Kikwete majaribu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete majaribu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, Sep 10, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Sep 10, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,522
  Likes Received: 81,918
  Trophy Points: 280
  Kikwete majaribu

  Mwandishi Wetu Septemba 10, 2008
  Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo

  CHAMA cha Mapinduzi (CCM) bado kinasukwasukwa, na safari hii tatizo kubwa ni hatua ya Jumuiya ya Vijana wa chama hicho (UVCCM) kutangaza kumtema mwenzao, Nape Nnauye, Raia Mwema imeambiwa.

  Nnauye, mtoto wa mwanasiasa maarufu, Moses Nnauye (sasa marehemu), amekuwa katika chati za juu za vyombo vya habari kwa muda sasa tangu atangaze kuwania uenyekiti wa UVCCM ambao sasa unashikiliwa na Emmanuel Nchimbi anayeondoka kwa sababu ya umri.

  Wiki hii, taarifa ya Nchimbi ilieleza kwamba Nnauye amefutwa uanachama wa UVCCM kwa kukiuka kanuni za umoja huo na taarifa zaidi zimekuwa zikisema kwamba sasa suala lake itabidi lifike katika ngazi nyingine za juu za chama hicho tawala; Kamati Kuu na Halmashauri Kuu, kwa kuwa yeye mwenyewe amekuwa akisema UVCCM si mwisho.

  Dhambi ya kijana huyo ni maoni yake kwamba kulikuwa na walakini na dalili za ufisadi katika uamuzi wa uwekezaji katika kiwanja cha umoja huo, Barabara ya Morogoro, Dar es Salaam na kwamba Bodi ya Wadhamini haikuwa imetenda haki katika kutoa kiwanja hicho.

  Baadhi ya wanasiasa, wakongwe na wengineo, wamekuwa wakiuona uamuzi wa kumfukuza kijana huyo kama unaorudisha nyuma demokrasia iliyokwisha kuanza kujijenga ndani ya CCM na ambayo chama hicho kimekuwa kikiiimba sana nje ya mtandao wake.

  Wanasema hatua hiyo ambayo imekuwa ikitangazwa sana na Katibu Mkuu Yusuf Makamba ni kama inaashiria kwamba Nnauye, kwa kusema maoni ya moyoni mwake, ametenda dhambi kubwa kushinda zote ndani ya chama hicho na ambayo haisameheki.

  Makamba, ambaye naye amekuwa akipingwa na baadhi ya watu ndani ya CCM wengine wakipendekeza apumzishwe kwa kuwa katika kipindi chake kifupi cha ukatibu mkuu kimeshuhudia maamuzi kadhaa ya kupindapinda, ameviambia baadhi ya vyombo vya habari kwamba Nnauye, hawezi kusamehewa hata mbinguni.

  Amenukuliwa Makamba akisema kuhusu kufukuzwa huko kwa Nnauye: “Imeandikwa kwenye Biblia kwamba mtakaowafungia duniani wamefungiwa na mbinguni”.
  Jaji Joseph Warioba

  Baadhi ya waliozungumzia suala hilo ni pamoja na Jaji Joseph Warioba, kijana wa zamani na mwanasiasa mkongwe ambaye ameiambia Raia Mwema kwamba haya yaliyofanyika kwa Nnauye, kama hatimaye ndiyo yatakayopitishwa, yatakuwa yakienda nje ya utaratibu wa chama anachokijua yeye.

  Alisema Warioba: “Kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) nilichokuwa nakijua, kwa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) niliokuwa naujua, sikutarajia wangechukua hatua kama hiyo na kwa sababu walizotoa.

  “Kama alitoa kauli za kupinga jambo lililokuwa linahusiana na Umoja huo si ajabu. Mbona ndani ya CCM kwenyewe kumekuwa na kauli nzito zilizosemwa na watu hao hawakufukuzwa, bado wamo.”

  Aliongeza Warioba katika mahojiano ya simu kuhusiana na hatua hiyo: “ Lakini kweli yeye anaweza kuwa ameusema vibaya UVCCM au CCM kushinda Wapinzani ambao wamekuwa wakitusema vibaya muda wote?

  “Na licha ya kusemwa huko na Wapinzani sisi wenyewe mbona tumekuwa na utaratibu wa kuwasaka mamluki katika Upinzani, waliotukana sana CCM, kwa mbwebwe tukawakumbatia katika chama?

  “Sasa lipi ni zito, kumkumbatia kwa mbwembwe aliyekuwa akiitukana sana CCM nje akiwa mpinzani, ambaye amekaribishwa kwa vifijo, au mwanachama anayeamua kusema kile kilichokuwa kinasemwa na hao tuliowachukua kutoka Upinzani?

