Kikwete On TBC1: Aongea na wazee wa mkoa wa Dar

Wandugu,
Kama kuna jambo ambalo huwa linanishangaza ni hili la wazee wa Dar es Salaam. Katika nyakati zote ambazo mtawala wa nchi hii Dr. Dr. Dr. (Heshima-UDOM, UTURUKI, UDSM) alidai anaongea na wazee, nilichodhuhudia ni uwepo wa akina dada wa 'mipasho' waliosiliba midomo yao na rangi wakishangilia kwa sauti ileile inayotolewa kwenye taarabu. Mbaya zaidi wengi wao huwa wanakuwa kwenye lindi la usingizi wakati mtawala na msomi wa PhD ya heshima akiendelea kutoa hotuba yake. Wakati mwingine huwa inakuwa kama mchezo wa kuigiza hivi.

Jambo jingine ambalo huwa najiuliza ni je hao ni wazee wa Dar es Salaam au ni wana ccm wa Dar es Salaam tena kutoka Ilala na Temeke kwa wala ubwabwa na wanywa kahawa?

hapo kwenye Red unazungumzia PHD Ya nini..???

hapo kwenye black "wazee wa dar" wenyeji wa DSM hivi inakupa shida kufukiri wenyeji wazee wa dar ni watu wa pwani... sasa mbona unadhihaki mila na desturi zao... nawashangaa mnaposema kunywa kahawa barazani ni uswahili na kunywa ma wisky na pombe ndio uzungu ..... wawapi weye ...????
basi sisi watu wa pwani hatutaki huo uzungu wenu tuacheni na huu uswahili wetu .....

kumbuka TANU baadaye ikawa CCM harakati na mambo yote yalikuwa dar.... je wadhani wale wazee ambao walikuwa toka enzi hizo za tanu au wamelelewa na wazee wao ambao walikunywa maji ya TANU ulitaka waje na reaction gani ...! kwamba CCM ife.. give them a break

Mfano akienda moshi na kusema nataka kuongea na wazee wa moshi ofcoz utakuta mandhari tofauti na wazee wa dsm kutokana na mila za wale watu wa eneo lile... yaani hata mtoto wa primary school hawezi akaja na thread kama hii totaly wasted + crap!


 

Imeandikwa na Oscar Mbuza; Tarehe: 18th November 2011

KATIBA mpya ya Tanzania itaandikwa na Watanzania wenyewe kwa kupitia maoni yatakayotolewa nao kwa Tume itakayoundwa kwa mujibu wa sheria ya mwaka huu.

Kauli hiyo ilitolewa jana Dar es Salaam na Rais Jakaya Kikwete alipozungumza na Taifa kupitia wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam. Alisema kila Mtanzania atapewa fursa ya kutoa maoni yake kwa Tume ambayo ataiunda kwa kushirikiana na Rais wa Zanzibar mara Muswada wa marekebisho ya Katiba uliopitishwa jana na Bunge la Jamhuri utakapokuwa umesainiwa.

Alisisitiza, kwamba Tume haitaacha kusikiliza maoni na hoja ya kila mtu atakayependa kushiriki kuchangia, lakini hayo yatafanyika kwa kuzingatia sheria. “Katiba iliyopo itafuatwa, kwa sababu ndiyo iliyopo kwa sababu kubadili Katiba lazima ya zamani iwepo, hivyo itafuatwa na kuzingatiwa katika mchakato mzima wa kupata Katiba mpya,” alisema Rais.

Tume kuteuliwa na Rais Juu ya malalamiko yanayotolewa na baadhi ya wanaharakati pamoja na wanasiasa, hususan wa upinzani kwamba yeye hastahili kuunda Tumeya kusimamia mchakato wa kuandika Katiba, Rais alishangaa.

Alisema hii si mara ya kwanza kwa Rais kuunda Tume kama hiyo, kwa sababu hata waliomtangulia walipata kufanya hivyo akitolea mfano wa Rais wa Kwanza Mwalimu Nyerere ambaye aliunda tume kama hiyo mara tatu; mwaka 1963, 1964 na 1965 Akifuatiwa na Rais wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, ambaye aliunda mara moja mwaka 1992 chini ya Jaji Francis Nyalali na Benjamin Mkapa mara moja ya Jaji Robert Kisanga.

Alisema Katiba iliyopo inampa mamlaka ya kuuda Tume hiyo, ambayo alisema itajumuisha watu wa kada mbalimbali na kufuatiwa na Bunge Maalumu la Katiba, ambalo litajumuisha wanasiasa wakiwamo wabunge, wawakilishi na watu wengine 300.

Kuhusu hoja kwamba Zanzibar isipewe fursa sawa na Tanzania Bara, Rais aliponda hoja hiyo, akisema udogo wa nchi si hoja na kinachotakiwa ni ushirikishi kwa usawa.

“Hizi ni nchi huru zenye hadhi sawa-udogo si hoja, Shelisheli ina watu 84,000, lakini ni Taifa huru, hivyo mkiamua kuungana nayo, lazima mnakuwa na haki sawa pia,” alisema Rais.

Katiba ya sasa si mbaya Pamoja na kutaka kuja na Katiba mpya, lakini alisema Katiba ya sasa si mbaya, kwani imewalea Watanzania kwa muda mrefu katika mazingira ya amani na utulivu na kupiga hatua kubwa ya maendeleo kuliko ilivyokuwa miaka 50 iliyopita.

“Tunachotaka kukifanya sasa ni kuhuisha Katiba itakayofanana na Tanzania ya sasa. Katiba ya miaka 50 ijayo ambayo itaendelea kudumisha amani na utulivu,” alisema. Alisema katika mchakato huo, kuna mambo ambayo yatatakiwa kujadiliwa na hasa kulindwa, kwa kuwa ndizo tunu za Taifa.

Aliyataja mambo hayo kuwa ni pamoja na kuwapo kwa nchi na mipaka yake; Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; Serikali ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar; Bunge; Mahakama; umoja; mshikamano na usalama; haki za binadamu; usawa mbele ya sheria; uhuru wa kuabudu na kuaminiana.

Alisema hayo yatazungumzwa kwa maana ya kulindwa na si kutaka kubomolewa, kuvunjwa au kukiukwa.

Kusomwa Muswada
Akifafanua kuhusu kusomwa kwa Muswada huo bungeni, Rais alisema Muswada wa Katiba ulisomwa mara ya kwanza bungeni, ukachapwa katika Gazeti la Serikali siku 21 kabla ya mkutano mwingine wa Bunge na kuwasilishwa katika Kamati ukajadiliwa na kupewa wadau ambao nao walichangia.

Kamati ilipomaliza kuujadili na wadau kuchangia, ukarejeshwa tena bungeni na kusomwa kwa mara ya pili na kujadiliwa pia na Bunge na kisha kurekebishwa na kupitishwa na kusomwa mara ya tatu pale Katibu wa Bunge aliposoma taarifa ya Muswada kupitishwa.

“Watu wanataka kupotosha tu, Muswada huu kila ulikopitia ulijadiliwa na tumeona mchango mkubwa wa majukwaa yaliyoundwa kuujadili na mikutano mbalimbali ya hadhara … simu zilitumika, mitandao … kilichokosewa ni kipi?” Alihoji.

“Kwa kuwa Bunge linataka Tume iundwe na kuanza kazi Desemba mosi … zimebaki kama siku 12, tutaufanyia kazi, mimi na Rais wa Zanzibar tutaunda Tume na mwakani kazi ya wananchi kutoa maoni ifanyike na ili ifikapo mwaka 2014 wakati tunasherehekea miaka 50 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tuwe na Katiba mpya … na uchaguzi wa 2015 ufanyike chini ya Katiba mpya,” alisema Kikwete.

Aliahidi kuwa watachagua watu wanaostahili kuunda Tume na si kwa kutumia urafiki wala kujuana na mtu bali weledi utazingatiwa.

Amshangaa Mbowe
Rais alishangaa malalamiko yanayojitokeza hivi sasa juu ya mchakato huo kiasi cha baadhi ya vyama kukataa kuchangia bungeni, huku akimtaja kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe (Chadema), ambaye alimpongeza Rais kwa kuruhusu mchakato wa Katiba mpya na sasa amegeuka.

Aliwataka wanasiasa na wanaharakati kuacha kupotosha wananchi kwa kutumia vibaya dhana ya nguvu za umma, huku jambo jema la Katiba mpya likiwa linasubiriwa na wengi.

