Kikwete: Nilitaka kunyonga wauaji wa albino | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete: Nilitaka kunyonga wauaji wa albino

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by anophelesi, Oct 14, 2012.

 1. a

  anophelesi JF-Expert Member

  #1
  Oct 14, 2012
  Joined: May 25, 2012
  Messages: 615
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 80
  Suzy Butondo, Shinyanga | Mwananchi | Oktoba 14, 2012


  RAIS Jakaya Kikwete amesema kuwa kuna wakati aliwahi kufikiria kuwanyonga watu waliokuwa wakikamatwa kwa kuhusika na mauaji ya albino yalipokuwa yamepamba moto kwa kuwa jambo hilo lilikuwa likimtia hasira.

  Rais Kikwete alisema hayo jana katika kilele cha kumuenzi Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.

  Rais alisema hayo alipokuwa akizungumzia tukio la uchomwaji wa moto makanisa lililotokea Mbagala, Dar es Salaam akieleza athari za mtu mwenye jazba kuchukua hatua.

  Juzi, Rais Kikwete alitembelea eneo la hilo la tukio na kushuhudia makanisa matatu yalivyoharibiwa pamoja na magari.

  "Kwenye lile la maalbino nilishaandika kwenye hotuba yangu nitanyonga watu kwa kuwa nilikuwa nina hasira, lakini washauri wangu waliniambia hiyo itakuwa ni kinyume cha sheria kwa kuwa kuna watu walikuwa wamepelekwa mahakamani na hata uamuzi haujatolewa," alisema Rais Kikwete na kuongeza:

  "Nilifuta baada ya kushauriwa, lakini hadi sasa nina hasira. Ninajitolea mfano wangu mwenyewe ili muone kwamba kujichukulia uamuzi kusivyokuwa vizuri wakati una hasira."

  Alirejea kauli yake kwamba kitendo cha mtoto kukojolea kitabu kitukufu cha Waislamu kilikuwa ni kosa kubwa na Waislamu walikuwa na haki ya kukasirika, lakini haikuwa sawa kwao kuvamia makanisa.

  Rais Kikwete alisema kitendo cha wao kuvamia makanisa na kuyachoma na kuvamia kituo cha polisi ni kinyume cha sheria za nchi.

  "Mtoto mwenyewe kwanza hakutumwa na kanisa pia alikuwa mikononi mwa polisi. Sasa kitendo cha kwenda kituo cha polisi kutaka wapewe mhalifu wao ni kinyume cha sheria pia kuvamia makanisa ilikuwa si sawa."

  Akerwa na rushwa
  Katika hatua nyingine, Rais Kikwete amesema anakerwa na jinsi vitendo vya rushwa vinavyozidi kushamiri nchini na kutoa wito kwa Watanzania wote kushiriki kwa pamoja kuwafichua na kuwataja hadharani wale wote wanaojihusisha na tabia hiyo.

  Alisema anachukizwa kuona vitendo vya rushwa vikizidi kushamiri, huku jamii ikikaa kimya bila kukemea kwa kuwafichua watu wanaojihusisha na vitendo hivyo ambavyo vinachangia kwa kiasi kikubwa kuwanyima haki Watanzania walio wanyonge.

  "Nawaombeni ndugu zangu tushirikiane kwa pamoja kupiga vita suala hili la rushwa, maana linaelekea kuota mizizi, ni wajibu wa kila mmoja wetu kujitoa muhanga kupiga vita ugonjwa huu wa rushwa. Tuikemee sisi sote raia na wasio raia, watumishi wa umma na wasiokuwa watumishi wa umma, wafanyabiashara binafsi na wasiokuwa wafanyabiashara na kila mmoja awe ni balozi wa kupambana na vitendo vya rushwa."

  Mbio za Mwenge zilizinduliwa Mei 11, mwaka huu huko Mbeya na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

  Waumini wasali nje
  Siku tatu baada ya makanisa kuchomwa moto na kuharibiwa vibaya, baadhi ya waumini wamelazimika kusali wakiwa nje, huku viongozi wao wakiwataka kutolipiza kisasi kama mafundisho ya dini zao yanavyoelekeza.

