Nina swali rahisi tu kwa Mwenyekiti Wa CCM
Katika mchakato wa utiaji nia hadi sasa, bado sijaona mwanamke hata mmoja aliyejaribu kufanya hivyo. Je Rais wangu, bado mfumo wetu wa kidemokrasia haujatuwezesha kuwa na wanawake majasiri, wenye uwezo wa kutuongoza?
Mfumo wetu wa Viti-Maalumu haujatuzalishia wanawake wenye uzoefu na wawezao kufanya kazi za kiuongozi?
Jamani, wanawake mko wapi? Mbona nyinyi mnabaki wa kupiga vigelegele tu kila ifikiapo wakati wa uchaguzi? Kwanini mnaruhusu mfumo-dume kuendelea kutia mizizi?