Kila kitu marufuku, nchi haina wasomi?

Kila kitu marufuku, nchi haina wasomi?

hekimanyingi

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2013
Posts
679
Reaction score
573
Sasa imekuwa mazoea kila jambo hata lisokuwa na maana ni marufuku kwenye nchi ya Tanzania. Magari kuwa na 'tinted' nayo imekuwa marufuku. Sasa hata wataalama walioweka vioo hivyo hawana maana achilia mbali wanaopachika.

Tinted kwenye magari inachukuliwa leo kuwa ni uhalifu kwasababu tu askari wetu wamekosa ubunifu wa kuwabaini wahalifu pasipo kuangalia faida kama kulinda faragha (privacy) ya mtu, kuzuia jua na kadhalika. Wakati huo huo wasomi wapo, viongozi wapo ila wapo kimya. Hii ni sawa na kusema nyumba zisiwekwe madirisha ya tinted au pazia kwakuwa wahalifu wanajificha na hili halina muda mrefu litapigwa marufuku.

Tunakosa ubunifu, nchi nyingi zina uhalifu na zilikuwa na uhalifu lakini hawana marufuku nyingi kama huku kwetu kwakuwa wanafanya kazi kwa weledi, wanabadili mbinu za kuwabaini wahalifu bila kuathiri maisha ya watu. Wakati umefika, wasomi kutokukaa kimya kwa kila marufuku. Haya mambo madogo tunayokatazwa leo kwa sababu za mbayuwayu kisha tunakaa kimya, yatakuja makubwa nayo tutakaa kimya.

Swala la msingi, tinted kwenye magari ina faida gani? Hasara zake nini? Na wenzetu wanafanya nini kupambana na uhalifu bila marufuku ya tinted?

Kwa maoni yangu, ni kuwa ubunifu wa kupambana na kuzuia uhalifu umekosekana sasa tunasingizia marufuku. Ni sawa na kusema watoto wa kike wasizaliwe kwa sabubu wanabakwa, au wa kiume kwasababu wanalawitiwa.

Tunahitaji kutathmini hizi marufuku.
 
Hadi CCM ikitoka madarakani ndo Watanzania watafunguliwa macho! maana ujinga wetu ndo unasababisha yote hayo, hakuna uongozi wa sheria, mtu akisha kuwa kiongozi basi anajiona yupo juu ya sheria....wananchi wenyewe majinga tupu, shida kidogo mnawategemea viongozi wasolve matatizo. Tungejifunza kuwadharau hawa viongozi wangejifunza kitu. Lakini akija kiongozi watu wanajazana barabarani utafikiri wanamsubiri Yesu! Pumbavu sana, huwa natamani sana nimiliki AK-47. Kila siku ni marufuku, mwishoni watatuambia "Kunya kwa siku ni mara moja tu au hakuna kupumua leo"
 
Yupo mengi yanayochochea uhalifu kuzidi tinted. Pikipiki - boda boda zina mchango mkubwa kwenye uhalifu.
 
Hizo zote ni dalili za kushindwa kazi. Wanashindwaje kuwakagua waliomo ndani ya hizo gari mpaka wapige marufuku kwa watu wote. Yaani wapo tayari kuwanyima haki wengi kwa sababu ya wachache. Viongozi wa hii nchi ni kero kubwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
anataka cheo huyu kama mwenzake FWAKENI

be___blessed
 
Hiyo ni kuingilia maisha ya watu binafsi, serikali inashindwaje kuwabaini wahalifu hadi kuzuia vioo tinted kwenye magari, hii maana yake ni kwamba serikali imekubali kushindwa na majambazi na badala yake wameamua kujificha kwenye kivuli cha vioo tinted

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa imekuwa mazoea kila jambo hata lisokuwa na maana ni marufuku kwenye nchi ya Tanzania. Magari kuwa na 'tinted' nayo imekuwa marufuku. Sasa hata wataalama walioweka vioo hivyo hawana maana achilia mbali wanaopachika.

Tinted kwenye magari inachukuliwa leo kuwa ni uhalifu kwasababu tu askari wetu wamekosa ubunifu wa kuwabaini wahalifu pasipo kuangalia faida kama kulinda faragha (privacy) ya mtu, kuzuia jua na kadhalika. Wakati huo huo wasomi wapo, viongozi wapo ila wapo kimya. Hii ni sawa na kusema nyumba zisiwekwe madirisha ya tinted au pazia kwakuwa wahalifu wanajificha na hili halina muda mrefu litapigwa marufuku.

Tunakosa ubunifu, nchi nyingi zina uhalifu na zilikuwa na uhalifu lakini hawana marufuku nyingi kama huku kwetu kwakuwa wanafanya kazi kwa weledi, wanabadili mbinu za kuwabaini wahalifu bila kuathiri maisha ya watu. Wakati umefika, wasomi kutokukaa kimya kwa kila marufuku. Haya mambo madogo tunayokatazwa leo kwa sababu za mbayuwayu kisha tunakaa kimya, yatakuja makubwa nayo tutakaa kimya.

Swala la msingi, tinted kwenye magari ina faida gani? Hasara zake nini? Na wenzetu wanafanya nini kupambana na uhalifu bila marufuku ya tinted?

Kwa maoni yangu, ni kuwa ubunifu wa kupambana na kuzuia uhalifu umekosekana sasa tunasingizia marufuku. Ni sawa na kusema watoto wa kike wasizaliwe kwa sabubu wanabakwa, au wa kiume kwasababu wanalawitiwa.

Tunahitaji kutathmini hizi marufuku.
Mkuu umesema vizur sana. Tunapoelekea watapiga marufuku kuendesha gari ukiwa umepandisha vioo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wangeachukua mfano huu,kuna dawa nyingi zina athali kwa binadamu, lakini kwasababu zinaponya wengi na kuwadhuru wachache zinaruhusiwa kutumika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom