi maisha mazuri..Ila awamu hii maisha nayafurahia sana pesa yaonekana tena sana hadi nashangaa wanaolalama.Chamsingi ni juhudi zako tu
 
Dr. Charles Tizeba na Dr. Charles Kimei ni watu wawili tofauti wenye Majina yanayofanana na ni wabobevu kwenye fani wanazozitumikia. Lakini kwenye siku za hivi karibuni wote wawili wamemwaga chozi hadharani.

Tizeba na Kimei wote wamelizwa na hali ya kuona wana wajibu fulani wa kutimiza lakini wanakwamishwa na ukata wa fedha. Watu wazima kama kina Tizeba kulia hadharani si jambo dogo hata kidogo.

Tizeba na Kimei ni watu maarufu na ndiyo maana habari zao za kulia zimesikika sana nchini mwetu. Jee ni watanzania wangapi wanalizwa na hali kama waliyoiona kina Tizeba na Kimei?
Walitoa chozi?
 
Back
Top Bottom