Kikwete wa 10 barani Afrika

Na tanzania ni nchi ya ngapi kiuchumi Afrika ? Au imepanda/imeporomoka mpaka kuwa ya ngapi kiuchumi ?
Je mfumuko wa bei umeshuka kwa asilimia ngapi ?Au je ni nchi ya ngapi kwa kudhibiti rushwa ?thamani ya pesa ikoje ,hali ya maisha ya wananchi wake nikiwemo mimi na wewe ,majomba,wapwa na wajukuu zetu zikoje,wanakwenda choo mara ngapi kwa wiki ?wakiugua
wanachimba mizizi au wanatibiwa hospitali.

Waambie watupe taarifa kwa maswali hayo hapo juu.

unazifahamu criteria walizotumia?
 
Kwani hamjui na hao wanaofanya tafiti wanaandika ili na wao wakalambe miguu ya hao jamaa. Sasa mbona na mshikaji wake wa Bondeni hamshangai amepataje wa sita sijui wakati kila kosa mbaka na kubaka analo. Nyie bwana acheni utani huyu mjamaa ni wa mwisho tu ila tu appearance labda mpaka na watafiti wanakoshwa nalo. Angekuwa Slaa hapa mpaka namba mbili au mmoja angeshika kwa performance yake

Padrimofia disease
 
Sina shaka na JK kuwa wa 10 katika bara ambalo una marais kama akina Bhagbo, Kibaki, Mgabe, Zenawi, Al Bashir, n.k. Maana hata ukienda katika shule zile ambazo hazijawahi kutoa hata mtoto mmoja kwenda sekondari tangu zianze, lazima wa kwanza, wa pili, wa tatu na wa mwisho utawapata KWA MAANA unaweza kuwa wa kwanza katika kundi la wabovu ila huyo wa mwisho kwenye kundi bovu ni balaa!


Wangesema JK ni 100 kwa ubora Duniani hapo ningechanganyikiwa lakini kuwa wa 10 Afrika sina tatizo kwa vile inafahamika kabisa kuwa Marais wazuri katika maana ya uongozi wenye upeo na dhamira njema katika Afrika hawawezi kuzidi 5.

again ANTIJAKAYA DISEASE
 
Hivi Jarida la East African credibility yake ipo wapi? Hayo ni magazeti ya Propaganda ya Nationmedia hayana ustaarabu yanatumika na serikali ya Kenya! tuwe waangalifu nayo hasa tukiangalia interest za wamaliki wake Tanzania tukianza na Prince Aga Khan!
 
Anastahili jamani,tusikatae sababu ya itikadi,ushabiki na mzugo wa kisiasa.

Kwa wachovu hata angekua wa kwanza hamna kitu. Hivi matumbo yetu yanashiba TZ na watoto wetu wanapata lishe? JK akifikia hilo lengo hapo ndo tutaona umaana wa yeye kua raisi wa KUMI Afirika kwa utendaji bora hasa baada ya CHAMA chao kua madarakani miaka yote hii.
 
again ANTIJAKAYA DISEASE

JK yeye ndo kashika funguo wa huko ambako sote tunataka kwenda, sasa kama tunaona hatufiki hata baada ya kupita miaka mingi ni dhahiri tutapata ANTIJAKAYA DISEASE. Hasa baada ya mpaka sasa tunachoona ama kupewa na JK ni maDOWANS tu.

Tunategemea wote, pamoja nawe, tukipata huo ugonjwa wa ANTIJAKAYA itasaidia sana kumchangamsha JK. Kama bado habadiriki baada ya wote kupata huo ugonjwa, sioni kwa nini CDM isipewe huo ufunguo wa kutupeleka huko ambako sote tunataka kwenda.

Binadamu wana utashi wa kufikiri. Wanapopinga utawala dhaifu wa JK ni kwa kua wamefikiri, wanapofikiri wewe unaita 'again ANTIJAKAYA DISEASE' - huu pia msamiati mzuri tu.
 
Tungepewa terms of reference tungejadili kwa mapana. Inawezekana kabisa vigezo vyao ni tofauti na ambavyo mnajadili. Kumbe kwa vigezo vyao angestahili hata kushika nafasi ya kwanza
 
Back
Top Bottom