Kikwete tumekukosea nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete tumekukosea nini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Technician, Jan 23, 2012.

 1. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #1
  Jan 23, 2012
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  KIKWETE TUMEKUKOSEA NINI?

  Josephat Isango  HUENDA kuna mambo tumemkosea Rais Jakaya Kikwete ndiyo maana analipa kisasi. Haiwezekani Watanzania mkakataa ukweli huu, hata kama mkikataa, mbona inaonyesha kuwa serikali ya Kikwete ndivyo imedhamiria?

  Kosa liko wapi, kwetu au kwake? Je, tulimchagua Kikwete kwa hasara yetu? Je, tujutie sasa kumchagua kiongozi huyo na serikali yake kuwa madarakani? Yawezekana kweli tumekosea sehemu fulani na ndiyo maana tunaadhibiwa na serikali yetu.
  Je, hata serikali haina huruma ya kawaida angalau itusamehe tu? Na kama imekosa huruma inaendelea kutuangamiza hivi, mbona ni sisi ndio tulioiweka, kwani aliyeiweka hana nguvu ya kuitoa?

  Aliyekusanya hana nguvu ya kutawanya? Aliyepanda hana uwezo wa kuvuna? Unyonge wetu huu mpaka tufanyiwe haya unatokana na nini? Tuna Tanzania nyingine kuliko hii ambayo kwa sasa tunaichezea jinsi kila mmoja anavyojisikia?
  Tujikumbushe tena, labda tumesahau Nyerere alivyofundisha. Alisema kuwa: "Tumeonewa kiasi cha kutosha, tumenyonywa kiasi cha kutosha, tumenyanyaswa kiasi cha kutosha na tumepuuzwa kiasi cha kutosha. "Ni unyonge wetu ndio uliotufanya tuonewe, tunyonywe, tunyanyaswe na tupuuzwe. Sasa tunataka mapinduzi ili tusionewe, tusinyanyaswe na tusipuuzwe tena."

  Mwalimu alizungumza haya akimaanisha kuwasaidia Watanzania kujitambua, alikuwa akipinga mfumo wa maisha ya aina hii, ambayo kwa sasa sisi tunayaishi, bila kuyapenda lakini tunayavumilia na yanataka kuzoeleka kuwa ndio mtindo wa kawaida kwa serikali yetu na chama kilichoiunda.

  Maisha yetu yote yamekuwa yakidhibitiwa na watu ambao mtazamo wao ni kujinufaisha, kutuibia, kutukandamiza, kutulipa mishahara midogo tena hata hiyo midogo mara nyingine hatupewi au inacheleweshwa sana. Bahati mbaya sana kwa miaka 50 tangu tupate uhuru Chama cha Mapinduzi (CCM) ndio wamekuwa wakiamua kuwe na aina gani ya serikali, shughuli za kiuchumi – kama zipo, elimu watoto wetu wapate. Katika muktadha huu wao ndio wenye maamuzi ya mwisho. Wao ndio wamefinyanga sura ya Watanzania wa kizazi hiki.

  Tumekuwa na Watanzania waliopigika kimaisha lakini wakitishiwa tunu ya Umoja na Amani ili wasipigane. Hata kama wananyanyaswa wataambiwa tusipoteze amani ya Tanzania ambayo naamini ipo kwa Watanzania wote si kwa baadhi ya watu.

  Rais Kikwete, je, kuna sehemu tutakuwa tumeikosea serikali yako kiasi cha kustahiki manyanyaso haya, uonevu huu au hivi vinafanyika kwasababu ya unyonge wetu? Hivi unyonge wetu ndio unasababisha serikali iamue kutoza kodi kubwa kwenye mafuta, vyakula sasa bei yake haikamatiki na kadiri siku zinavyosonga ndivyo inavyoongezeka.

  Serikali imeamua kutuua kidogo kidogo. Inapandisha bei ya vitu ili watakaoshindwa kuvipata wakaibe na wakiiba watu wanajichukulia sheria mkononi na kuwaua wenzao. Serikali imepandisha bei ya umeme licha ya kuwa nishati hiyo si ya uhakika na haijawafikia Watanzania wengi, serikali haitoi sababu ya kueleweka ya kupandisha umeme, haisemi kama imeongeza wafanyakazi katika sekta hiyo, haisemi kama imeboresha upatikanaji wa umeme kwa wananchi wake.
  Hatuambiwi kama mashine mpya zimenunuliwa au mishahara ya wafanyakazi wa Tanesco imepandishwa lakini inasema kuwa imepandisha gharama za umeme, Je, ni kwanini, kwa ajili ya nani?

