Kikwete Rais wa kwanza kutia mguu Kitunda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete Rais wa kwanza kutia mguu Kitunda

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Mar 12, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 12, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [​IMG] Magari yakwama, trekta layakwamua
  [​IMG] Helikopta ya jeshi yaitwa kuokoa jahazi

  Ziara ya Rais Jakaya Kikwete kwenye kata ambayo haijawahi kutembelewa na rais yeyote tangu Tanzania ijitawale, juzi ilikuwa ngumu baada ya baadhi ya magari kukwama kwa muda likiwamo na la Mama Salma.
  Hali hiyo iliyotokea juzi ilitokana na ubovu wa barabara ambayo ililazimu trekta kutumika kuyakwamua.
  Adha hiyo iliyapata magari hayo ambayo yanatumiwa na watu waliopo kwenye ziara ya Rais Kikwete mkoani Tabora.
  Rais alikuwa akiendelea na ziara yake akitokea Tabora Mjini kwenda kata ya Kitunda ambayo haijawahi kutembelewa na rais yeyote tangu Tanzania ipate uhuru mwaka 1961.
  Kutokana na ubovu wa barabara, helikopta ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ililazimika kuitwa kutoka Tabora mjini kwa ajili ya kwenda kumchukua rais kumpeleka Wilaya ya Sikonge.
  Baada ya Rais kumaliza kuhutubia wananchi katika kata hiyo, helikopta hiyo ilitua na kumchukua tena kumrudisha Sikonge.
  Aidha, baadhi ya magari yaliyokuwa katika msafara huo nayo yalizama katika madimbwi na kulazimika kuvutwa na trekta.
  Akizungumza na wananchi wa kata hiyo ya Kitunda, Rais alifurahishwa na maendeleo ya elimu na kisha akatoa Sh. milioni sita kwa ajili ya ujenzi wa shule katika kata tatu za tarafa ya Kiwelu wilayani Sikonge.
  Alisema elimu ndiyo njia pekee ya kuwakomboa wananchi hivyo lazima waikazanie.
  Aidha, Rais aliagiza ijengwe barabara inayopitika muda wote kwa mwaka badala ya ilivyo sasa. Kuhusu maji, pia aliagiza yapelekwe kabla ya Julai ili atakaporudi akute kuna huduma hiyo.
  Aliwataka wananchi kubadilika na kuachana na tabia ya kuishi kwa kuhamahama kufuata malisho ya mifugo.
  “Hii tabia imepitwa na wakati, lazima mbadilike na kuanza kufuga kwa njia za kisasa ikiwemo kupanda nyasi za malisho badala ya kuhamahama kufuata malisho,” alisema. Kwa upande wao wananchi katika eneo hilo walifurahi kutokana na kutembelewa na rais ikiwa ni mara ya kwanza tangu wapate uhuru.
  Wakati huo huo, Rais Kikwete amewaonya Watanzania kuachana na tabia ya kutegemea wafadhili wawafanyie kila kitu, badala yake amewataka wajitahidi kujiletea maendeleo kwa kutumia raslimali chache walizonazo.
  Alitoa onyo hilo jana wilayani Uyui, Mkoa wa Tabora alipokuwa akizungumza na wakazi wa kijiji cha Mbola katika kata ya Ilolangula alipotembelea mradi wa Millennium Village (Kijiji cha Mileniamu).
  Alisema wafadhili bado wanahitajika kuwasaidia wananchi kujikwamua kiuchumi, lakini sio kazi yao kuwafanyia wananchi kila kitu. “Sisi wananchi tatizo letu tunataka hawa wafadhili watusaidie kila kitu, jambo ambalo haliwezekani,” alisema.
  Rais Kikwete alitembelea mradi huo ambao unawasaidia wakazi wa vijijini 15 katika Wilaya ya Uyui ambao unafadhiliwa na nchi mbalimbali zikiwemo Japan na Marekani na kusimamiwa na Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP). Aliwaambia wananchi hao kuwa waone misaada wanayopewa sasa ni kama changamoto ili waweze kujitahidi kujikwamua wenyewe kimaisha.
  Mradi huo unalenga kuwajengea uwezo wananchi wa vijiji 15 kwa kuwasaidia katika nyanja za kilimo, afya, huduma za jamii, kuondoa umasikini na kuwapatia pembejeo ikiwemo mbolea ya ruzuku na kuwapatia elimu. Aliongeza kuwa kama wananchi wataendeleza dhana ya kuisubiri serikali kuwaletea maendeleo, watachelewa na kuachwa nyuma na watu wengine duniani.
  Alifafanua kuwa Tanzania na nchi nyingine za Kusini mwa Jangwa la Sahara ni maskini na kwamba wananchi wakiendelea kutegemea kuletewa maendeleo watakuwa wanajidanganya.
  Akisisitiza umuhimu wa kujitegemea, Rais Kikwete alitoa mfano wa mji wa Osaka nchini Japan ambao pato lake linazidi nchi za Afrika zilizopo Kusini mwa Jangwa la Sahara.
  Aliwasisitiza wananchi kuanza angalau na walichonacho ili wakiwaita wafadhili wawe wamesogea kidogo.
  Meneja wa mradi huo, Dk. Gilson Nyadzi, alisema umepata mwitikio mkubwa kutoka kwa wananchi.
  Alisema wameanza vizuri katika sekta ya maji ambapo wamechimba visima, kujenga zahanati, shule na kuhimiza kilimo bora katika vijiji husika. Aidha, alisema wanatarajia kutumia zaidi Sh. milioni 350 kujenga barabara.
  Katika hatua nyingine, Rais Kikwete aliwatahadharisha wakazi wa kata hiyo kuacha kutumia mbolea ya ruzuku wanayopewa na wafadhili kulimia tumbaku.
  Alifafanua kuwa tumbaku ni kitu hatari ambacho wafadhili hawawezi kukubali kukifadhili hivyo wananchi wasithubutu kuwachokoza.
  Akitoa taarifa kwa Rais, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Abeid Mwinyimusa, alisema hivi sasa watoto wanapenda kwenda shule kwa kuwa wanapatiwa chakula shuleni.
  “Mheshimiwa mahudhurio yameongezeka, baada ya wazazi kuchangia mahindi ili watoto wao waweze kupata chakula,” alisema.
  Rais Kikwete jana aliweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Chuo cha Jamii ambacho kitakuwa kinatoa mafunzo mbalimbali, kuzindua miradi ya visima iliyofadhiliwa na UNDP.  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #2
  Mar 12, 2010
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mwanzo nilidhani unazungumzia Kitunda ya hapo Ukonga :D
   
