Kila kitu kina mwanzo na Mwisho

bryan2

JF-Expert Member
Jun 8, 2016
3,321
4,671
Kipindi cha nyuma kuna kituo kimoja cha Television kilikua kinapenda sana kuonyesha ni jinsi gani Waafrika hatupendani.

Walikua wakionyesha jinsi Sisi Wenyewe tunavyofanyiana ukatili,Tukiuana bila sababu zozote,kupeana vilema vya Maisha bila sababu zozote,watoto kuachwa yatima baada ya wazazi wao kuuliwa bila sababu zozote.

Walikua wakionyesha ni Jinsi Gani watu wa Angola kipindi kile cha JONAS SAVIMBI wakipata mateso bila kuwa na hatia,Nlikua na umri mdogo kipindi kile ila siwezi kusahau siku nimeangalia kile Kipindi Nikaona mamia ya watu wakiwa wamekufa na kulala barabarani huku malori yakipita na kuwakusanya nlipata mawazo mengi sana juu ya zile picha za Maiti.

Nikawaza ivi ni madaraka tu au kuna kingine?

Akaja Mwingine tena FODAH SANKOH wa liberia huyu naye hivyo hivyo akimaliza watu wake wasiokuwa na Hatia,

Mohamed Farah Idid mbabe wa vita mwingine tena huyu naye akimaliza wanachi wake bila sababu zozote zile,Nikajiuliza kwanini Hawa watu hawaogopi Damu za binadamu wenzao na wao walijua wataishi Milele juu ya uso wa Dunia hii?

Ushauri tu tunavyowatendea wenzetu tujue kuna kesho na keshokutwa na hakuna aijuae kesho yake itakuaje tuwe na Amani na watu wote hapa duniani tunapita tuu.
 
Back
Top Bottom