  Kimsingi maamuzi haya hayajaangaliwa kikamilifu kama yanamsaidia mwananchi au yanamnyonga? Wananchi nao wamekubali kunyongwa au wanakandamizwa kimabavu kwa kuwa hawajui wajibu wao wa kuiwajibisha serikali?
  Serikali ya Kikwete itaacha lini utaratibu wa kupitisha sheria, sera na matamko mbalimbali ambayo yapo kwa ajili ya kunufaisha tabaka fulani tu?

  Umeme wa Tanzania unapatikana kwa kutumia nguvu za maji, makaa ya mawe na mafuta. Suala la maji katika maeneo kunapozalishwa umeme kuna mafuriko, maana yake hakuna shida ya uzalishaji, je makali ya umeme yamepungua? Kama hayajapungua ni kwanini?

  Mikataba aliyoahidi Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, wakati wa kipindi cha Bunge ilikuwa ni kuwadanganya Watanzania. Tunatofautishaje mikataba ya ukoloni iliyokuwa ya kinyonyaji na hii ya siku hizi ndani ya serikali?
  Tunawezaje kumkejeli Chifu Mangungo wa Msovero, kwa kutia sahihi mkataba wa kilaghai miaka ya 1880 na kuwapa wakoloni mkataba wa miaka 99 kumiliki ardhi ya nchi yake, chini ya mpelelezi, Dk. Karl Peters. Vivyo hivyo alivyofanyiwa Chifu Lobengula na Mzungu, Cecil Rhodes, huko Rhodesia. Lakini, kuna tofauti gani kati ya mikataba ya sasa kati yetu na wawekezaji tunaoambiwa na serikali na ule wa Chifu Mangungo na Karl Peters?

  Ukweli unabaki kwamba kina Chifu Mangungo, Lobengula na Kinjikitile walipogundua wamefanyiwa hila walipambana. Viongozi wetu wasomi wa Havard wanatetea wawekezaji matapeli; inavyoonekana, mikataba ya wawekezaji hao inaandikwa na viongozi hao kwa manufaa binafsi na ya matapeli wabia wao.

  Kutokana na hali hiyo, serikali ya Kikwete imeshindwa hata kudhibiti bei ya unga, sukari, mafuta na sasa imeamua kuonyesha kuwa inaweza kutufanyia lolote na sisi tusionyeshe kupinga au kuikasirikia. Kama tunaona kinachofanywa na serikali ni kizuri, kwanini tulalamikie ugumu wa maisha na ubadhirifu wa mali za serikali unaofanywa na viongozi tuliowapa dhamana ya kutuongoza? Hatujui tumekosa wapi lakini serikali inatuadhibu, serikali nayo imeonyesha haina nia ya kutusamehe. Maisha ni magumu kiasi cha kutosha, nini hatima ya Watanzania?

  Nimefanya mazungumzo na mfanyakazi mmoja wa kampuni ya ulinzi mkoani Singida ambaye mshahara wake ni sh 80,000 ambazo hamzitoshi hata kufikisha nusu mwezi. "Gunia la mkaa ni sh 13,000, debe la mahindi sh 8,000, sukari kilo sh 2500, kusaga debe moja ka mahindi ni sh 1,000, mafuta ya taa lita moja inauzwa sh 2200, mchele kilo moja sh 2400, maji ya kutumia ndoo moja inauzwa sh 500, kodi ya nyumba sh 5,000, umeme sh 5,000," anasema. Mfanyakazi huyo anasema katika hali ya kawaida anashindwa kumudu maisha licha ya kufanya kazi aliyonayo, anauliza serikali imemkosea nini kiasi cha kuweka mazingira magumu ya kuishi kwa raia wake?

  Akaniuliza kuwa kama yeye mwenye kazi na analipwa mshahara mambo anayaona magumu kiasi hicho, je, yule asiye na kazi wala kipato cha maana anaishije? Anahitimisha mjadala wetu kwa kunihoji: "Serikali imeamua kuwakomoa wananchi wake kwa kupandisha bei ya kila kitu hata umeme ambao hatungetarajia upande katika musimu huu wa mvua?"

  Serikali inanunua umeme kutoka kwa kampuni za kigeni kwa kutumia fedha za kigeni (dola), inawauzia Watanzania kwa kutumia fedha ya hapa nchini ambayo kila siku inashuka thamani kila kukicha. Sijajua tumekosea wapi, ila mateso tunayoyapata kwa sasa ni fundisho. Siku nyingine tusikimbilie kuchagua ovyo kwa kuhongwa na kudanganywa, lakini sasa nadhani umefika wakati kwa wananchi kujua ni heri punda mzima hata kama ni wa thamani ndogo, kuliko farasi mgonjwa japo ni wa thamani kubwa. Serikali angalieni mnakotupeleka!

  Click here:Kikwete tumekukosea nini?
   