  Hata hivyo, viongozi hao wameitaka Serikali kutekeleza ahadi yake ya kuwachukulia hatua za kisheria waliohusika na uharibifu huo ili liwe fundisho kwa wengine.

  Juzi, Rais Kikwete alitembelea makanisa hayo na kuagiza polisi kuwasaka na kuwakamata wote waliohusika ili wafikishwe kwenye vyombo vya sheria.

  Jana, Mkuu wa Jimbo la Kusini la Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Mchungaji Aman Lyimo alisema kwamba katika Usharika wa Mbagala, kamwe hawatalipiza kisasi dhidi ya waovu hao.

  "Waliofanya kitendo hicho si Waislamu, bali ni wahuni wanaotumia dini kama kichaka cha kuficha uovu wao, tuliosomea dini mbalimbali tunafahamu kwamba hakuna dini yoyote inayoruhusu kufanya uovu kama huu uliofanywa katika makanisa."

  "Hatutawalaani wala kuwahukumu kwa sababu hawajui walitendalo, tutakachokifanya ni kuendelea kuwaelimisha bila kuchoka kwamba wanatakiwa kutubu kwa sababu wamemkosea Mungu."

  Kiongozi wa Kanisa la Anglikana, Usharika wa Mbagala Kizuiani, Emmanuel Mng'ong'o alisema waumini wa kanisa hilo wamefanya ibada yao katika mazingira magumu baada ya vurugu hizo.

  Alisema madirisha 36 ya vioo vya kanisa hilo yalivunjwa, huku madhabahu ikiwa imeharibiwa... "Tuna imani na ahadi ya Rais Jakaya Kikwete kwamba waliofanya uhalifu huo watachukuliwa hatua za kisheria."

  Kamanda wa Mkoa wa Temeke, David Misime alisema jana kwamba hadi sasa jeshi hilo linawashikilia watu 122 kuhusiana na vurugu hizo.

  CCM walaani
  Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimelaani kitendo cha kukojolea Kitabu cha Quran na uchomaji wa makanisa.

  Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisema, "Vitendo hivi havifanani na utamaduni wetu Watanzania, wanaosifika kwa amani na utulivu."

  Aliwataka wananchi kuwa na subira yanapojitokeza matukio kama hayo na kwamba vyombo vya dola vitachukua hatua stahiki kwa wote waliohusika.

  ------
  Kwa namna ya ajabu, story hii na ya Tanzania Daima zinaonekana kufanana sana; ni kama mwandishi ni mmoja - Ref: https://www.jamiiforums.com/habari-na-hoja-mchanganyiko/337990-kikwete-pamoja-na-utoto-wake-kijana-alifanya-kosa-kubwa-kukojolea-msahafu.html
   
 2. K

  Kagalala JF-Expert Member

  #2
  Oct 14, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 2,372
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 145
  I hope atasahini kuuawa na waliomuua Mwangosi
   
 3. Annael

  Annael JF-Expert Member

  #3
  Oct 15, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 13,400
  Likes Received: 10,517
  Trophy Points: 280
  Hivi lini kweli JK aliahidi wauaji wa albino kunyongwa?
   
 4. C

  Chibolo JF-Expert Member

  #4
  Oct 15, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 2,975
  Likes Received: 1,391
  Trophy Points: 280
  Jamani hizi blabla hakuna kitu hapa!
   
 5. TZ biashara

  TZ biashara JF-Expert Member

  #5
  Oct 15, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 523
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Muuwaji auliwe
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  Oct 15, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280
  Ana matatizo makubwa zaidi; tulimkatalia wakati ule na kumwambia hana uwezo huo!!!
   
 7. S

  Savannah JF-Expert Member

  #7
  Oct 15, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 238
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sheria ya kipo ipo kwanini asiitumie kwa wahusika.
   
 8. Che Guevara

  Che Guevara JF-Expert Member

  #8
  Oct 15, 2012
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 1,178
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145
  Hapa napata kizunguzungu:
  Yaani Rais Kikwete alitaka watuhumiwa wanyongwe bila Mahakama kuthibitisha kama wana makosa au hapana???
  Eti aue mtu kisa ana hasira!
  Mhh... Kwa mtindo huu, tuiombee nchi yetu.
   
Loading...