Kalunguine
JF-Expert Member
- Jul 27, 2010
- 2,543
- 134
Hakuna katika wakati mwingine wowote katika historia ya nchi yetu ambapo chombo cha habari kama vile redio Imaan kimeachiwa kufanya uchochezi wa Ki-jinga wa vita vya kidini. Ni katika utawala wa JK tu ndipo gazeti la serikali – Habari Leo likishishirikiana na magazeti ya Uhuru, Mtanzania, Rai na An-nnur vimetumika kuchochea chuki za kidini kwa manufaa ya utawala wa CCM unaomomonyoka kwa sababu ya kuendekeza unyonyaji wa kifisadi kwa wananchi kupitia mikataba feki ikiwemo Richmond, Dowans, n.k.
Bado tunakumbuka jinsi TCRA ilivyoruhusu meseji za kichochezi za Rashid Makame zilizotumwa kwa watumiaji wa Vodacom na Zain bila ridhaa zao wakati wa kipindi cha uchaguzi. Kilele cha uchochezi huo wa kidini unaopigiwa debe na JK kimefikiwa pale Diamond Jubilee. Watu wenye akili wanashangaa, huu ushirika wa JK, TCRA, Polisi, Usalama wa Taifa (UWT) kuacha uchochezi wa kidini kuendelea kupitia Radio Imaan na magazeti tajwa hapo juu kuna manufaa ya nani? Je nchi ikiteketea kwa udini ndiyo JK atafurahi? Hivi intelijensia ya vyombo vya serikali inayosemwa na Siad Mwema iko wapi katika uchochezi huu wa vyombo vya habari? Kwa nini nchi isambaratike katika mikono ya JK kwa minajili ya kufunika ufisadi wa Serikali ya CCM kwa kutumia mgongo wa uchochezi wa Radio Imaan na mlolongo huo wa magazeti?