Kikwete ni Mwanademokrasia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete ni Mwanademokrasia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kigarama, Nov 10, 2010.

 1. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #1
  Nov 10, 2010
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kiuhalisia Jakaya Kikwete sikumpigia kura, na hata kama atagombea tena kesho kwa kupambana na Dr. Slaa siwezi kumpa kura yangu. Kwa maoni yangu si mwanadamu anayefaa kuwa Rais Imara kwa kipindi hiki tulicho nacho.

  Lakini Kikwete anayo sifa nyingine ambayo wengi wetu hatutaki kuiona. Tofauti yake na mtangulizi wake B. Mkapa katika kutumia mitulinga ya dola kulinda chama chake ni kubwa sana.

  Wakati Mkapa alitumia Mitulinga ya dola komba kura za Kagasheki mwaka 2005 dhidi ya Lwakatare, Kikwete ametumia mbinu za medani kuzipata kura hizo. Hali ya joto la kisiasa lilivyokuwa mwaka huu sijui kama angekuwa Mkapa ndiye Rais ingekuwaje!?

  Kwa kiasi fulani Kikwete ni mwanademokrasia zaidi kuliko mtangulizi wake.
   
 2. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #2
  Nov 10, 2010
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,540
  Likes Received: 422
  Trophy Points: 180
  saaana . kwa hilo tunampongeza .
   
 3. Mabel

  Mabel JF-Expert Member

  #3
  Nov 10, 2010
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,018
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Kigarama,
  Naomba nifundishe kidogo maana halisi ya Demokrasia, na mwanademokrasi wa kweli anakuwaje, then nitarudi kwenye maada. Maana tayari umenichanganya.
   
 4. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #4
  Nov 10, 2010
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Vipi yale mabomu ya machozi kule Mbeya, Mwanza, Arusha, Shinyanga mjini, Kigoma mjini na Sumbawanga mjini?
  Au umepima Bukoba peke yake?
   
 5. M

  Mtama Member

  #5
  Nov 10, 2010
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  In short hakuna demokrasia mahali popote duniani,ila unaweza kuipata kwenye maandishi tu,hicho ni kitu cha kufikirika au cha nadharia tu,demokrasia ya kweli ipo mbinguni
   
 6. N

  Ngandema Bwila JF-Expert Member

  #6
  Nov 10, 2010
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 1,000
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Msingi wa demokrasia ni wengi wape, je ndivyo ulivyo tokea sumbawanga mjini, Kibaha, shinyanga mjini, Segerea. Mimi nampas sifa Mwema kwa kuanza kujenga jeshi la polisi lenye kuzingatia haki za binadamu. Kuna tofauti kubwa sana kati ya poilisi wa Saidi Mwema na wale wa Mahita. Japo bado kuna baathi ya polisi ni mbu mbu. mfano Kamanda wa Mkoa shinyanga, Daudi Siasi, alimshikilia Shibuda kwa siku tatu ndani,mpaka Manumba alikuja mtoa, huku akijua na kukili kuwa Shibuda hakuwepo eneo la tukiao la vurugu. Lkn alimhoji na kumwachia mgombea wa CCM aliyempiga ngwala na kumwangusha chin OCD wake kituoni.
   
 7. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #7
  Nov 10, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Mi naona ni heri mtu anayetumia physical means na wote mkaona, (maana bomu unaweza ukalala au kukimbia lisikupate)... Mbinu za kizayuni na kimafia za JK ni za hatari sana, maana sisi tunadhania anacheka, kumbe anatumaliza kijinsia(imagine habari ya kuingiza kura toka S/Africa)!..Sijui ni Demokrasia gani mwenzetu unaiongelea~!
   
 8. nginda

  nginda JF-Expert Member

  #8
  Nov 10, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 745
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  usitofautishe kati ya nyani na tumbili. Wote ni wezi wa mahindi.
   
 9. LoyalTzCitizen

  LoyalTzCitizen JF-Expert Member

  #9
  Nov 10, 2010
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,806
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 160
  Umekuwa honesty na maelezo ni mazuri sana mkuu Kigarama, labda tuelewe haswa nini maana ya demokrasia sababu maelezo ya Kigarama yamenitoa nje kabisa ktk maana halisi ya demokrasia! sababu personally i can not see JK practicing democracy! :sorry: remember we are talking about rule to the people, power to the people, human rights and equal rights at all times, open media, freedom to citizens, listening and engagements to citizens ....etc, etc which Tanzania is lacking!
   