 2. TECHMAN

  TECHMAN JF-Expert Member

  #2
  Jan 23, 2012
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 2,677
  Likes Received: 162
  Trophy Points: 160

  Ndio, tumemkosea kikwete, ni kweli analipiza kisasi. Si kweli kuwa tulimchagua kikwete.


  • Kikwete Jakaya Mrisho/CCM kura 5,276,827= 61.17%
  • Watu waliojiandikisha kupiga kura walikuwa 20,137,303 (idadi hiyo ilipungua hadi Milioni 19)
  • Watu waliopiga kura walikuwa 8,626,283 sawa na asilimia 42.84% (ya wote waliojiandikisha)
  • Kura zilizoharibika ni 227,889 ambazo ni asilimia 2.64% ya kura zote zilizopigwa.
  • Kura halali zilikuwa 8,393,394 yaani asilimia 97.36% ya kura zote zilizopigwa.
  Watu walijua kuwa CCM watatuia hila zote ili kumrudisha Kikwete katika Madaraka Ili kuficha aibu kuwa Kiongozi wa kwanza wa uraisi aliye tawala msimu mmoja. Wananchi wakasusa.

  Je Kikwete anahaki ya kudai kuwa ni Raisi wa watanzania. Jibu ni NO. Kwa idaidi ya kura alizopata na idadi ya watanzania haviendani kabisa. ( Hapo hatuja angalia idadi ya kura zilizo ibwa).

  Nikweli kuwa kikwete analipiza kisasi kwa watanzania kwa kummkataa.
   
 3. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #3
  Jan 23, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  Nice observation rais wa watu mil.5 kwenye nchi ya watu mil.50.
   
 4. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #4
  Jan 23, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  huu ni upupu.fanyeni kazi,kulalamika sio mtaji na sio suluhisho la kuondoa ugumu wa maisha.
   
 5. nginda

  nginda JF-Expert Member

  #5
  Jan 23, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 745
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kumbe. halafu hata mkifa wote yeye hana hasara.
   
 6. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #6
  Jan 23, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  dawa ya ugumu wa maisha ni kujiongezea kipato sio kulalamika.kubana matumizi sio silaha ya kushinda maisha.tatizo la kuyumba kwa uchumi ni ladunia nzima lakini haliwezi kutupumbaza tukabaki walalamikaji badala ya kupendekeza majibu.<BR>tusifiche udhaifu au uvivu wetu kwa kuitupia lawama serikali.
   
 7. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #7
  Jan 23, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  Huna jipya hebu toka kidogo nenda kajisaidie ndipo urudi na mawazo yenye akili !
   
 8. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #8
  Jan 23, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mkuu si lazima nawe uropoke ili ujione umechangia,jamaha kaja na hoja ya msingi nawe ulitakiwa kujibu hoja zake!sio unakurupuka na kuanza kutukana,hizo ni akili za panzi!ukiwa kimya kama hauna hoja uwa si rahisi mtu kugundua upumbavu wako
   
 9. H

  Honolulu JF-Expert Member

  #9
  Jan 24, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 5,654
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Watanzania wanafurahisha! Wanapiga kura kama vipofu, halafu wanalalama kama vichaaa!
   
 10. K

  Kiduku JF-Expert Member

  #10
  Jan 24, 2012
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 480
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  &#8203;ni kweli hatukumchagua ni rais wa nec
   
 11. B

  Bigaraone JF-Expert Member

  #11
  Jan 24, 2012
  Joined: Jun 29, 2011
  Messages: 722
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ndugu mwandishi sio kuwa tumemkosea nini. Sisi ndio tuliojikosea na kosa la kwanza na kubwa tulilifanya 2005 pale tulipomchagua kwa kishindo au kwa ushindi wa sunami. Walewale tuliomchagua ndi haohao 2010 au hatumpigia kura au tulisusa baada ya kile tulichokitarajia kukikosa. Lakini sote tu mashahidi kuwa kwa katiba ya Tanzania na unyangau wa wa CCM na tume ya uchaguzi (NEC) ni vigumu kumshinda rais aliyeko madarakani ambaye anatumia raslimali za serikali/umma kujipigia kampeini. Hivyo 2005 tulipaswa tujiulize tunachagua kiongozi wa nchi/kioo cha taifa au tunachagua mwigizaji wa sinema? Watanzania wasomi na wasiosoma, viongozi wa dini, wanafunzi na wanadiplomasia waliaamua kuchaguliwa rais na vyombo vya habari. Tuliamisha akili zetu tukaacha kuhoji na mwisho tukaenda kupiga kura kwa ushabiki tu bila kufanya upembuzi. Tulishindwa kuangali uadilifu (integrity) wake, uchapakazi wake, elimu yake, falsafa yake ya siasa, uzalendo wake, hofu ya Mungu (sina maana dini yake au dhehebu), uelewa wa mambo ya kimataifa (sio uzoefu), wepesi wa kujifunza, kujikatalia (self negation) na mambo mengi. Kwa kufanya kosa hilo tumejikuta tulichoambiwa na magazeti sicho na tukaanza kuomboleza. Tusikate tamaa na we should not waste time to bank ton Kikwete anymore or anybody from CCM as all are birds of the same feather.

