Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 40,000
Mkuu Mwanakijiji;
...
Ndege moja ya Aribus ambayo sisis tulikuwa tunakodi(iliyotimika) bei yake ikiwa mpya ni dola million 50 ba inachukua muda wa miaka mitatu mpaka unakabidhiwa ndege yao;Jiulize serikali ilikuwa inakodi kwa bei gani?mara mbili zaidi ya bei ya kununulia
tatu,Mpaka leo mashirika haya pamoja na interview kufanyika na faili kupelekwa kwa mkuu ila hajateua watendaji wa mashirika haya;sijui muungwana anafanya kazi gani
1.Mkurugenzi wa Consolidated Holdings Corporation(miaka miwili)
2.Mkurugenzi wa National Insurance Corporation(NIC)
3.Mkurugenzi wa TANESCO
4.Mkurugenzi wa TTCL
5.Mkurugenzi wa ATCL
Hao wote nafasi zao ziko acted kwa muda mrefu na hakuna maamuzi yoyote yanayofanyika;watu hawahoji kwanini inachukua muda mrefu ila hii yote ni kwasasabu tunapenda mapmbo mepesi mepesi
Shirika la NBC tunatakiwa kuteua Mwenyekiti wa Bodi ila mpaka sasa yule Mpungwe anakaimu ;matokeo yake kunakuwa na maamuzi mabovu sana katika kufanikisha
Hapo bado kuna mambo mengi yanakwama tu ukiangalia hata Luhanjo muda wake umeisha ila naye sijui nani kamuongezea muda wa kukaa pale ila anatakiwa kustaafu;
suala la mambo mepesi mepesi limenikumbusha haya
Unajua tatizo moja la kupenda kuzungusha watendaji (recycling) ni kuwa unaweza ukafika mahali ukakuta hauna watu wa kuwazungusha tena. Sasa inabidi utegee tu. Kuna katabia ambako kamekubalika kuwa nafasi fulani za juu bado ni za kundi fulani la watu na hivyo ni hao hao watazungushwa kiasi kwamba wale makada wa ngazi ya kati ni vigumu kwela kupasua paa hilo la nafasi za juu.
Matokeo yake Mkurugenzi wa taasisi moja kubwa anahamishwa na kuwa Mkurugenzi wa taasisi nyingine na vivyo hivyo hadi inafika mahali wanapofika wakati wa kustaafu hatuko tayari wastaafu kwa sababu hatuna watu wengine wa kuingia katika nafasi hizo. Matokeo yake waliostaafu wanaoengezewa muda zaidi si kwa sababu wanahitajika sana la hasha; kwa sababu "hakuna" watu wa kuchukua nafasi zao.
Lakini hili pia linaelezea matokeo ya tatizo jingine ambalo naweza kusema ni sehemu ya "gharama ya ufisadi". Unapokuwa na mfumo wa kiutawala wa ufisadi (MUK) waliomafisadi na makuwadi wao ni wengi sana kwenye system kiasi kwamba ikitokea nafasi nyeti ya kujaza ni vigumu mno kwa sababu wale wote ambao unafikiria wajaze nafasi hizo tayari wana harufu ya ufisadi fisadi.
Pia ni dalili ya mfumo mbaya ambapo hata wakurugenzi wa makampuni ambayo hayahusiani na utendaji wa serikali moja kwa moja wanateuliwa na Rais! Kwanini mtendaji wa Shirika la Bima ateuliwa na Rais? Kwanini mtendaji wa Shirika la Tanesco ateuliwe na Rais? Vipi mtendaji wa ATCL ateuliwe na Rais na wakati huo huo Rais anatakiwa ateue Mkuu wa Usalama wa Taifa n.k ?
Kama wabunge wetu wangeamua kufikiri kidogo wangeondoa mzigo huu wa uteuzi kwenye makampuni yafanyayo biashara ili wakurugenzi wake waingie kwa kushindanishwa (kuomba) na kuteuliwa na Bodi ya Wakurugenzi ambayo nayo iundwe na wadau siyo na wanasiasa.
