Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 2,439
- 6,691
Wakuu,
Rais wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO), Geofrey Kiliba, amewataka vijana nchini kutambua nafasi yao katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, akisema matokeo ya uchaguzi huo yatakuwa na mchango mkubwa katika mustakabali wao.
Akizungumza katika kipindi cha Maswali na Majibu kinachoongozwa na mtangazaji Wilberforce Ngoto kupitia Jambo TV, Kiliba amesema vijana wanapaswa kufuatilia kwa makini sera na ahadi zinazotolewa na wagombea, ili kutathmini uwezo wao wa kuzitekeleza kwa vitendo.
“Sisi kama vijana wa leo wa Kitanzania, lazima tujue mustakabali wa maisha yetu unategemea sana uchaguzi wa mwaka 2025. Misingi ya namna ya upatikanaji wa ajira, mazingira wezeshi ya kumuinua kijana na kumfanya awe huru inategemea sana mbegu inayopandwa na viongozi wetu,” amesema