 3. O

  Omumura JF-Expert Member

  #3
  Mar 12, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kwa kutia kwake mguu, ameyabadilisha maisha ya wana kitunda au usanii tu?
   
 4. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #4
  Mar 12, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Angekua serious, kitu cha kwanza ingekuwa kutafuta immediate solution ya tatizo la barabara, badala ya kutoa mawaidha ya jumla, kaa vile haimuhusu.
   
 5. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #5
  Mar 12, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  Yes wakuu, niliwaambia juzi kwenye thread yangu kuhusu hii tarafa - nikahoji hivi Rais atatumia usafiri gani kwenda kwenye tarafa hii? sasa wengine ndiko walikozaliwa just imagine. leo hii 2010 tunaita karne ya sayansi na technologia Rais anakwama kwenye matope, nafikri sasa ndiyo mnajua matatizo tuliyokuwa nayo sisi wananchi wa tarafa hii - binafsi kusoma na kujikwamua kutoka tarafa hii wanza lazima JF mnipongeze sana.

  Pole sana Rais na mama salma lakini pia tupeni pole zaidi sisi ambao tumeishi kwa hali hiyo tangu uhuru hadi leo.

  Najua tu kama akitumia gari angekwama bunga inaitwa "Ipembampazi" au "Kururu" mbuga hizi ziina urefu wa takribani km 12, hupiti pale hata kama una Six wheels V8 Land Cruiser.
   
 6. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #6
  Mar 12, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  kwa haraka haraka nikiwa mzawa wa huko kitunda ni usanii tu mkuu, kila kukicha kwetu sisi ni afadhali ya jana.
   