  Mnajua ni Chama gani na kiongozi gani mbadala. Tuwe wakweli wa nafsi zetu. Mini bila ushabiiki maana sina chama mpaka naandika hapa kiongozi aliyeko moyoni mwangu ni Dr.Slaa. Kama nitalazimika kumpigia kura aksimamishwa na chamchake basi nitapigia kura yeye maana hatujawa na mgombea binafsi bado .Huyu kwangu ni kiongozi anayeongea lugha ya wengi ya walalahoi. Haongei lugha ya wahisani wala mabepari anaongea lugha ya watanzania. Anachokiamini anakiongea bila woga wala kusita. Haongei matusi wala kejeli. Hana uswahili wala ubaguzi wa huyu mwenzetu bali kwake Tanzania kwanza. Kama kuna anayemwona kinyume na aseme tu naye atajibiwa. Tungeijua wapi EPA, MEREMETA, Richmond, IPTL, na kuchomekwa muswada wa maadili ya uchaguzi kama sio Dr.Slaa.

  Mungu ibariki Tanzania Mungu mbariki Dr.Slaa
   
 12. chuki

  chuki JF-Expert Member

  #12
  Jan 24, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,691
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Kama ndivyo ilivyo basi Dr. Slaa hana maana yoyote kujiita alikuwa mgombea urais kwani aliambulia kura Mil 2 tu na ushee katika nchi ya watu Mil 50. kweli dokta alidanganywa aache ubunge akaabike, naamini anajuta, kipindi kingine hawezi kukubali, maana nchi ya watu Mil 50, Mil 48 hawakuhitaji. Mwambieeni asirudie, na yeye 2015 hawezi kukubali ushaurin wowote.
   
 13. G

  Gwesepo Senior Member

  #13
  Jan 24, 2012
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  kwa kweli huyu Mkuu,kashindwa,ni bigwa mzoefu wa kuongea porojo,watanzania tumelishwa libwata,haiwezekani watu wakaishi maisha ambayo hayaeleweki harafu yeye anakaa kimya kama hayupo hivi harafu alipo nifurahisha sana akasema hamjui mmilki wa Dowans hivi kweli?,rushwa,ufisadi ,ubadhilifu wa fedha na mali za umaa Mikataba mibovu vimetawala,Magamba yamegoma kutoka Tanzania imegeuka kuwa chuma ulete ni sawa na mti wa zambalau kila mmoja anapopoa na mawe akijaza kikapu anaondoka ,yeye yupo anaangalia tu, ni sawa na mpira unao chezwa bila refa tujifunze kitu hapa ujinga na ulimbukeni wetu ndiyo umetufikisha hapa tulipo tunavuna matunda yetu tusilaumu.Vitu vinapanda bei watanzani tupo tuna lalamikia chinichini kama kobe .Wakati wa kampeni Rais anadanganya kwa kutoa ahadi rukuki ambazo hazitekelezeki kila akiona maji anaahidi meli mara barabara za juu n.k kweli Mtazania bila kumdanganya huwezi kushinda kwenye uchaguzi wowote ukishidwa kumuongoza mtanzania hata kuku huwezi kuongoza hayo ni majaabu.Ni bora watanzania wote tusipige kura uchaguzi ujao maana ukipiga kura tu wanaiba.nguvu ya umma inaweza kumtoa madarakani kwa kuandamana watanzania wote sio kukiachia chama cha chadema hatoki ng'o !! watanzania wana historia ya kukataa kujiuzuru kwa maana ya uajibikaji.
   
 14. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #14
  Jan 24, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Kosa tulilofanya ni kumpa kura mtu ambaye hana kichwa.
   
 15. M

  Maengo JF-Expert Member

  #15
  Jan 26, 2012
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndo maana ulikuwa unaililia ila sera ya Cameron maana uliona itakunufaisha.
   
 16. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #16
  Jan 26, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Hana kichwa tena? Hivi kwani alipewa kura au aliiba kura maana awamu ya kwanza alipewa na hakuboronga kama kipindi hiki alichoiba
   
 17. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #17
  Jan 26, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Well said but hawajiuzulu kwa 7bu wanajua hamwezi kuwafanya chochote na hao hao wanawajia kwenye chaguzi zijazo na mnawapa kura
   
 18. M

  MPG JF-Expert Member

  #18
  Jan 26, 2012
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 483
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kikwete ni mnafiki sana na mswahili sana,mi simpendi kabisa,hana uwezo wa kuongoza nchi.
   
Loading...