beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,879
- 6,356
Mwenyekiti CCM, Rais mstaafu Jakaya Kikwete, amewaomba wazee kote nchini, kumuunga mkono Rais John Magufuli katika uongozi wake ili kumpa moyo wa kuwatumikia Watanzania.
Alisema, kipindi ambacho Dk Magufuli ameingia madarakani hadi sasa ni mda mfupi, hivyo si vema kuanza kudodosa na kulaumu panapopwaya, badala yake Wazee na watanzania kwa jumla wazidi kumuunga mkono ili kumtia moyo wa kutekeleza yote aliyokusudia kuyafanya kwa manufaa ya taifa.
Kikwete alitoa ombi hilo alipokuwa akizungumza katika mkutano na wazee wa Mkoa wa Singida, ambapo alisema kuwa kuongoza bila ushauri wa wazee nchi inaweza kuyumba. "Kuongoza nchi bila wazee mambo hayaendi vizuri na ukikosa mzee kwenye jahazi wapiga makasia vijana wanaweza kuanza kuzozana na chombo kwenda mrama, lakini wakiwepo wazee watawaongoza vizuri na chombo/ nchi kwenda salama". Alisema Kikwete huku akishangilia na wazee.
Si Kila mzee ni mwasisi wa chama, kila mwenye mvi na mwasisi, wengine wameingia kwenye chama wazee. Alisisitiza kwamba ukitaka nchi itulie kamata wazee, lakini ukiongoza nchi kwa kutumia vijana pekee nchi inaweza kuyumba, na itafika mahali mtakosa mahali pa kushika. Alisema kuwa hata yeye kwa mara ya kwanza .alipokwenda kuomba ubunge jimboni kwake Bagamoyo, Pwani aliunda kamati ya wazee ambayo ilimsaidia sana.
Wazee ni sehemu ya matumaini ya chama na Serikali, panapokuwepo wazee hapaharibiki jambo. "Nawashukuru sana wazee endeleeni kukijenga chama na kuiunga mkono Serikali inayoongozwa sasa na Dk John Magufuli." Alisisitiza Kikwete na kuongeza kuwa, "Hata kwenye chama chetu tumeunda Baraza la Washauri la Wazee wasitaafu, ambapo wengi walipinga, hata hao wazee tuliowataka waunde baadhi yao walipinga, lakini mwisho walikubali kwa masharti kwamba wawe wanaitwa panapotokea jambo kubwa litakalohitaji ushauri wao."
Alisema mmoja wa viongozi aliyekuwa msitari wa mbele kuunda baraza hilo, alikuwa Rais msitaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa ambaye alitoa ushauri wa kuitwa kutoa ushauri panapotokea jambo kubwa na kwamba hata wakitoa ushauri, viongozi waliopo madarakani wawe hiari kuukubali au kuukataa'.
Aliwataka wazee kuendelea kuiunga mkono serikali ya sasa ambayo kwa hivi sasa imetimiza muda mfupi wa miezi mitatu ambaye ni sawa na mtoto mdogo anayekua. Alisema kuwa Jambo kubwa ni kuwaunga mkono, kuliko kuwalaumu ama sivyo watavunjika moyo, ndani ya miaka mitano itakuwa hasara. watieni moyo ili wajiamini wahudumie vizuri zaidi ili nchi isonge mbele kimaendeleo.
Kikwete alisisitiza kuwa hata yeye akitakiwa kwenda kutoa ushauri atakwenda, na akiwa na jambo la kushauri atakwenda pia, lakini aliwaasa kuwa si kila jambo wazee watake kwenda kutoa ushauri, itachelewesha mambo mengi.
Chanzo: Michuzi