Kila mwanakijiji alipata kitita cha elfu 10

Kila mwanakijiji alipata kitita cha elfu 10

JEKI

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2013
Posts
4,845
Reaction score
2,966
Umasikini kitu kibaya sana, jana nimemsikia mwenyekiti wa kijiji fulani akisifia mradi wa msitu una faida kwani wanakijijiji walitunza na kuja kuuza miti na kila mwanakijiji kuondoka na KITITA cha elfu kumi.

Jamani elfu 10 hapa mjini unafanyia nini? hadi mtu atambe kapata KITITA cha elfu 10, naomba ujumbe huu uwafikie wajumbe wa bunge maalumu la katiba, waje na katiba mwokozi kwa watu wetu vijijini, elfu 10 kwa watu kama kina mama la mama, Price, King'asti, miss chagga, @husniyo, utafiti, Kongosho ni ya kifurushi cha internet cha siku moja tu, wakati wenzao huko kijijini wakipata KITITA cha elfu 10 wataongea mwaka mzima.
 
Kwa maisha ya mjini hata kifurushi haitoshi mkuu, labda huko kijijini sijui wanafanyaje hadi wanaita KITITA
 
Kitita ninavyo fahamu mimi! Au walipewa jelo jelo
 
Kwa maisha yalivyo panda elfu 10 siyo chochote ila kwa ajili ya dhiki mtu wa kijiji awez kukataaa
 
Kwa kijijini inaweza ikawa kitita maana ukitaka kuchange usishangae unazunguuka kijiji kizima hupati change.
 
Ni kweli elfu kumi ni hela ndogo ila kinachonifurahisha ni dhana nzima iliyotumika kugawana pato la kijiji, kila mtu alipata hakuna kulalamika. Ingekuwa heri hata mapato ya gesi, dhahabu, utalii kila mtanzania mwenye umri kuanzia miaka kumi na nane pamoja na kufanyia maendeleo, kwa zingine angekuwa anavuta mshiko wake kila mwaka kama alivyopendekeza professa mmoja wa uchumi nimemsahau.
 
Miaka ya mwisho mwisho ya utawala wa muhammar ghadafi libya iliwahi kutenga sehemu kubwa ya bajeti ya nchi kwa ajili ya kuirudisha kwa wananchi, nadhani ghadafi alikuwa akijaribu kuona kama wananchi mmoja mmoja anaweza kuchangia uchumi wa nchi kutoka mifukoni mwao, au ndiyo kuwa shirikisha wananchi kwenye kuifaidi keki ya taifa,, ila hiki KITITA cha Ten sauzendi du!!!!!!!!!!
 
Ukimuona mtu anaiita shiling 10,000 tena ya kiTz "KITITA" basi umwombee pumziko jema na la haraka!!!!
 
ndiyo mkuu, kila mwanakijiji aliondoka na KITITA cha elfu 10.
Hii ni kudhihirisha jinsi wananchi walivyomaskini, elfu kumi wanaona ni kitita.

Wazee wa vijisenti na yule wa pesa ya ugoro natamani wangelielewa hili.
 
kijijini kitita cha elfu 10 mbona kinatosha sana.....!
 
so sad.... aisee ngoja niwawakilishe vyema kuna vijiji hela hawajui aisee
 
Hapa ndio tunapaswa kuelewa kuwa hali ya maisha ya mtanzania bado ni ngumu sana...sio ajabu ukaenda kijijiji na kukuta mtu anashindwa kununua pakti ya chumvi...ambayo kimsingi haizidi shs 300! Sembuse kukutana na shilingi 10,000? Hakika hiki ni KITITA kama sio BULUNGUTU kabisa...
 
Kwa upande wangu mimi,ninauponge huo uongozi wa kijiji kwa hatua hiyo walio fikia ya mgao wa 10000.kutoka mapatato ya kijiji,na kama sikosei ndio cha kwanza tz kwa wananchi wake kupata mgao wa mafao ya kijiji. Hongera sana uongozi wa kijiji,inaonekana hata wakipewa nchi tutafaidika kwa mengi ya rasilimali tulizo nazo,
 
Kijiji cha Msange Singida,
1.Guest Tsh 4000/-kwa siku
2.chai Tsh 1500/.
3.Lunch Tsh 2000/
4.Dinner Tsh 2000/
5.matunda/sigara tsh 500/
Kitita kimeisha kwa raha zako.
 
Nawalaumu sana nyie vijana mnaojiita wasomi mnapoenda likizo vijijini kwenu mnashindwa kutoa elimu ya uraia kwa watu waliokuzunguka mfano sasa hivi wanasiasa wanatumia kete ya barabara, maji, na umeme kama ngazi ya kuupata uongozi vijijini ilhali hizo huduma zinatakiwa lazima ziwepo kutokana na kodi anayolipa mwananchi na rasilimali zinazomzunguka zinatakiwa zimnufaishe kila mwananchi kwa kutambua umbumbu mwananchi wa kijijini aliokuwa nao wanatumia turufu hiyo kuwahadaa wananchi jamani tutoe elimu ya uraia ili vizazi vijavyo visijejiuliza kama enzi zetu walikuwa wakiishi binadamu wenye akili kama za wanyama.
 
Kweli maisha kiuchumi yapo tofauti miongoni mwa Watanzania, na ndio maana hata kuna maamuzi yanafanyika, watu wengine wanakuwa hawaelewi kwamba mtu kafanyaje uamuzi huo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom