Kila siku visingizio ni kazi

Kila siku visingizio ni kazi

Eliza Green

Member
Joined
May 30, 2016
Posts
16
Reaction score
14
Ndugu zangu wa forum naombeni ushauri,mimi ni binti wa miaka 21, niko kwenye mahusiano na mwanaume ambaye ni mchumba wangu bado ajanioa lakini tunaishi pamoja ni miaka 2 sasa na tunafanya kazi idara moja, na ninavyo ongea nina mimba yake ya miezi 7, kwa bahati nzuri au mbaya huyu mwanaume alipata uhamisho kutoka mkoa wa Singida akaamishiwa mkoani mbeya, na mimi kuniacha Singida tangu ameondoka kwenda mbeya mawasiliano yetu yamekuwa ya shida sana, ukiachana na hilo amekuwa ni mtu anaeonekana ataki mawasiliano na mimi ila anajilazimisha.

Anakuwa mkali kama simba ukimpigia simu bila kuwa na sababu za msingi, baada ya miezi kadhaa na mimi nikapata uhamisho kuamia mkoa wa jirani na yeye yaani Mkoani Songwe,ambapo nina uwezo wa kwenda na kurudi kutoka yeye alipo mpaka kwangu, lakini tangu nimefika kwake tunalala wote usiku bila hata kusex mpaka asubuhi na akiondoka hiyo asubuhi anarudi usiku saa 5, yaani ajui mimi nimeshindaje ?

Na ukizingatia hali niliyo nayo ya ujauzito napata shida sana, ananiambia mazingira ya kazi ya mkoa tuliokuepo na huo ni tofauti kwahiyo muda mwingi amechoka, tangu nimetoka singida mpaka mbeya ni miezi 4 sasa hatujawahi kusex Ingawa tunalala kitanda kimoja na ukimlazimisha anakwambia mwanamke gani unawaza mapenzi mida wote!

Na anadai nampa wasiwasi kwa kitendo cha mimi kumtaka kimapenzi ikafikia stage ananiita mimi malaya na wakati nimemtunzia penzi lake tangu amehama huo mkoa mpaka tumeonana, Je ndugu zangu ni kweli napendwa au nalazimisha penzi? Na je huyu mwanaume ana mapenzi ya dhati na mimi mpaka ananinyanyasa kihisia wakati nina mimba yake

NB:kuhusu matumizi na pesa kila ninacbotaka ananipa lakini ananinyima haki ya mimi kusema kweli nipo kwenye ndoa yenye furaha nisaidieni maana sijui cha kufanya!
 
Ningekua Mbeya au jirani ningekusaidia hilo tatizo lako, ila kwa sababu umelileta humu usijali ndugu zangu kina malyafare hawajawahi kuniangusha kwenye suala la kusaidia watu wenye tatizo kama lako ukizingatia wanashindia maparachichi. Ni matumaini yangu utahudumiwa vizuri na hutomsumbua tena mmeo kuhusu hilo tatizo lake.
 
Hii wiki imetawaliwa na mikasa ya mabinti kutoka kwa watu wao.

We rudi kwako, focus kwenye ujauzito. Jamaa mwangalie tu mpaka mtoto atakapozaliwa, asipobadilika ni-PM.
Mkuu kupitia hiii thread

Maajabu ya mimba ya huyu mwanamke

Alijibu mimba yake imemfanya awe Na ham sana Na mumewe lakini mume hataki hata kusikia

Me nahisi n vibweka vya ujauzito hebu atulie ajifungue then aangalie je kutakua Na mabadiliko au mambo ni yaleyale?
 
Ndugu zangu wa forum naombeni ushauri,mimi ni binti wa miaka 21, niko kwenye mahusiano na mwanaume ambaye ni mchumba wangu bado ajanioa lakini tunaishi pamoja ni miaka 2 sasa na tunafanya kazi idara moja, na ninavyo ongea nina mimba yake ya miezi 7, kwa bahati nzuri au mbaya huyu mwanaume alipata uhamisho kutoka mkoa wa Singida akaamishiwa mkoani mbeya, na mimi kuniacha Singida tangu ameondoka kwenda mbeya mawasiliano yetu yamekuwa ya shida sana, ukiachana na hilo amekuwa ni mtu anaeonekana ataki mawasiliano na mimi ila anajilazimisha ,anakuwa mkali kama simba ukimpigia simu bila kuwa na sababu za msingi, baada ya miezi kadhaa na mimi nikapata uhamisho kuamia mkoa wa jirani na yeye yaani Mkoani Songwe,ambapo nina uwezo wa kwenda na kurudi kutoka yeye alipo mpaka kwangu, lakini tangu nimefika kwake tunalala wote usiku bila hata kusex mpaka asubuhi na akiondoka hiyo asubuhi anarudi usiku saa 5, yaani ajui mimi nimeshindaje ? Na ukizingatia hali niliyo nayo ya ujauzito napata shida sana, ananiambia mazingira ya kazi ya mkoa tuliokuepo na huo ni tofauti kwahiyo muda mwingi amechoka, tangu nimetoka singida mpaka mbeya ni miezi 4 sasa hatujawahi kusex Ingawa tunalala kitanda kimoja na ukimlazimisha anakwambia mwanamke gani unawaza mapenzi mida wote! Na anadai nampa wasiwasi kwa kitendo cha mimi kumtaka kimapenzi ikafikia stage ananiita mimi malaya na wakati nimemtunzia penzi lake tangu amehama huo mkoa mpaka tumeonana, Je ndugu zangu ni kweli napendwa au nalazimisha penzi? Na je huyu mwanaume ana mapenzi ya dhati na mimi mpaka ananinyanyasa kihisia wakati nina mimba yake
NB:kuhusu matumizi na pesa kila ninacbotaka ananipa lakini ananinyima haki ya mimi kusema kweli nipo kwenye ndoa yenye furaha nisaidieni maana sijui cha kufanya!
Piga chini hamna mtu hapo, yaani miezi kadhaa hajaonana na wewe bado hajisikii ku-do nawewe. Hapa una sababu mbili za kupiga chini.

1.Kama amekaa miezi kadhaa mbali nawewe na hana hamu ya kufanya mapenzi nawewe it means alikua ana-cheat ndo maana hana usongo

2.Kama alikua ha-cheat wakati haupo atakua kapata u-hanithi ndiyomaana hawezi ku-do

Nakuja Songwe kikazi next week naomba uni-inbox namba zako ili nikifika tu nikutafute tuijadili vizuri hii changamoto iliyokukumba
 
Si ajabu aliomba uhamisho akukimbie kijanja wewe bado unajipelekesha, mwisho wa siku anaeumia ni wewe kwasababu mwanaume hakupi yale unayotegemea kutoka kwake. Shukuru Mungu kuwa una ajira. Anza ku tune your brain as a single mother and make preparations for your coming baby. Huyo mwanaume mtoe akilini mwako, utaona maisha yatakavyokuwa murua.
 
Si ajabu aliomba uhamisho akukimbie kijanja wewe bado unajipelekesha, mwisho wa siku anaeumia ni wewe kwasababu mwanaume hakupi yale unayotegemea kutoka kwake. Shukuru Mungu kuwa una ajira. Anza ku tune your brain as a single mother and make preparations for your coming baby. Huyo mwanaume mtoe akilini mwako, utaona maisha yatakavyokuwa murua.
Nimependa ushauri wako sky eclat
 
Back
Top Bottom