Kikwete udini ameukuta

Kikwete udini ameukuta

Status
Not open for further replies.

abdul 28

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2012
Posts
325
Reaction score
38
Masuala ya kuchinja yalianza kwa mwinyi yakajibiwa kirahisi na kuitwa mzee ruhsa

masuala ya oic yalianza tangu utawala wa nyerere mkapa mwinyi yakajibiwa kirahisi

waisilamu kuto kuwa na imani na necta tangu utawala wa nyerere mwinyi mkapa

masuala ya kutopeleka maendeleo mikowa ino waisilamu wengi mtwara lindi tanga tabora
tangu nyere mkapa na mwinyi

muungano tangu utawala wa nyerere mwinyi mkapa kero zilitatuliwa kirahisi

misamaha ya kodi kwa kanisa tangu utawala wa nyerere mwinyi mkapa

kikwete ni rais alieleta uhuru wa mtu kusema kile anacho taka hivyo ndio watu wanasema yale yoto yalio ndani ya vifua vyao
kikwete inaonekana wazi kywa ni rais anae taka kutatuwa matatizo ya muungano kupitia katiba mpya
nani alifikiria kama kutatokea mageuzi haya

kikwete ni mstaarabu wa bpwani hivyo munae mchukia tizameni mafaniukio yake kwenye elimu ya juu na vyoo vya sayansi
hivyo masuala ya dini na kero zote ziko mikononi mwa warioba

warioba ndie mtatuzi wa kero hizi akicheza nazo basi tanganyika damu itamwagika ikiwa kwa udini au siasa chafu
warioba kazi kwako
 
Ndugu zang kuna issue ambayo iko hot sn currently kwamba JK ana udini.Binafsi naona hana udini kwani amekuwa akishiriki mambo mbalimbali ktk dini zote.Watanzania tuache kulaumu tufanye kazi zetu za kimaendeleo.
 
This is Holy Cra.p
Wasubiri Ndugu zako waje Ku Support huu Upuuzi..
 
Aisee kumbe??Watanzania wa leo unafikiri unaweza ukaja na hoja nyepesi hivi??Hatuoni,hatujui kuchambua mambo eti??Kati ya dhambi itakayomtafuna Mr.Dhaifu ni hii ya udini.Hilo hata yeye analijua.Hotuba yake ya aliyotoa ilikuwa ya kinafki maana mchezo anaujua vizuri sana.
 
Mkuu Ngoja asubiri Ndugu zake wenye Taahira ya akili kama yeye waje kum Support.
 
Ndugu zang kuna issue ambayo iko hot sn currently kwamba JK ana udini.Binafsi naona hana udini kwani amekuwa akishiriki mambo mbalimbali ktk dini zote.Watanzania tuache kulaumu tufanye kazi zetu za kimaendeleo.

Unajua kosa lililopo mnabuni mikakati huku mmeunderate watu na kuwaona wote hi wale mnaofaulisha pasipo kujua kusoma wala kuandika.

Labda hii ungeipeleka kwa wenye upeo wa hao mnaowatengeneza ili mzidi kuwatawala ungepanda chati.

Ila kwa hapa nachelea kwamba unatafuta orodha ya watu wa kung'oa meno na kucha. Please tumia njia nyingine.
 
Ninavyomuona mimi rais wa tanzania katika hawamu zote hajawahi kuwa mdini. Hila watanzania wa sasa wanataka rais atende vile wanavyotaka. Mimi nasema rais wangu endelea kuitetea katiba yetu na utamaduni wetu watanzania wa utawala wa sheria. Urais ni taasisi ya dola hivyo lawama za udini kwa rais hazina mashiko. Watanzania kuweni na uzalendo katika hili la dini hotuba ya rais isibezwe hata kidogo. Viongozi wa dini hubirini watu kuacha maovu kama vile mmomonyoko wa maadili na kushuka kwa moyo wa uzalendo kwa baadhi watanzania. Hakuna rais ambaye katika nchi yake amefanikiwa kuwafanya wananchi wake wote kuwa na kipato sawa. Tufanye kazi usiku na mchana maisha yatakwenda vema. Mataifa ya iran, china,korea kz na japan wamefanikiwa kwa kufanya kazi ya kufa na kupona. Matatizo yetu yakutofikiria namna ya kujitoa katika wimbi la umaskini wa kipato, ndiyo yanatufanya kuleta hoja dhaifu za udini, ushirikina na ukanda. Watanzania wenzangu tutumie mitandao hii ya kijamii zaidi kupeana mbinu za kuondokana na ufukara tulionao na si kujadili hayo mambo ya kufikirika.
 
mkuu ngoja asubiri ndugu zake wenye taahira ya akili kama yeye waje kum support.
ninashaka na kule ulikolelewa, elimu yako pia akili yako. Neno taahira ni kashfa kwa wana jf wenzako. Naomba uwende kwenye nyumba yako ya ibada waumini wa kweli wakakuombee!
 
Hata mwizi akiiba akakamatwa akipelekwa polisi au mahakamani hubisha kuwa hajafanya hivyo. vivyo hivyo na watuhumiwa wengi hata ambao waonekana wazi wazi. Hili la udini ndio kabisa usitegemee mtu akubali kuwa ni mdini.

