Kama JK ndy rais bora katika historia ya TZ mpaka sasa, basi hii nchi haijawahi kupata rais.
Ndo maana hamuelewi kila siku;
Sijui hata kama unachangia hata shilingi kwenye
kodi; nyie ndo wakwepaji kodi na majungu kibao;
Napenda Tanzania napenda CCM.
JK amejitahidi sana kujenga miundombinu japo hela zenyewe za madeni na sijui atakuja kulipa nani.
barabara ya kutoka singida hadi arusha ni moja ya sehemu zilikuwa zinaniudhi sana!!
HONGERA JK JAPO CCM mwisho wao ni 2015
Tunasubiri meli ya ziwa nyasa, TAnganyika na reli ya umeme kutoka dar hadi kigoma. maji kutoka ziwa victoria hadi tabora usijidai umesahau mkuu wa nchi
Mkuu kama watanzania tungekuwa ni watu wenye kufatilia mambo tungejua ni kwanini angalau barabara zinajengwa? Hivi nchi masikini kama Tanzania inaweza kuiacha reli ife halafu ielekeze nguvu zake kwenye kujenga barabara kweli! Hakuna nchi yenye viongozi sahihi inaweza kununua huu ujinga ni Tanzania tu hili linaweza kutokea!
Hebu tujiulize kwanini barabara lakini siyo reli? Mwakyembe amepiga tambo weeee lakini mkulu hakuna hata siku moja ameonyesha kumuunga mkono! Kuna agenda gani kwanini reli haitakiwi kufufuka? Ni kweli barabara ni rahisi kusafirishia makontena toka dar mpka mwanza,kigari, burundi, kongo nk? Ni kweli tunahitaji barabara kwa ajili ya kuwafikia wakulima kwa urahisi lakini je tunaweza kujenga uchumi mkubwa kwa kusafirisha mizigo kwa barabara kweli?
Magufuli amekuwa akilialia kuhusu magari makubwa kuharibu barabara lakini hata siku moja hadhubutu kusema hilo mbele ya raisi ni kwanini? Anaogopa nini? Kuna masilahi gani kwenye barabara? Barabara zenyewe za mkopo na zimeishi sana ni miaka 2-3 baada ya hapo ni vumbi kama kawaida!
Kwa nini tusiwe na reli imara kwanza ambayo itahakikisha mizigo yote mizito haitatumia barabara na hivyo barabara zitakazojengwa zitadumu kuliko hivi sasa tunajenga barabara za mkopo halafu ndani ya miaka 2 zimechoka na mkopo bado haujalipwa! Nani atakuja kulipa haya madeni ambayo hata investiment zake hazitakuwepo wakati wa kudaiwa?
Kwa maoni yangu raisi anafanya tu ilimradi yeye anatimiza ahadi zake bila kujali hasara na mzigo atakaotuwachia! Kama anataka akumbukwe kweli basi ajenge kwanza reli ili barabara zitakazo jengwa zidumu na mikopo ile ijekulipika bila maswali maana investiment zake zitakuwa bado zinaonekana na kila mtu!
Tunasubiri miaka 2 Kigoma iwe kama Dubai
Tunasubiri reli ya kati ya kisasa - train iendayo kwa kasi.
Yapo Shinyanga yanaelekea Nzega, Nzega ni wilaya ya mkoa gani?
wa kwanza kukumbuka ni dr slaa na freeman mbowe. hawa watu kila kukicha wanamtukana lakini kimoyomoyo wanampongeza. nakumbuka siku ile wakati JK alipofanya ziara yake jimboni kwa mbowe aliposhindwa kuzuia hisia zake na kutamka maneno yafuatayo: mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Jk kajenga marabara nzuri jimboni kwangu kuliko marais waliomtangulia. mwisho wa kunukuu
Tunasubiri miaka 2 Kigoma iwe kama Dubai
. Mkipewa ukweli mnasema ni mipasho.Hiyo ni Mipasho tu kama ya Hadija Kopa...
Hebu sikiliza huu mpasho mwingine hapa...View attachment 111470
Deni aliloacha mkapa lilikuwa trillion 6...kilaza kikwete kaongeza deni mpaka sasa trillion 25...then anajigamba eti kaleta maendeleo...pesa za mikopo zinatumika kwenye campaign za ccm, plus uchakachuaji then anadanganya wananchi kwa hizo barabara zinazojengwa kwa kiwango duni cha chini kabisa sijapata ona popote pale duniani.kweli kikwete ni janga kubwa la taifa. Mpaka amalize muhula wake deni litakuwa trillion 30 na hazitajulikana ziliko...kikwete ni mtu mbaya sanaaa hafai hata kidogo.