GE2025 Kiliba: Tumeshuhudia Nepal na Madagascar vijana wameiua nchi yao wenyewe

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mafyangula

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2025
Posts
505
Reaction score
887
Mwenyekiti wa Kampeni ya Kitaifa ya Mama Asemewe Bw. Geofrey Kiliba amesisitiza umuhimu wa kila mmoja kuwajibika kulinda amani ya Tanzania, akitaka pia wale wote wenye maoni na hisia tofauti kutumia njia rafiki za kutaka mabadiliko badala ya maneno ya kichochezi na yenye kuhatarisha amani na hatua za maendeleo zilizopigwa pamoja na ustawi wa jamii.

Kiliba ametoa wito huo leo Jumanne Oktoba 14,2025 wakati alipozungumza na wanahabari Mkoani Kagera akiwasihi Vijana pia kujiepusha na kutumia kwenye matendo ovu na kuwataka kujifunza kukosa umakini na umoja kwa Vijana wa Nepal na Madagascar kulivyozisambatarisha nchi hizo na kuua ustawi wa jamii yake.

"Hatukatai kuwa Tanzania yetu sio peponi tupo duniani na mojawapo ya sifa ya uwepo wetu duniani ni pamoja na kukutana na kukabiliana na changamoto mbalimbali. Hatuna sababu ya kuua ama kudhohofisha msingi wa maendeleo tuliyonayo kwasababu ya madai ya kutatua changamoto zilizopo." Amekaririwa Kiliba akiwaambia wanahabari.

Ningekuwa karibu naye ningemshauri akae kimya hususani masuala ya kimataifa, siasa zake ni ngumu na zinahitaji wabobezi wa diplomasia
 
Mwenyekiti wa Kampeni ya Kitaifa ya Mama Asemewe Bw. Geofrey Kiliba amesisitiza umuhimu wa kila mmoja kuwajibika kulinda amani ya Tanzania, akitaka pia wale wote wenye maoni na hisia tofauti kutumia njia rafiki za kutaka mabadiliko badala ya maneno ya kichochezi na yenye kuhatarisha amani na hatua za maendeleo zilizopigwa pamoja na ustawi wa jamii.

Kiliba ametoa wito huo leo Jumanne Oktoba 14,2025 wakati alipozungumza na wanahabari Mkoani Kagera akiwasihi Vijana pia kujiepusha na kutumia kwenye matendo ovu na kuwataka kujifunza kukosa umakini na umoja kwa Vijana wa Nepal na Madagascar kulivyozisambatarisha nchi hizo na kuua ustawi wa jamii yake.

"Hatukatai kuwa Tanzania yetu sio peponi tupo duniani na mojawapo ya sifa ya uwepo wetu duniani ni pamoja na kukutana na kukabiliana na changamoto mbalimbali. Hatuna sababu ya kuua ama kudhohofisha msingi wa maendeleo tuliyonayo kwasababu ya madai ya kutatua changamoto zilizopo." Amekaririwa Kiliba akiwaambia wanahabari.

Ukiwa mwanaume, then kwa bahati mbaya mshipa wa kupeleka hewa kichwani kwenye ubongo ukawa umepitia kwenye njia ya haja kubwa...ndio matokeo yake haya!
 
Hajaona jinsi mtu mmoja alivyosaini mktaba wa Dola 30M kukodi software kutokea India ya kufuatilia umeme kukatika tu basi.
Unajua hii pesa ngapi imeua watu. Yaani sijui unajua kuwa watu wanakufa kisa hawaipati huduma muhimu mahala Fulani. Kuna binti anajiuza kisa Kuna mahala kiongozi akabofya remote
 
Back
Top Bottom