 10. Double X

  Double X Senior Member

  #10
  Nov 10, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 184
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa wizi wa kura alioufanya uyu baba ridhiwan hana chembe ya kuitwa mwana demokrasia.
   
 11. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #11
  Nov 10, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  mimi kama mwanaharakati natoa big up kwa kikwete kwa kutokuwasakama watu wanaodai haki zao, wapinzani n.k. Ni kweli kwamba mabomu ya machozi yalitumika katika sehemu mbali mbali lakini maan halisi ya mabomu ya machozi ni kutawanya watu waliopewa amri ya kutawanyika wakakataa kutii amri hiyo. Hivyo huwezi kuhusisha matumizi ya mabomu ya machozi na mhe jakaya kikwete.

  Japo ulegevu wake wa kushughulikia mafisadi unanikera lakini kwenyesuala la kukuza demokrasia kwa maan ya kuwaachia wananchi uhuru wa kutoa maoni na kutenda watakayo yuko juu. Ni lazima tukiri jk nana kifua cha kuvumilia. Nafasi aliyonayo wangekuwa ni wengine miongoni mwetu sijui hata kama watu wangeweza kusema lakini wapo watu hudiriki hata kumuita fisadi lakini bado huvumilia.

  Suala la kura kuibiwa au kuchakachuliwa lipo popote hivyo kama wewe ni mwanasiasa unatakiwa kuwa makini. Soma thread ya regia mtema kushukuru hao waliokuwa wakitaka kumchakachua nao walitoka ccm?
   
 12. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #12
  Nov 10, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  zama za nyerere au mkapa hata huo wizi mngeweza kuujadili kama mnavyofanya sasa
   
 13. F

  Froida JF-Expert Member

  #13
  Nov 10, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Kikwete ana chuki na visasi angalia anavyotaka kumuangamiza Sitta,walimtosa Shibuda kwa kuwa alitaka kutumia haki yake ya kidemokrasia ya kugombea uraisi kwa tiketi ya CCM,hana demokrasia yeyote amtumia rafiki zake na familia yake kwenye kampeni huu ni uchu wa madaraka na uzandiki
   
 14. F

  Froida JF-Expert Member

  #14
  Nov 10, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Magazeti yaliyoandaliwa na KIKWETE,ROSTAM NA LOWASSA YA the express,Rai,Mtanzania,Majira ya wakati huo mbona walimuandama sana Mkapa na hakuyafunga kama kikwete alivyolifungua mwanahalisi na Alasiri
   
 15. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #15
  Nov 10, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Shibuda alikimbia mwenyewe kwa woga wake.

  Seriously speakin Shibuda is not a president material labda ndani ya Chadema
   
 16. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #16
  Nov 10, 2010
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,389
  Likes Received: 3,706
  Trophy Points: 280
  Kabaaaaaaaaaaaaaaaaa..........daaaaaaaaaaaaa .................. Hata kama mmoja anaiba huku anacheka na mwingine anaiba huku anagasira......bado wote ni wezi tena wa kitu kile kile.......MAHINDI YETU............
   
 17. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #17
  Nov 10, 2010
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,389
  Likes Received: 3,706
  Trophy Points: 280
  JAMBAZI.........MWIZI..............KIBAKA.................MKWAPUAJI................MPORAJI.................. jangili...............wote ni walewale tuuuu
   
 18. F

  Froida JF-Expert Member

  #18
  Nov 10, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Basi ingetamkwa hivyo kwenye vikao halali na ni wananchi wanoweza kusema nani si president material sio wewe na mimi ni ghiriba za KIKWETE ana roho ya korosho
   
 19. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #19
  Nov 10, 2010
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Napata hisia kuna watu hawaelewi maana ya democrasia, haina maana kuwapa shavu washkaji na familia.
  Angekuwa mwanademocrasia angetoka ikulu mwaka huu kuwapisha wengine maana alizidiwa.

  Mtikilila ndo anajua JK ni nani
   
 20. Antonov 225

  Antonov 225 JF-Expert Member

  #20
  Nov 10, 2010
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 310
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Naona mtoa mada alikuwa anajaribu kupima kati ya majangili hawa wawili yupi ni JAMBAZI, Halafu naona kuna watu akilini mwao tayari mmeshaanza kuwa brainwashed mpaka mnafikiri kuwa kuibiwa kidogo ama kupigwa na chelewa ni nafuu kuliko kupigwa na fimbo, kuweni free minded people jamani wewe hutakiwi kupigwa, usianze kujimegea megea kuonewa.
   
Loading...