KUJITETEA TU KUWA SIO MDINI NI DHAHIRI TOSHA KUWA KUNA TATIZO.

kama sio mdini wala huna haja ya kuwaeleza watu kuwa wewe sio mdini
 
kama udini unavyowa-backfire na huu ujinga wa utekaji*mauaji ya raia*matumizi ya vyombo vya usalama kwa manufaa ya chama* na vinginevyo ,vyote vita backfire na hamtaweza kurudisha wakati nyuma ili mrekebishe makosa
 
Tatizo ni uisilamu wake mbegu mnayoipanda leo siku moja mtaivuna
 
Tatizo ni uisilamu wake mbegu mnayoipanda leo siku moja mtaivuna

Mfano wa udini ni kama Huyu hargeisa, ana udini, hakujawahi kutokea rais tanzania akawa na tabia hizo, Kikwete aliharibu kwenye kampeni akisaidiwa na mkapa kwa kuzungumzia udini kwenye majukwaa maana ilisababisha watu waanze kuhisi kuna tatizo na ndipo hali ilipoharibika, lakini kiutendaji mimi ni chadema damu kwa maana ya mpinzani wake lakini nasema toka moyoni KIKWETE HANA UDINI.!
 
Kila mtu ana dini na anaruhusa ya kuwa na dini, nadhani ni afadhali kuwa na rais anayeipenda dini yake kuliko kuwa na rais asiye jali wala kuhofu kuwa zaidi yake kuna Mungu, muhimu tu asivunje katiba kuathiri dini nyingine..
tatizo la serikali yake imeshindwa kudhibiti wachochezi wa udini, amekuwa mpole hata kwa mambo ambayo dhahiri yanaweza kuharibu taifa kirahisi kabisa, wenzake akina nyerere na mwinyi walizikabili chalenge za namna hii kabla watu hawajafikia mahali pa kuuamini uongo kuwa ndo ukweli na kuleta bughudha kwa jamii nzima
 
Ndugu zang kuna issue ambayo iko hot sn currently kwamba JK ana udini.Binafsi naona hana udini kwani amekuwa akishiriki mambo mbalimbali ktk dini zote.Watanzania tuache kulaumu tufanye kazi zetu za kimaendeleo.
Jamani ndugu Take home siwezi kujua unawakilisha kundi gani la WaTZ - kizazi kipya? kizazi kizee? wasomi? wambumbumbu? mafisadi? walalahoi? mateja? nk - ni vigumu kuelewa mnachomoka wapi na kuja na hoja kama hizi nyepesi. Watu wenye uelewa hawajali whether or not JK anashiriki mambo yote kwenye misikiti, makanisa, majumba ya mfalme, hekalu. Hawajali anasali msikiti gani. Hayo ni yake binafsi. Anayo haki kabisa ya kusali kwenye msikiti wo wote na kushiriki au kutoshiriki shughuli mbali mbli za makanisa na misikiti. Ugomvi wetu na masikitiko yetu ni kwamba nguvu alizopewa kikatiba kama Rais anaweza kabisa kuzitumia kuturejesha kule ambapo Watanzania wa dini zote waliheshimiana (ilikuwa ni aibu mtu kusimama hadharani na kuanza kukashfu na kukejeli imani ya mtu mwingine) kama yeye mwenyewe anavyokiri katika malalamiko yake. Enzi ambazo hapakuwepo na watu wazima wenye akili mbovu za kuwa-set watoto wadogo wakojolee Kurani ili wapate mahali pa kuanzia vurugu! Rais na serikali yake wanao uwezo mkubwa sana wa kuzuia haya yote anayosimulia. Tunachoshindwa kuelewa ni kwa nini aje kulialia kwa wananchi ambao nao wanamlilia kwa kuamini kuwa anao uwezo wa kukomesha uhuni huu- sio kama Kikwete bali kama Rais Kikwete (serikali)!!!
 
kikwete ni rais alieleta uhuru wa mtu kusema kile anacho taka hivyo ndio watu wanasema yale yoto yalio ndani ya vifua vyao

kikwete ni mstaarabu wa bpwani hivyo munae mchukia tizameni mafaniukio yake kwenye elimu ya juu na vyoo vya sayansi
hivyo masuala ya dini na kero zote ziko mikononi mwa warioba

warioba ndie mtatuzi wa kero hizi akicheza nazo basi tanganyika damu itamwagika ikiwa kwa udini au siasa chafu
warioba kazi kwako

no comment!
 
kabla ya kuweka uzi,pitia mara 2 unaweza ukapoteza maana nzima ya ujumbe kwa kukosea maneno kidogo tuu
 
kabla ya kuweka uzi,pitia mara 2 unaweza ukapoteza maana nzima ya ujumbe kwa kukosea maneno kidogo tuu

Mie ujumbe nimeuelewa na hasa ikizingatiwa kuwa Jf haina ubaguzi ali mradi mtu ana kimchina chake au kompyuta na net, basi!!! Ruksa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom