Kikwete naye mchochezi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete naye mchochezi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Mar 20, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Mar 20, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 421,163
  Trophy Points: 280
  Kikwete naye mchochezi?
  [​IMG]

  Innocent Nganyagwa

  [​IMG] MAANDAMANO ya hivi karibuni ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika mikoa ya Kanda ya Ziwa, yameshitua baadhi ya viongozi. Pia mandamano hayo yamewashtua hata Watanzania wengi, wakiwamo CHADEMA wenyewe.
  Kuna baadhi ya watu ndani ya CHADEMA ambao bado walikuwa hawaamini jinsi wananchi walivyovutika na chama hicho, hasa baada ya matokeo ya kura za urais katika uchaguzi mkuu uliopita kutangazwa.
  Lakini zaidi maandamano hayo yaliwashtua watawala. Chama Cha Mapinduzi (CCM) na serikali yake wanaonekana walishituka vilivyo. Hali hiyo ilijidhihirisha kutokana na jinsi ambavyo walionekana kuijibu CHADEMA kwa hoja ambazo hazikuwa na mashiko.
  Hakuna aliyeamini kuwa bado CHADEMA ilikuwa na mvuto kiasi kile. Lakini baada ya kuona umati wa Watanzania, ambao ulikwenda kwa hiari yao bila kushawishiwa na kitu chochote kusikiliza ujumbe ulioletwa na wale wanaoamini kuwa ni wakombozi wao, CCM na serikali wakatahamaki!
  Ni dhahiri kuwa walikuwa wakiamini kuwa baada ya uchaguzi, chama hicho cha upinzani kilikuwa ‘kimekwisha’ na kuwa kingetumia muda mwingi kujipanga ili kurejea katika ulingo wa siasa za ushindani.
  Lakini kikubwa kilichowashitua watawala ni ujumbe uliotoka vinywani mwa viongozi wa CHADEMA walioshiriki katika maandamano yale.
  Ujumbe wao ulikuwa muruwa, uliowafurahisha wananchi na kuwaacha wakiwa na matumaini kuwa mkombozi wao bado hajafa kama ambavyo walikuwa wakiaminishwa.
  Hali hii ndiyo iluyoifanya CCM na serikali yake ione kuwa wananchi wamechochewa.
  Hilo wala si la kujificha, ni kweli wananchi walikuwa wamechochewa. Lakini kutokana na kutazama mambo kwa macho ya makengeza, CCM na serikali ikaona kuwa CHADEMA na viongozi wake ndio walikuwa wamewachochea wananchi. Kumbe sivyo.
  Walianza wapambe wadogo wadogo, makada wa CCM na viongozi wa serikali, wakiwamo mawaziri wakiwashambulia CHADEMA kuwa mandamano yao yalikuwa na maana nyingine zaidi ya kile wanachokieleza hadharani. Walisema kuwa CHADEMA imedhamiria kuwachochea wananchi wakichukie CCM na serikali.
  Baadaye, Mwenyekiti wa Taifa wa CCM na Rais, Jakaya Kikwete naye akamalizia shutuma hizo kwa kubainisha kuwa CHADEMA walikuwa wamelenga kuleta machafuko nchini.
  Hawa wote, kilichowafanya waingie uwoga ni jinsi wananchi walivyojitokeza kwa wingi kuiunga mkono CHADEMA bila kurubuniwa na kitu chochote kama vile vikundi vya burudani, fulani, kofia, kanga au kubebwa na magari hadi kwenye viwanja vya mikutano. Watu walijitoa kwa hiari kushiriki mandamano na mikutano ya CHADEMA.
  Hivi CCM wanadhani kuwa ni kazi ya CHADEMA kuwashawishi wananchi wakipende chama hicho? Kama chama mbadala cha siasa, jukumu kubwa la CHADEMA ni kuiondoa CCM madarakani ili chenyewe kipate fursa ya kuunda serikali na kutekeleza sera zake. Wanaweza kufanya hivyo kwa kuonyesha ubaya wa CCM na jinsi ilivyoshindwa. Baadaye, CHADEMA ikijionyesha kwa wananchi kuwa ina uwezo wa kuyafanya yale ambayo CCM imeshindwa.
  Na ujumbe waliokuwa wakiutoa CHADEMA ulikubalika kwa wananchi. Mbaya zaidi, ujumbe waliokuwa wanautoa CHADEMA ni tofauti na ule uliowahi kutolewa na CCM.
  Wakati CCM waliahidi kuboresha maisha ya Watanzania, CHADEMA wakaja kuwaeleza wananchi kuwa hali si hivyo.
  Na kwa hakika, wala haihitaji CHADEMA au mtu mwingine yeyote yule kuwaonyesha Watanzania kuwa wamepigika. Kwamba ahadi ya maisha bora haijatekelezwa, si suala la siri linalohitaji hotuba za majukwaani. Kila Mtanzania, ukiondoa wale wachache ‘wenye nchi’, ni shuhuda wa hali ngumu ya maisha.