 7. senator

  senator JF-Expert Member

  #7
  Mar 12, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 1,927
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Napata picha ELNINO ww ni mtoto wa mkulima haswaa sio wakina walee wanazaliwa wanakuta baba anamigari kumi na mijumba ya kumwaga hizi taabu anabaki kuzisikia magazetini na kuona luninga..Pole mdau nyumbani ni nyumbani
   
 8. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #8
  Mar 12, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  Upo sahihi Abdulhalim - ndiyo maana watu wanamwita msanii, sasa sijui alikuja kwetu kufanya nini wakati hatujasikia tamko rasmi la kushughulikia hii barabara mbali na ngojera za kawaida.

  Rais unakwama unaokolewa na helkopta - unarudi jijini - then what next?
   
 9. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #9
  Mar 12, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  lol, ina maana jibu hulijui? Watakwambia 'tenda imeshatangazwa', 'mradi upo kwenye upembuzi yakinifu' etc etc.. au lile neno la jumla 'tupo kwenye mchakato', yaani hatuna haraka na maendeleo.
   
 10. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #10
  Mar 12, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  kaka nakumbuka nikiwa nasoma secondary - tukifunga shule december unaweza fika home two days before shule ifunguliwe - likizo yote inaishia kwenye shida hizi za usafiri.

  Yeah Mkuu, sisi wengine bila bidii binafsi na huruma ya Kambarage kuweka free education to all basi tusingekuwa online accessing JF saa hizi - tungekuwa vijijini wake 4 na watoto kama 16 hivi.
   
 11. M

  Mchili JF-Expert Member

  #11
  Mar 12, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kumbe una uzoefu na adha ya mafuriko ndio maana ukaitwa ELININO :D
   
 12. Isimilo

  Isimilo JF-Expert Member

  #12
  Mar 12, 2010
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 219
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ana bahati hata hiyo helicopta ingekuwa mbovu kwani wabongo huwa hawajiandai kwa dhalula kama hizi. ufisadi hadi kwenye vitu nyet kama hivi. hiyo helicopta pia ni bahati labda ingeshindwa kunyanyuka
   
 13. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #13
  Mar 12, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  yeah mkuu umepatia kabisa...... :), mimi nimejikwamua tatizo wenzangu waliobaki huko.....
   
 14. K

  Kikambala Senior Member

  #14
  Mar 12, 2010
  Joined: Jun 28, 2008
  Messages: 163
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  kampeni zimeanza kujisifu kwingi lakini wakipata ndio jumla,haina mshiko hata kama amuekuwa rais wa kwanza so what?
   
 15. J

  Jafar JF-Expert Member

  #15
  Mar 12, 2010
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Sio hiyo tu ya Kitunda, yaani huyu amevunja rekodi nyingi tu na kuwazidi waliomtangulia kwa nyuma sana. (naomba nisizitaje)
   
 16. M

  Mchili JF-Expert Member

  #16
  Mar 12, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Pole sana ELNINO, kwani alienda kufanya nini Tabora wakati waziri mkuu alikuwepo huko hivi karibuni? Kwa nini hakumtuma hiyo kazi.
   
 17. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #17
  Mar 12, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  Alikwenda Tabora kwa shughuli ya kina mama, baada ya hapo akaambiwa wananchi wa tarafa ya Kitunda na vitongoji vyake wanaweza kuipiga chini CCM - ndiyo maana akaamua kwenda mwenyewe front kusafisha njia ya CCM ipite tena 2010 bila matatizo.

  Inawezekana Mkuu zikawa ni kampeni tayari za undergound...
   
 18. MTWA

  MTWA JF-Expert Member

  #18
  Mar 12, 2010
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 1,026
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Ofcourse huo ni usanii mtupu, kuna wenzenu aliwaahidi tangu mwaka juzi hakuna la maana lililofanyika
   
 19. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #19
  Mar 12, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Kuna watu wanamiliki Visiwa ziwa Victoria na wana serikali yao ndani ya serikali ya nchi.
   
 20. MTWA

  MTWA JF-Expert Member

  #20
  Mar 12, 2010
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 1,026
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Ni kweli Mkuu haina maana ya kuja kutuinjoy huku akitafuta ujiko. ameshaona mambo yanaweza kuwa magumu mwaka huu so anaturushia michanga akijua itaangukia machoni naye aendelee kutesa na jamaa zake. Tusubiri kuona atafanya nini.
   
Loading...