Kile tulichofikiri hakipo………..! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kile tulichofikiri hakipo………..!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Oct 21, 2011.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Oct 21, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Kabla ya ndoa, wanandoa huwa na ndoto tamutamu ambazo sio halisi kuhusu ndoa. Kwa kuwa tuna hizi ndoto tamu, tunapokuja kuingia kwenye ndoa na kugundua kwamba tulichofikiria hakipo, ndipo tunapoanza kuvunjika moyo na kujiuliza kama ndoa ina maana.

  Kwa kawaida tunachotarajia kukipata kabla ya ndoa, tunapoingia kwenye ndoa hatukipati na hili huvuruga kila kitu. Inaonekana kama matarajio ya wanaume siyo makubwa sana kama yale ya wanawake kabla ya ndoa.

  Huenda hili huchangia katika kuwafanya wanaume wasishangazwe sana na kile wanachopambana nacho baada ya ndoa.
  Inawezekana pia ni kwa sababu wanaume wameshika ‘mpini' kwenye masuala mengi ya kiuhusiano wakati wanawake wameshika kwenye makali.

  Hata hivyo badala ya wanandoa kukwaruzana kutokana na kukutana na hali ambayo hawakuwa wanaiota kabla ya ndoa, inabidi wajifunze maana ya ndoa wakiwa ndani ya ndoa yenyewe.
  Inabidi wakubaliane na yale ambayo hawakuwa wameyatarajia na kujifunza kupitia kwayo.

  Badala ya kukimbia hali halisi ya ndoa, ni vyema kujifunza na kuikubali, ni vyema kubadilika ili kwenda nayo na sio kutegemea hali hiyo ibadilike.
   
 2. GAZETI

  GAZETI JF-Expert Member

  #2
  Oct 21, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 3,561
  Likes Received: 1,070
  Trophy Points: 280
  Ahsante Mkuu!
   
 3. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #3
  Oct 21, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Mtambuzi yaani hiki ulicholiwekla leo hapa loh. Umenibamba. Nilikuwa namsikiliza Mch. Mwakasege on the same issue. Nimegundua kuwa inawezekana kabisa kuwa malengo ya mwanaume na mwanamke juu ya ndoa yanatofautiana kwa kiwango kikubwa. Kuna wanaume wanaoamua kuoa kwa kuwa tu wamechoka kula chipsi vumbi mtaani, anaoa ili apate chakula cha nyumbani. Sasa mtu wa hivi no matter what happens kwenye ndoa yake ilimradi anapata chakula (ambacho hata msichana wa kazi can cook) yeye ni sawa tu. Inawezekana ni tofauti na mkewe ambaye alipoolewa lengo lake lilikuwa ni kumpata rafiki, mwenza ambaye atakuwa naye muda wote, washee stori za maisha n.k. sasa huyu mume anapokuwa sie kama anavyotegemewa, mke huumia sana.
   
 4. m

  mjasiria JF-Expert Member

  #4
  Oct 21, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 3,790
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Mimi sikuwa na ndoto tamu wala nini nilioa kutimizia wajibu tu.
   
 5. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #5
  Oct 22, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Wale waleeeee.................
   
 6. GAZETI

  GAZETI JF-Expert Member

  #6
  Oct 22, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 3,561
  Likes Received: 1,070
  Trophy Points: 280
  Kina nani?
   
 7. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #7
  Oct 22, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  MJ1, niliwahi kusema wakati fulani kuwa nimependa maneno yako haya:
  "......Marriage is like a Dance, No matter how the Music changes you keep on Dancing..."
   
 8. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #8
  Oct 22, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  wafanye nini na bigG imekwisha utamu
   
 9. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #9
  Oct 22, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  We nawe............. Si kina Mtambuzi!
   
 10. yahoo

  yahoo JF-Expert Member

  #10
  Oct 22, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 3,424
  Likes Received: 363
  Trophy Points: 180
  mimi nilioa kujipa uhakika wa "kunanihii", nilichoka kusubiri chini ya miti baa nk, mala mtu aje,mala *asije akwambie nilikua bize sana, wakati mashine imejikoki unaweza kubaka bure mtto wa mtu,au kuzaa na chizi.
   
 11. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #11
  Oct 22, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Mwee..!!!
   
 12. mka

  mka JF-Expert Member

  #12
  Oct 22, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 318
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hahahaahahahah
   
 13. M

  Mocrana JF-Expert Member

  #13
  Oct 22, 2011
  Joined: Sep 10, 2011
  Messages: 532
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  umenena vema, yani siku hizi ndoa zimekuwa kama ni fashion tu watu wanaagalia zaidi harusi na si ndoa, wasichana wanwaza na mie niolewe nisionekane kuwaniko nyuma, akili yote ikiwa kwenye siku ya harusi tu, na si maisha baada ya hapo, matokeo yake ukifika ndani ya ndoa ukakutana na misukosuko kidogo tayari ndoa inakuwa ndoana, tunasahau neno la Mungu linasema mwanamke mpumbavu hubomoa nyumba kwa mikono yake, mm naamini pamoja na kuwa mwanaume ni kichwa cha familia, Mungu alitupendelea wanawake akatupa uwezo mkubwa wa kumiliki familia zetu na ndio maana mwanamke asipokuwa stable kwenye nyumba ndoa lazima itayumba, ila kwa wanaume kama uliamua kuoa mana yake huyo ndiye mwanamke uliyemchagua hata kama utakta anamapungufu ni kazi kwako kumrekebisha kwa upole, chukulianeni mizigo yenu, upendo, msamaha viwe kama sala kwenu kulala na kumka na mtu maisha yako yote si kazi ndogo, lakini yahitaji uvumilivu na kuchukuliana, neno linasema enyi waume wapendeni wake zenu kama kristo alivyolipenda kanisa, palipo na upendo wa kweli amani na furaha itatawala, mana kama mmekuwa mwili mmoja sidhani kama mtu anaweza akauchukia mwili wake au akautesa, jamani tusifike mahali ukawa na ndoa za mikataba kama huko kwa wenzetu, ndoa na iheshimiwe na watu wote.
   
 14. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #14
  Oct 22, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  kwa hyo ulidhani waliooa wanafaidi kunanilii tu!pole kwa mkeo. Your not mature kaka
   
Loading...