  Labda walichofanya CHADEMA ni kuwakumbusha tu kuwa hali ya maisha imekuwa ngumu kutokana na mfumko wa bei. Gharama za maisha zimepanda kuliko uwezo wao. Bei za bidhaa muhimu kwa ajili ya maisha yao hazikamatiki tena wakati vipato vyao havijapanda kwa muda mrefu.
  Ujumbe huu, ambao ni dhahiri kwa yanayotokea katika maisha ya kila siku ya Watanzania, ndiyo ambao Rais Kikwete na wenzake ndani ya CCM na serikali, waliona kuwa ni uchochezi.
  Kauli hizi za CCM na serikali nimezielewa kwa maana moja tu kuwa walichokisema CHADEMA si kitu cha kweli. Lakini akili zisizoathiriwa na kitu chochote kama za kwangu, zinakataa kukubali kuwa wananchokisema CHADEMA si cha kweli kwa sababu hayo yanayosemwa ni sehemu ya maisha ya kila siku ya Watanzania wengi.
  Lakini Mungu hamfichi mnafiki kwani siku chache baadaye, tumeshuhudia mabadiliko ya ajabu.
  Baada ya kumaliza majukumu yake ya kusuluhisha mgogoro wa Ivory Coast pamoja na marais wenzake kadha, Rais Kikwete sasa amepata muda wa kuanza kutembelea wizara na taasisi mbalimbali za kitaifa.
  Lengo kubwa, kama tulivyoelezwa, ni kufuatilia utekelezaji wa maagizo yake aliyotatoa yapata miaka mitano iliyopita mara baada ya kuchaguliwa kuwa Rais katika awamu yake ya kwanza ya uongozi.
  Alipokuwa Wizara ya Fedha, rais alitoa maagizo akiitaka wizara hiyo kuhakikisha kuwa mfumuko wa bei unashushwa haraka iwezekanavyo. Niliposikia hivyo nikashindwa kuamini. Huo mfumko anaosema kuwa ushushwe ni upi?
  Mbona CHADEMA juzi juzi hapa waliwaeleza wananchi kwenye mikutano yao kuwa mfumko wa bei uko juu na wakaambiwa kuwa wanafanya uchochezi? Kuwaambia CHADEMA kuwa walikuwa wanaanya uchochezi kwa kauli yao kuwa mfumko wa bei uko juu, ilimaanisha kuwa anachokisema si cha kweli.
  Sasa kimetokea nini katika siku hizi chache hadi leo ionekane kauli ile ya CHADEMA ilikuwa kweli na agizo kutolewa na mkuu wa nchi kuwa mfumko ushushwe?
  Alipokuwa Bandarini na sehemu nyingine alizotembelea hadi hivi sasa, maagizo yake mengi alilenga kuleta ahueni katika hali ngumu za maisha ya Watanzania.
  Haiyumkini kuwa mtu anaweza kutoa maagizo yanayolenga kuboresha maisha yaliyo bora. Sasa kama CHADEMA walipoyasema haya walionekana wachochezi, viongozi wa nchi wanayazungumzia hayohayo sasa tuwaeleweje?
  Au Kikwete naye ameamua kuwachochea wananchi kama CHADEMA?
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Mar 20, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 421,163
  Trophy Points: 280
  PHP:
  Sasa kimetokea nini katika siku hizi chache hadi leo  ionekane kauli  ile ya CHADEMA ilikuwa kweli na agizo kutolewa na mkuu  wa nchi kuwa  mfumko ushushwe?
        
  Alipokuwa Bandarini na sehemu nyingine alizotembelea hadi hivi sasa,   maagizo yake mengi alilenga kuleta ahueni katika hali ngumu za maisha ya   Watanzania.
      
  Haiyumkini kuwa mtu  anaweza kutoa maagizo yanayolenga kuboresha maisha  yaliyo boraSasa  kama CHADEMA walipoyasema haya walionekana  wachocheziviongozi wa nchi  wanayazungumzia hayohayo sasa tuwaeleweje?
       
  Au Kikwete naye ameamua kuwachochea wananchi kama CHADEMA?
  Msema kweli hawezi kuwa mchochezi...............................ugumu wa maisha uliosababishwa na ubutu wa uwezo wa kufikiri na uongozi duni uliokithiri ubinafsi ndivyo vimeiporomosha CCM na kuijenga Chadema......................
   
 3. DCONSCIOUS

  DCONSCIOUS JF-Expert Member

  #3
  Mar 20, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 1,272
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  patamu hapo
   
 4. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #4
  Mar 20, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Uchambuzi makini, sijui kama umemfikia mkwere:smash:!!!
   
 5. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #5
  Mar 20, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  your very right!!
   
Loading...