Kikwete vs wafanyakazi

Zawadi Ngoda

JF-Expert Member
Aug 13, 2009
3,804
1,871
Jaribio la Rais Kkwete la kutingisha kiberiti cha wafanyakazi lilifanikiwa, lakini joto la maisha ya wafanyakazi bado liko palepale. Swali tunalojiuliza watazamaji wa mechi hiyo ni nini kilichomo katika mioyo wa wafanyakazi au nini kinachofuata?

Wafanyakazi walikatishwa tamaa sana na mlipuko wa JK, kwani vitisho alivyovitoa viliwakumbusha enzi ya 'Chama chashika hatamu' au Unyerere Nyerere design. Leo ni miaka kadhaa toka tuanzishe vyama vingi, isitoshe uchaguzi upo karibu ni wapi JK amepata ubavu wa kutamka maneno mazito kama hayo. Kwa ufupi ukimuangalia vizuri katika hotuba ile, alitawaliwa na kutokujiamini, woga, hasira na simanzi.

Hasira na simanzi za JK ZILITOKANA NA kukatishwa tamaa na yeye mwenyewe jinsi alivyoshindwa kutekeleza ahadi yake ya MAISHA BORA KWA WATANZANIA WOTE IKIWA PAMOJA NA WAFANYAKAZI. Leo tunahesabu siku chache tu za kipindi chake cha mwisho na maisha ndio magumu zaidi. Woga watokana na kutojua ni nini hatima ya mgogoro huo, hasa akizingatia kuwa uvumilivuy wa WAtanzania karibu unakwisha. Kutokujiamini, hakujua na bado mpaka leo hajui kama alichukua hatua sahihi katika kutatua tatizo hilo, hasa akizingatia kuwa uchaguzi u puani na wafanyakazi ni nguzo kubwa ya TEGEMEO LA ccm.

Jibu la Wafanyakazi katuiika hotuba hiyo ilikuwa kutoweka mguu barabarani na kuelekea kazini. Kwa nini waliamua hivyo? Jibu ni rahisi kuwa bado mambo hayajawafikia Shingoni au uvumilivu bado upo. Lakini hali halisi si hiyo, kwani hata baada ya hapo hakuna mfanyakazi asiyeacha kulalamika kuwa mshahara hautoshi. Ni dhahiri kuwa mshahara wa mtanzania hautoshi kabisa, kwa sababu panga pangua huwezi ukabajeti 80 000 sh kwa mwezi, au kwa mwalimu wa Sekondari aliyefuzu chuo kikuu na kupata shahada yake ya kwanza na kupewa 300 000 kwa mwezi ni utani mkubwa sana. Sasa JK yakwake ameshasema, ya wafanyakazi ni yapi?

Wafanyakazi bado wananafasi kubwa ya kumchonga JK afike pale wanapotaka. Kwa mfano uchaguzi u karibu, kwa nini wafanyakazi hususan walimu wasitumie kura yao ya VETO kumtoa JK ikulu? Hapa pana hitaji roho ngumu, kasababu hawa CCM watakuja na ahadi nono zitazowahadaa wafanyakazi. Unapopata nafasi ni lazima uitume, na safari hii wafanyakazi wananafasi ni muhimu wasonge mbele.

Katika hili ni lazima CHAMA CHA WAFANYAKAZI kiwe wazi, kuwa ni chama kipi inakiunga mkono. Chama cha wafanyakazi kina haki ya kuwashawishi wanachama wake kukipigia kura kile cha ambacho kikiingia madarakani kitasikiliza matakwa yao. Na kwa maana hiyo ni lazima izungumze na wapinzani na kandikishiana mkataba leo juu ya vipi marekebisho ya mishahara yatakuwa ikiwa wakiingia madarakani.

Mechi hii ni lazima matokeo yake yapatikane, na wafanyakazi ni lazima washinde. Wakati ni huu, ama za Chama tawala ama za Wafanyakazi. Wakati mwingine inabidi kuonyeshana misuri, na huu ndio wakati muafaka kwa Wafanyakzi. Ushindi ni lazima upatikane. Wafanyakazi OYEEEEEE!
 
Back
Top Bottom