Alisisitiza, kuwa Serikali haijakosea popote wala haijafanya kinyume cha sheria kutokana na mchakato wa Muswada wa Katiba hiyo, hata kusababisha tuhuma na malalamiko yanayojitokeza hivi sasa.

Hali ya uchumi
Awali akizungumzia hali ya uchumi, Rais alisema matatizo yaliyopo hivi sasa ni matokeo ya hali mbaya ya uchumi duniani, huku akisema hali ya uchumi katika mataifa makubwa imetetereka.

“Huko ndiko yaliko masoko, watalii, mitaji ya uwekezaji na vifaa mbalimbali vya viwanda vyetu hivyo kukitikisika nasi tunatikisika … dola ya Marekani hivi sasa imeimarika ikilinganishwa na euro ya Ulaya hivyo kuathiri uchumi.

“Bei ya mafuta duniani nalo ni tatizo na imesababisha bei ya chakula na bidhaa zingine kupanda … hiyo ni pamoja na sera za kifedha kubadilika, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inachukua hatua za kukabiliana na hali hiyo,” alisema Rais.

Alisema kama mataifa makubwa yatarekebisha uchumi wao, mataifa madogo ikiwamo Tanzania nayo yataokoka.

Alitolea mfano wa mfumuko wa bei ambao Oktoba mwaka jana ulikuwa asilimia 4.2 lakini mwezi huo huo mwaka huu ukafikia asilimia 17.9. Alisema hali hiyo iko pia katika nchi nyingine za Afrika Mashariki.

Akifafanua kuhusu mafuta, alisema utaratibu uliopendekezwa na kukubaliwa nchini wa wafanyabiashara kuagiza mafuta kwa pamoja, utasaidia kurekebisha hali na unatazamiwa kuanza mwezi ujao.
 
Aibu, Wazee watia aibu ya mwaka.

Wazee wametuwasaliti Watanzania, wanao na vijukuu kwa kutunyima fursa ya kutengeza katiba shirikishi.

Wazee wameturithisha mfarakano.
 
Saturday, November 19, 2011, 5:55


*Asema tatizo lake ni kutoa uhuru mwingi
*Asisitiza Katiba mpya itapatikane kabla ya 2015
*Asema mchakato umefuata taratibu zote

Arodia Peter na Esther Mbusi



HATIMAYE Rais Jakaya Kikwete, amevunja ukimya na kusema yeye si kiongozi dikteta kama ambavyo baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakidai.


Akihutubia taifa kupitia wazee wa mkoa wa Dar es Salaam, Rais Kikwete alisema kama angekuwa dikteta uhuru uliopo nchini usingetumika kama ulivyokusudiwa.

"Mimi ningekuwa dikteta, hata anayeniita dikteta asingethubutu kufanya hivyo na wala asingekuwepo hii leo.

…Rais dikteta anayetoa uhuru wa watu kuongea watakavyo, kuandika watakavyo… kama kweli Rais angekuwa dikteta hata yeye huyo asingethubutu kuniita hivyo, mimi ninachojua ni kwamba nasemwa sana kuwapa uhuru vyama vya siasa na vyombo vya habari, hii ndio lawama ninayoipata.



"Labda nijaribu udikteta siku moja tuseme basi, hapa itabaki TBC, Daily News na gazeti la chama changu (Uhuru), lakini kwa nini tufike huko, mimi naamini hao wanaoniita dikteta wangekuwa hapa nilipo wangekuwa zaidi ya hapa," alisema Kikwete.



Akizungumzia mchakato wa Katiba mpya, Rais Kikwete alisema si kweli Serikali imefanya kosa lolote, kwani ilichofanya sasa ni kuongeza kitu kimoja cha kuwapa Watanzania uhuru wa kutoa maoni yao.


Alisema kiu kubwa ya Watanzania ni kupata Katiba mpya ambayo watakuwa wameshiriki kuitunga wenyewe tofauti na nyingine zilizopita.



Alisema, mchakato huo utaanza Desemba mosi, mwaka huu ambapo Muswada huo utaanza kufanya kazi rasmi na atashauriana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein ili kuunda tume itakayokusanya maoni ya wananchi na baadaye kuandaa rasmu ya Katiba.


