Kikwete na CCM Kuendelea Kuwanyima Watanzania Katiba Mpya kwa Miaka 5 ijayo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete na CCM Kuendelea Kuwanyima Watanzania Katiba Mpya kwa Miaka 5 ijayo

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Mbunge, Oct 29, 2010.

 1. M

  Mbunge Senior Member

  #1
  Oct 29, 2010
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 104
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  KWA mujibu wa kauli ya Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi, Bw. Jakaya Kikwete yeye na chama chake hawana mpango wa kuridhia Watanzania kuwa na Katiba Mpya kwa miaka mitano ijayo.
  Katika Mahojiano ya kirafiki na Redio Clouds FM pengine na Televisheni (Sikuiona kwa kuwa siipati) mgombea huyu amesema kama kawaida ya chama chake kinachopenda kutumia viraka kwenye sheria, kanuni na mifumo mbalimbali CCM itaendelea kuweka viraka kwa miaka yote kitakapokuwa madarakani.
  Vyama vyote Mbadala nchini vimeahidi kuwapatia Watanzania Katiba Mpya ndani ya miaka michache kama vitaingia Ikulu.
  Katiba Mpya ni madai ya Watanzania wengi ambao wanaiona katiba iliyopo sasa ni ya chama kimoja na haizingatii kwa mapana na marefu kuwepo kwa mfumo wa vyama vingi hivi leo.
  Tamko la kwamba CCM haina mpango wa kuruhusu kuwepo kwa katiba mpya halitapokelewa kama lilivyo na upo uwezekano mkubwa wa wanaharakati nchini wakiongozwa na wanasheria huru na Watanzania waliojaliwa kuona mbali na mbele wataingia kambini kuanza kuandaa Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ili kuweza kukidhi mahitaji na matarajio ya kizazi kipya cha Watanzania.
  Kwa kutolea nje haja ya kuwepo kwa katiba mpya itakayokubalika na Watanzania wote bila kinyongo wala dharau ni hoja ya mwanzo katika kuleta mustakabali mpya kwa taifa ambalo kwa sasa linaelekea halina dira na maamuzi mengi yanafanywa kialwatani bila kufuata ushauri wa wataalamu wanaotegemewa katika masuala husika.
  Kukataa katiba mpya kama alivyofanya Bw.Kikwete kunaashiria kiburi cha CCM na mtazamo wao kwamba wao ndio baba na mama wa Watanzania na kwamba wakitakacho wao tu ndicho kinachoweza kufanyika. Haiyumkiniki kwa kizazi cha leo kama walivyokuwa wazazi wao kuswagwaswagwa kama vile mbuzi au kondoo au ng'ombe.
  Ni uamuzi ambao pia utachelewesha maamuzi makubwa kama vile kulipa bunge uwezo na mamlaka zaidi kuliko ilivyo hivi sasa; kuwepo kwa Tume huru ya Uchaguzi na kukubalika kwa Mgombea binfasi katika chaguzi za nchi hii.
   
 2. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #2
  Oct 29, 2010
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hapa ndipo umakini wa Mgombea makini unapobainika,kwa hata gari likigongwa na rangi ikachubuka badala ya kweka viraka vya rangi hupigwa rangi upya ili iwe nadhifu.
   
Loading...