Kila nikijaribu kumsamehe/kuwasamehe nashindwa

NothinGold ]Daah, pole Sana mkuu, pia hongera kwa uwasilishaji mzuri wa bandiko!!

Kweli hii story imenigusa Sana Mimi km kijana, Tena sijaoa napata wakati mgumu Sana kuhusu ndoa ,

Kikubwa walee watoto vizuri kbsa, hao upande wa pili achana nao na jiepushe nao mbali sanaaaaa Tena sanaaaaa, Maana machungu,tabu na shida wanazopitia Sasa hata kwa mganga wanaweza enda kukuroga,

Mungu akutangulie ktk majukumu yako na akutunze na familia yako!!
 
Msamehe lakini msirudiane,anaweza kukumaliza.Msaidie sana pale inapowezekana.Pia nawewe muombe msamaha kwa kumkosea coz ww ndio uliesababisha familia kuvurugika.
 
Suala la kurudiana hilo lisiwepo ila tu huyu kaka anaweza kuwasamehe kimya kimya akaendela na shughuli zake

Mkuu, kwenye maisha sote tumetendwa uovu kila mtu anaona ni heri asisamehe tu lakini hatujui tusiposamehe moyoni bado wanakua wanaishi tena saa zingine nafsi hufurukuta kwa hasira lakini ukikubali hali na kusamehe unakua sawa moyoni huna kisasi tena
Apo mwanamke sidhani Kama anataka msamaha Bila kurudiana
 
Chuki ni mzigo ila tulipewa akili ya kujua jema na baya na kutoentertain ujinga wa watu flan kisa mapenzi apambane na hali yake
 
Dah! Kati ya nyuzi chache nilizozisoma mwanzo mwisho....pole sana bob.
Hongera kwa uvumilivu maana ingekuwa mimi Wala yasingefika huko kabisaa

Muhimu we wasamehe tu kwa ajili ya amani yako ya moyo Ila sio mrudiane endelea na yako
 
Suala la kurudiana hilo lisiwepo ila tu huyu kaka anaweza kuwasamehe kimya kimya akaendela na shughuli zake

Mkuu, kwenye maisha sote tumetendwa uovu kila mtu anaona ni heri asisamehe tu lakini hatujui tusiposamehe moyoni bado wanakua wanaishi tena saa zingine nafsi hufurukuta kwa hasira lakini ukikubali hali na kusamehe unakua sawa moyoni huna kisasi tena
Hakika!
Kuweka donge moyoni ni kujilisha sumu roho
 
Kama nikusamehe yaliyopita msamehe yaishe lakini usikubali akapata nafasi yakurudi kwenye maisha yako, kwanza mm ningewaambia watoto mama yao amekufa ili wasimtafute kabisa
 
Uneacha pointi muhimu sana. Umesema sababu kuu ni kukuta sms ya mchepuko wako, lakini nadhani kuna sababu zaidi ya hiyo. Hiyo sms ilikuwa sehemu ya kutokea tu. Naamini alikuwa na mtu (mchepuko) ukiomwingiza chaka.

Naomba kama unajua, sababu halisi ya kukutelekeza.

Bazazi!
 
Bonge la Hoja Kinzani

Bazazi
Daaaah....nmesoma kila neno uliloandika...ni uhondo juu ya uhondo....nashauri utoe kitabu kabisa ....

Hz ndoa hz duuh.....wanawake wasomi wasumbue, na wasio wasomi pia wasumbue...mambo n balaaa
 
Kidogo nitakuwa tofauti na kila mtu humu.

Kwanza nianze kwa kukwambia pumbavu! Pumbavu sana! Pumbavu tena!
Ukitembea na mchepuko mkeo alikua kakukosea nini? Umefanya kazi ya kuweka akili kwenye Mali ukasahau watoto wanahitaji malezi ya baba na mama na si ya bibi. Nikweli mkeo alikosea kwa hatua alizochukua baada ya wewe kutenda kosa ila unajua mkeo ni zaidi ya wewe unavyomwona mkeo? Huyo binti unaejivunia mzuri anamwita mkeo mama! Nafikiri unajua maana ya neno mama.

No matter what kwa wanao huyo ni mama yao, ukizingatia upendo wako kwa wanao utaanza na kulijua hilo utajua watoto wanahitaji uwepo wa mama kama wanavyohitaji uwepo wa baba pia. Nyote wawili hamjui watoto wanataka nini mnawaza Mali za dunia na starehe zenu, ndio maana yeye alikua bize na biashara kuliko watoto na wewe ulikua busy na kumvua chupi mchepuko pumbavu sana! Ndoa na iheshimiwe nakwambia hili kutoka moyoni pumbavu sana!

Kuna kitu kinaitwa malipizi ya dhambi hivyo ulikua kwenye malipizi ya dhambi na kadhalika mkeo nae kawa kwenye malipizi ya dhambi zake. Hakuna mtu mwenye haki kwenye hii dunia mrudushe mkeo kwako na chukua wanao mkae nao. Kubwa tu siku zote unapohama hama na mkeo shetani yuko mtaani anasaka wafwasi wake. Ndoa ni ndoa na ni above your emotions.

Samahani kama utahisi sielewi uliyopitia. Pumbavu sana.
 
Back
Top Bottom