Kikwete should learn something from this Dude...

TANMO

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
11,507
11,252
Angalia hii clip kwa umakini..



My Take:

1. Nimevutiwa na jinsi alivyokuwa anajenga hoja na kwa kutumia reference.
2. Ameongea kisomi zaidi na kwa muda mfupi amegusia mambo mengi. Kuna vitu nimejifunza kwa kuitazama hii clip.
3. Nimehamasika kuona jinsi alivyoshangiliwa baada ya kuingia uwanjani.
4. Body language yake alivyosalimiana na Mpinzani mwenzake Mbatia inafurahisha.
5. Hajiamulii nini cha kufanya, ana washauri na ameonesha kuwaheshimu, alivyoambiwa kukaa aongee na mtoto amekaa mara moja,, (marekebisho kidogo yanatakiwa kwenye kupangilia utaratibu wao). Ila kwa mbali sana ametofautiana na JK linapokuja suala la kuheshimu washauri. JK anasifika kwa kupuuza ushauri anaopewa (Rejea Kauli ya JK akiwa Mwanza baada ya kuishiwa nguvu na kuanguka!!)
6. Mungu ambariki huyu Bwana, ana umuhimu wake kwenye jamii yetu
 
Last edited by a moderator:
Unlike Lipumba, Kikwete talks and acts like this...

 
Last edited by a moderator:
Wakati mwingine "hujisahau" na kuleta utani kwenye kila jambo:

 
Last edited by a moderator:
nilimsikiliza Lipumba ,yuko makini sana huyu jamaa u Prof wake hauna shaka.
 
nasikia jana kasafiri, eti nasikia huko ivory coast sijui kuna nini eti kaenda kusaidia hahahahaha!
 
Tunaweza kuwa na tofauti za kisiasa na kiitikadi n.k. Lakini Mh.Lipumba ametuonyesha kuwa sisi ni Watz na kwa hili tukubaliane kuwa Mh. anabusara.Ameongea kama kiongozi na si mwanasiasa .
Kuna jambo limenigusa katika clip hii, wakati Lipumba anaongea na mtoto, kuna sauti ya mwana mama mmoja imesikika vizuri '' Tumeshakuwa wakimbizi ndani ya nchi yetu''. Mama huyu ameitoa kauli ile na kwa kusikia tu inaonyesha jinsi alivyokata tamaa na anavyoogopa ukimbizi. Kauli ameitoa kwa tukio la ajali tu nasi vita, lakini msikilize kwa makini.
Tafadhali nawaomba sana wale wenzetu ambao kazi yao humu JF ni uchochezi wa hisia za kikabila na kidini, wamsikilize mama yule, halafu wajiulize wanataka kusikia nini zaidi?
Wasikilize sauti ile na wajiulize, kama sauti ile ni ya mama, dada au shangazi yake atajisikia vipi akiwa huko aliko baada ya uchochezi usio na maana.
 
Tafadhali nawaomba sana wale wenzetu ambao kazi yao humu JF ni uchochezi wa hisia za kikabila na kidini, wamsikilize mama yule, halafu wajiulize wanataka kusikia nini zaidi?
Wasikilize sauti ile na wajiulize, kama sauti ile ni ya mama, dada au shangazi yake atajisikia vipi akiwa huko aliko baada ya uchochezi usio na maana.

Naam, umenena. Mungu atujalie Busara ili tutambue funzo lililomo kwenye hili angalizo lako..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom