Kila la kheri Daktari Mashinji, watanzania wote tupo nyuma yako

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Kamanda, Mhe. Vincent Mashinji ambaye ni Katibu mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA amekuwa tishio jipya kwa utawala huu usiozingatia katiba ya nchi na sheria, ukiachilia mbali wanasiasa na wanaharakati mahiri na machachari ambao wamezoeleka au majina yao yapo Sana vinywani mwa wengi, mfano Mhe. Tundu Lissu (MB) ambaye ni Mnadhimu wa Kambi rasmi ya upinzani Bungeni na mwanasheria Mkuu wa CHADEMA pia ni Rais wa TLS, Mhe. Freeman Mbowe (MB) ambaye ni kiongozi wa upinzani Bungeni (nchini) na mwenyekiti wa CHADEMA nchini, na wengineo, ambao wamekuwa tishio hata kuikosesha usingizi serikali ya CCM na Magufuli, nitazungumza kwa uchache kuhusu Daktari Mashinji.

Mhe. Mashinji ni Daktari bingwa wa mgonjwa ya binadamu; msomi mwenye shahada moja ya udaktari (MD), shahada tatu tofauti za uzamili (Masters degree) na shahada moja ya uzamivu ya uongozi (PhD), mtafiti wa kujitegemea, mwenye karama ya uongozi na asiyeogopa chochote katika kuitetea nchi, wananchi na haki zao, amekuwa akifanya siasa zinazoidhoofisha CCM pamoja na serikali iliyopo madarakani, kwa kutekeleza majukumu yake ya kisiasa nchini kimkakati, chini kwa chini, ambapo siku moja atakayotoa maelekezo nchini, nchi nzima itasimama.

Daktari Mashinji, mzaliwa wa sengerema ukanda wa ziwa, ameweka mkazo juu ya suala la upatikanaji wa KATIBA mpya nchini, na amekuwa jasiri katika kuizungumza KATIBA ya nchi, tofauti na wengi wadhaniavyo. Dr. Mashinji alipokuwa mkoani Mwanza alielekeza kuwa kipaumbele Kikuu cha chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA ni KATIBA mpya, na aliapa kulihakikisha hilo suala la KATIBA mpya linafikiwa muafaka wa kitaifa. "Kipaumbele chetu ni katiba ya wananchi. Ni kitu cha kwanza tutakachokisimamia. Tunachohitaji kwa sasa ni kufumua mfumo wa kiutawala kwa kuwa kumekuwa na mwingiliano wa kimajukumu. Kingine ni kwenda kuuwezesha umma uweze kutambua haki zao na uwe tayari kutetea haki zao" alisema Daktari Mashinji.

CHADEMA kimewahi kuwa na makatibu wakuu watatu, kabla ya Daktari Mashinji, alikuwepo Bob Makani, akafuatiwa na Dr. Walid Amani Kabourou, Kisha Dr. Wilbroad Slaa, na sasa ni Dr. Mashinji, ambaye anao mfumo mpya wa kiuongozi, kukiimarisha chama kuanzia ngazi za msingi mpaka taifa, kukijenga CHADEMA kitaasisi zaidi na kukiandaa kukamata hatamu za dola na kuiongoza nchi.

Kumekuwepo na maneno ya chini chini, kwamba Mhe. Mashinji amekuwa kimya wakati nchi inaumizwa na watawala, wananchi wamekuwa wakihitaji uongozi wa CHADEMA utoe kauli, wananchi wapate kuamua juu ya uelekeo wa nchi kisiasa, maana hatima ya Tanzania ipo mikononi mwa watanzania wenyewe. Daktari Mashinji amekuwa akiwataka wanachama na viongozi wote wa CHADEMA nchini kujenga mifumo ya kitaasisi na kuiimarisha kwa kushirikiana na kushikamana, badala ya kuliacha jukumu Hilo kwa viongozi wachache.

Ikiripotiwa na mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa CHADEMA kamanda Tumaini Makene, mnamo tarehe 15 July 2017, Daktari Mashinji alikamatwa na jeshi la polisi akiwa mkoani RUVUMA kwenye shughuli za kichama, akiwa ameambatana na wabunge na viongozi wa chama mkoani humo, wakiwepo Mhe. Cecil Mwambe (MB) na Mhe. Sakuru (MB).

Mhe. Mashinji pamoja na kukamatwa, amekuwa jasiri na mwenye Ari na nguvu mpya, na amesema haiwezekani kuiacha demokrasia ya nchi ikichezewa, ilhali ili watanzania wapate maendeleo ni sharti kwanza wapate demokrasia ya kweli, hata akatoa mfano wa kumuachia shamba ngedere, mfano ambao haujawaacha salama watawala.

Kila la kheri Daktari Mashinji, watanzania wote tupo nyuma yako, M4C Daima.
 
Mashinji yupi? huyo amoeba ambaye miaka miwili sasa hata hajawahi ku-develop any credible political programme? Makubwa!
 
Until i see him fight, then i will accept what your saying. Otherwise its just a bluff like any other. The war zone is active now there is no need for underground operations, he should act immediately.
 
humu sikuhizi kumekuwa nakaugonjwa ka kuonyesha ukumbato wa siasa ktk mlengwa fulani!
 
Back
Top Bottom