Kila la kheri kwenu Morocco πŸ‡²πŸ‡¦ Algeria πŸ‡©πŸ‡Ώ

DesertStorm

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2015
Posts
3,184
Reaction score
2,597
Wale mnaowatakia ama kuwaombea mabaya waarabu waondolewe kwenye mashindano haya ya AFCON na wabakie weusi tu mmefeli, tena sio kidogo, hakunaga duaa mbaya kwa mwenzio na ikakubaliwa.... huo ni ubaguzi na chuki ya wazi kabisa, wewe kama una imani haswaa na khofu ya Mwenyezi Mungu huwezi kufanya huu ujinga kisa mpira tu, wengine mpaka wanatukana matusi, mara oh acha waarabu watoke wote sijawahi kuwapenda kabisa, oh Hawa mambuzi wa kiarabu hawatochukua chochote n.k hahhaaa mtu anaongea upumbavu mtupu anajiona ameongea point πŸ˜‚This is football bwana.

Hebu angalia hii clip ndio utaona ile haikua penati, mshkaji alianza kuzama/kujiangusha kabla jamaa la Morocco halijapushi for hand....Shida kuna watu mmejawa chuki na ubaguzi tu, tukubali tukatae wenzetu wametuacha mbali kisoka
Your browser is not able to display this video.

Kama mnakumbuka mamelodi walichotufanyia wanayanga mbona hamkuingiza ubaguzi kisa wale ni weusi na hawa ni weupe sio ila wote ni wa AfrikaπŸ˜‚πŸ˜‚ chuki ni mbaya sana, na ndio maana wenye chuki wengi wao huwa ni masikini sana

Mtawaombea sana mabaya ila ndio kwanzaa tunawapa credit wenye mpira wao, na hata ikitokea wametolewa basi sio rizki yao kutwaa kombe hilo na ndicho wanachoamini wao, na sio dua zenu hizo, hakuna duaa ya kumuombea mabaya mwenzio na ikakubaliwa, never!
 
Inaonekana una matatizo ya akili mzee wahi ukapate matibabu aisee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…