"Wale wanaosema wasipopata Katiba mpya kabla ya mwaka 2015 patakuwa hapatoshi, sasa mimi nataka patoshe, tunataka ipatikane mwaka 2014 na tutakapoingia kwenye uchaguzi mkuu tuwe nao"


MCHAKATO
Alisema suala la mchakato mzima wa Muswada wa Katiba ambao umeridhiwa na wabunge wengi wa CCM, UDP CUF na TLP, lakini umepata upinzani mkali kutoka kwa vyama vya Chadema na NCCR – Mageuzi pamoja na wanaharakati, umepita utaratibu wote unaohitajikai.

Kuhusu madai ya kuupinga Muswada huo kwamba ulipaswa kusomwa kwa mara ya kwanza Bungeni, Rais Kikwete alieleza kwa undani taratibu zilizotumika hadi kufikia hatua za kusomwa kwa mara ya pili, akisema tayari wananchi walikwishapata nafasi ya kujadili na kutoa maoni yao katika vituo vya Dar es salaam, Zanzibar na Dodoma na kusema si Muswada mpya kama ambavyo wanaoupinga wamekuwa wakipotosha umma.


"Taratibu za kuwasilisha na kusomwa kwa Muswada zilifuatwa tangu Februari, kwanza ulitangazwa kwenye gazeti la serikali kwa muda wa siku 21 na baadaye kukabidhiwa kwa Kamati ya Sheria na Katiba ya Bunge na kamati hiyo iliupeleka kwa wananchi katika vituo vya Dar es Salaam, Zanzibar na Dodoma, wananchi waliujadili na mapendekezo yao yalizingatiwa,

"Sijui hoja ya Muswada kusomwa kwa mara ya kwanza hapa inatoka wapi, sababu yake siioni, ndiyo maana Spika (Anne Makinda), ameukataa kusomwa kwa mara ya pili" alisema Rais Kikwete

Rais Kikwete, hakuchifa hisia zake, baada ya kumshambulia Mnadimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu kwamba licha ya taaluma yake ya Sheria, lakini amekuwa mstari wa mbele kuutoposha umma kuhusu Muswada huo.


Kuhusu hoja ya wapinzani na wanaharakati, Rais Kikwete alisema amepewa madaraka makubwa katika mchakato huo, na kusisitiza kinachofanyika ni kutumia mamlaka aliyo nayo kikatiba kuhakikisha unafanikiwa.

"Katika hilo, hakuna ambapo Serikali imekosea, kupata muafaka wa kupata Katiba mpya, lazima katiba iliyopo sasa itumike.

"Hakuna ambacho serikali imekosea, hatuwezi kufuta katiba iliyopo kabla hatujapata nyingine, lazima tutumie maelekezo ya hii tuliyonayo ili kupata nyingine ili bora zaidi

…Naomba Watanzania wanielewe, Kenya walitaka kutumia njia wanayoitaka hawa wenzetu, lakini walikwama kwa miaka 20, lazima kuwe na msimamizi wa vitu hivi, na msimamizi wa jambo hili ni mimi Rais kwa mujibu wa Katiba"

"Rais ndiye mkuu wa nchi, ndiye mwenye mamlaka ya kufanya hayo, haki na mamalaka hayo ya Rais yapo Kikatiba sijui wanataka nini zaidi"

"Wakati mwingine inasikitisha, watu wanaojua kujifanya hawajui ukweli, hasa kupotosha ukweli kwa jambo lililofanywa na Serikali… sijui ndiyo hiyo nguvu ya umaa? Alihoji Rais Kikwete

Kuhusu mfuko wa bei ya bidhaa nchini, akijitetea kuwa hiyo ni tatizo la dunia nzima na hata uchumi wa mataifa ya Ulaya nao umeathirika kwa kiasi kikubwa na si kama ilivyokuwa zamani.

"Uchumi wa Ulaya unapotetereka, ujue na sisi tutayumba kwa sababu bidha nyingi zinatoka huko huko, utalii pia tunawategemea wao, sasa wanapoyumba na sisi tunaingia katika matatizo makubwa," alisema Rais Kikwete.

Mwisho

 
Kwa hili la Udikteta rais wangu nakuunga mkkono. Tuache ushabik, rais kikwete huwezi ukamlinganisha na mkapa. Tuseme mambo mengine lakini si swala la uhuru. Mimi ninampongeza sana rais kwa swala la demokrasia.
Tatizo kubwa ni wapambe wake ndani ya ccm ndo wanamperekesha. Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.
 
Back
Top Bottom