inauma sana, lakini sijui tutafanyaje mana ukitaka kuleta mabadiliko wanakuzima mara moja kama mshumaa. lakini umoja ni nguvu tukiamua pamoja tunaweza. inauma kweli
UN, imeunda jopo la watalaamu na wanasiasa maarufu kufanya uchunguzi wa kina juu ya utajiri wa AFRICA usioinufaisha AFRICA, bali ULAYA.
Taarifa ya UN ya awali inasema, AFRICA inapokea dolar billion 25 kama msaada lakini madini na rasilimali za AFRICA zinazopelekwa ULAYA, ni zaidi ya dollor bilion 50.
Jopo hilo, limejuisha mwanasiasa maarufu wa Africa kusini Thabo Mbeki, ndiye mweusi pekee aliyeteuliwa na UN kufanya utafiti huo.
SOURCE: BBC SWAHILI, habari ya 06:00hrs
Swali langu ni kwa viongozi wetu hasa rais wetu anayeamini kwenda nje, ni kutaufta misaada. Je anajifikiriaje kwa msimamo wa UN?
Washauri wake na wataeule wake, wamefanya nini kuiendeleza Tanzania iache kuwa ombaomba na kuwa na uchumi unaojitosheleza?
CCM, nini mnajivunia mmewafanyia watanzania kwa miaka 36 mliyokaa madarakani na kuuza utajiri wetu nje ya nchi mpaka UN inawashtukia?
NADHANI MALENGO YAO NI KUPITA KILA NCHI YENYE EXPORT YA KUTOSHA LAKINI PATO LA TAIFA NI HOHE HAHE. TANZANIA TUKO KUNDI HILI, KWA EXPORT INAYOFANYWA HASA KATIKA VITO VYA THAMANI, NI WAZI KAMA ZINGERATIBIA NA KUZIFANYA ZIWE NUSUNUSU, UCHUMI WETU UNGEKUWA IMARA.hii kitu nzuri lakini huo mchanganuo wangeutoa kwa kila nchi
hapa si suala la kumlaumu mtu mmoja au kikwete kama rais,hili ni suala la waafrika wote ukiwamo wewe.
wewe umeifanyia nini tanzania na afrika kwa ujumla zaidi ya kulalamika tu hapa????????????????
kama ungekuwa na akili ungekuja na majibu baada kuwa umefanya utafiti wa kisayansi ili utusaidie,na kumsaidia huyo rais,kwa style ulokuja nayo umejiingiza katika kundi la walalamikaji.