  “Mtindo huu maana yake ni kwamba aliyeko nje anakaribishwa, aliyeko ndani anafukuzwa. Na bahati mbaya Katibu Mkuu amehusika sana katika hili. Amekuwa akikaribisha wapinzani. Kwa mwendo huu wana CCM watatupwa nje, wapinzani ndio watakuwa wana CCM.

  “Demokrasia yetu ndani ya CCM imekwenda wapi? Hili ni suala la Vijana, inakuwaje Katibu Mkuu analivalia njuga? Na wala si Vijana tu, hata jumuiya nyingine za CCM zimeingiliwa sana katika siku za karibuni na CCM yenyewe. Ni kana kwamba kuna mpango wa kuengua baadhi kwenye chama na kutafuta wengine”.

  Cleopa Msuya

  Juzi mkongwe mwingine Cleopa Msuya alieleza kushangazwa kwake na uamuzi wa kumfukuza Nnauye akisema kwamba naye alikuwa ametafuta sababu za hatua hiyo bila mafanikio.

  “Wangekuwa angalau wamemsimamisha (awali) uanachama wa Umoja wa Vijana tungeshangaa kidogo, lakini kumfukuza… nimeshangaa… wanaposema avuliwa nyadhifa zote maana yake nini? Yule ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, kofia hiyo nayo avuliwe? Hapa hoja ni kosa lake la kuhoji mradi wa jengo la UVCCM au kuna jambo jingine,” amekaririwa akisema mzee Msuya.

  Lakini wachungzi wa mambo wameiambia Raia Mwema kwamba hatua hii ni matokeo ya kuiva kwa migongano ya kimakundi yanayoendeshwa ndani ya CCM ya leo ya wanasiasa wafanyabiashara na wapambe wao na mengine yenye kutafuta wala haki kidogo.

  Wanasema kwamba kuna uwezekano mkubwa kwamba makundi haya si tu kwamba yamemyumbisha Katibu Mkuu, bali yanamsukasuka hata Mwenyekiti, Jakaya Kikwete.

  “Ni makovu ya mchakato wa uchaguzi uliopita. Anaposimama Nnauye akasema wazi kwamba Mwenyekiti wa Wadhamini UVCCM, Edward Lowassa anahusika katika sakata ya kiwanja, usitarajie Lowassa au wapambe wake, ndani ya UVCCM na nje watakaa kimya,” anasema mwanasiasa mmoja akiongeza kwamba Lowassa na Nnauye ni sura wakilishi za makundi mawili makuu kinzani ndani ya CCM.

  Anaongeza mwanasiasa huyo: “ Kwamba Nnauye ameanika suala hilo la jengo na ukweli kwamba kuna timu ya wanasheria kuhusiana na mradi huo na ukweli pia kwamba katika uchaguzi wa mwaka 2005 Nnauye hakuonekana kuwa upande wa Mwenyekiti wa sasa, maamuzi yoyote ya juu yataangalia zaidi mlengo huo”.

  Mjumbe mmoja wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) wa Kanda ya Ziwa ameiambia Raia Mwema kwamba alichofanya Nnauye ni kama "kuchokoza tu, lakini mikakati ilikuwa inakwenda kwa siri na kichinichini na inakwenda mbali zaidi hadi katika kuwashughulikia wale wote wanaohusika na kupiga vita miradi kama hiyo ya jengo la Vijana”.

  Kabla ya sakata la Nnauye kufikia hapa lilipo, skandali zilizokuwa zimeshika uongozi ni pamoja na za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) na mradi hewa wa umeme wa Richmond ambayo ufumbuzi wake haujakata kiu yote ya wengi.

  "Rais alipozungumzia Richmond kwa wepesi na kuona kama hakuna makosa, tulichanganyikiwa. Baadaye Waziri Mkuu Mizengo Pinda alipowasilisha taarifa ya Serikali ilikuwa ni kana kwamba Serikali imebadili mwelekeo,” anasema mbunge mmoja.

  Kuhusu suala la Nnauye mbunge huyo ambaye ni mjumbe wa NEC, alisema kwa siku kadhaa kabla na baada ya kikao cha UVCCM kuchukua uamuzi wa kumdhibiti Nnauye, kulikuwa na heka heka nchi nzima na baadaye kuhitimishwa na matumizi makubwa ya fedha katika kuhakikisha kijana huyo anadhibitiwa.

  "Waliwatafuta wenyeviti wa mikoa wa UVCCM, wakimtumia mwenzao mmoja na baadaye kumtumia mbunge mmoja kijana katika kufanikisha hilo. Kwa kweli nimethibitishiwa kuhusu fedha zilizomwagwa," anasema mjumbe mmoja wa Baraza Kuu la UVCCM.
   
Loading...