Kilichopungua kampeni za arumeru | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kilichopungua kampeni za arumeru

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by Mtaka Haki, Mar 18, 2012.

 1. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #1
  Mar 18, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Napenda kuvipongeza vyama vyote vinavyoshiriki katika kampeni za uchaguzi Jimbo la Arumeru kwa kujitahidi kuyajua na kuyasema mahitaji ya msingi na kero za watu wa eneo husika.
  Kuna mambo ambayo kwa maoni yangu yamepungua. Kuna mambo ya kitaifa ambayo ni muhimu yakaongezwa kwenye yale ya sehemu husika. Tatizo kubwa la watanzania ni elimu. Kwa kuwa wengi hawajihusishi na matatizo yaliyo mbali na eneo lao, hii haiwafanyi wanasiasa kutokutumia fursa za kampeni kuelimisha jamii katika yale ya kitaifa.
  1. Suala la Ufisadi ni la kitaifa na ni la kuelewesha wanakijiji. Watu watu watakaoanza kuelewa na kuwa na chachu ya kuuchukia ufisadi na kuusema.
  2. Mifano ya mambo ambayo bado ni ya muhimu hata vivjijini kuyasikia ni
  a) Serikali ya leo watu wanaiba na mabilioni mpaka nchi nyingine inatusaidia kufuatilia wizi lakini walioiba wameachwa.
  b) Matatizo ya umeme kuwa wa gharama kubwa ni kwa sababu ya ubadhirifu wa mabilioni.
  c) Serikali iliyoko madarakani kuiba mabilioni za Epa, Meremeta, Tangold bila hatua yoyote kuchuliwa.

  3. Chama tawala kinakumbatia ufisadi na wale wanaoonekana kuupinga wanaundiwa tuhuma au wanaondolewa, kama ilivyokuwa kwa spika wa Bunge.
  4. Utamaduni wa kujiuzulu haupo kwa sababu hatuna serikali inayowajibika.

  HAYA HAPO JUU NA MENGINE NDIYO YALIYOMFANYA DR. SLAA KUWA MAARUFU. MREMA ALIPATA UMAARUFU KWA KUPINGA MAOVU. SOKOINE ALIPENDWA KWA KUPINGA MAOVU. WANAOCHUKIA MAOVU SIKU ZOTE WATAENDELEA KUWA WENGI.
  Wako watu wengi na mimi ni mmojawapo sababu pekee ya kutokuiunga mkono CCM ni hizo nilizozitaja hapo juu. Bado sio mwanachama chochote cha siasa lakini sababu pekee ya kuvutwa na CHADEMA ni hiyo hapo juu.
   
 2. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #2
  Mar 25, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Bado tunatamani ujumbe wa ufisadi, umuhimu wa upinzani, ubovu wa sera zilizotufikisha hapa visikosekana hata mara moja. Huu ndio mtaji endelevu wa kufungua macho. Pia nashauri msichukue muda mwingi kujibu mambo ya kibinafsi yanatoletwa na watu waliotarajiwa kuwa na heshima kama Mkapa nk wakati walitarajiwa kuleta sera.
   
 3. Chakunyuma

  Chakunyuma JF-Expert Member

  #3
  Mar 25, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 811
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  I do support what you have said.
   
 4. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #4
  Mar 25, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Thanks ( Hopefuly someone in the campaign will take a note at least for the remaining days)
   
 5. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #5
  Mar 25, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,330
  Likes Received: 3,535
  Trophy Points: 280
  Mwigulu Nchemba amesema ukimwaga sera za aina hiyo kule Arumeru hupati watu kwenye mikutano...

  Dawa yao ni kupiga maji taka halafu kama hawaeleweki unanunua shahada zao. Huo ndio mwenendo mpya wa siasa za nchi hii
   
Loading...