Matokeo yake Mtawala anaamua Kusettle; yaani kuteua mtu yule ambaye aidha ni fisadi "mdebe mdebe" (mdogo) au fisadi asiyejulikana sana. Na hili linaweza kuelezea kwanini hadi leohii Rais Kikwete anapata shida ya kuachia watu wastaafu na kuteu watendaji wengine.
Hebu angalia taarifa hii kutoka katoto ka "nzi"...
Hakuna lolote sio vetting process. Kama kuna vetting mbona kunatakataka kibao zinaingia kwenye processing system. Hiyo sasa ni vetting gani?Lakini kweli kuna ugumu wa kujaza nafasi hizi au ndiyo vetting process ni ndefu kiasi hiki?
Mzee Mwanakijiji,
Kuna Power Struggle Tanzania ambayo imeota mizizi kotoka vyama vya kisiasa, kuelekea Serikalini na mpaka kwenye Taasisi.
Badala ya kuwa na Utamaduni wa kuchagua watu on merit basis, tunachagua watu kutumia loyalty and pleasing!
Labda anasubiri wale watakaomchangia bulungutu kubwa kwenye kampeni zake za 2010 wampe majina ya nani wanaofaa katika nafasi hizo. Si unakumbuka huyo Rweyemamu aliingizwa Ikulu kupitia mgongo wa Rostam, basi nafasi hizo labda zimeachwa ili akina Rostam, Jeetu, Manji, Subhash Patel na wengineo wakishatoa mabilioni yao wampe na majina ya wale watakaofaa kupewa nyadhifa hizo nzito.
Huenda marafiki wa kuwapa hizo nafasi wameisha ndo tusubiri hadi baada ya uchaguzi ila hii inaonesha kwa jinsi gani tunaongozwa kisanii nchi makini na kiongozi makini hawezi weka viporo.
Swala la kuwa CCM imeshiaka utamu si la kuhiji lipo wazi sana na yule aliyesema mawazili wanajibu mbofumbofu angesema tu selikali yetu ni mbofumbofu maana hakuna hata kero moja ya wapiga kura Jk anaweza kujigamba na kusema amerekebisha zaidi ya kupindukia kuwa Vasco Dagama.Ndiyo ari mpya, kasi mpya na nguvu mpya ya msanii wetu hiyo. Nchi nyingine asingeruhusiwa kugombea kutokana na utendaji wake dhaifu lakini kwetu tunaambiwa chama chake kina utamaduni wa kumuachia aliyeko madarakani akae awamu mbili bila kujali maslahi ya nchi hata kama anavurunda vipi. Kweli CCM imeshika utamu. Kigumu chama cha map...Ooops! cha mafisadi! Kigumu!
Hata vile viti maalumu 10 vya wabunge hajamaliza kuteua 4 years down the road........
umenikumbusha aisee.. nadhani kulikuwa na nafasi mbili za wazi!!
umenikumbusha aisee.. nadhani kulikuwa na nafasi mbili za wazi!!
Unajua tatizo moja la kupenda kuzungusha watendaji (recycling) ni kuwa unaweza ukafika mahali ukakuta hauna watu wa kuwazungusha tena. Sasa inabidi utegee tu. Kuna katabia ambako kamekubalika kuwa nafasi fulani za juu bado ni za kundi fulani la watu na hivyo ni hao hao watazungushwa kiasi kwamba wale makada wa ngazi ya kati ni vigumu kwela kupasua paa hilo la nafasi za juu.
Matokeo yake Mkurugenzi wa taasisi moja kubwa anahamishwa na kuwa Mkurugenzi wa taasisi nyingine na vivyo hivyo hadi inafika mahali wanapofika wakati wa kustaafu hatuko tayari wastaafu kwa sababu hatuna watu wengine wa kuingia katika nafasi hizo. Matokeo yake waliostaafu wanaoengezewa muda zaidi si kwa sababu wanahitajika sana la hasha; kwa sababu "hakuna" watu wa kuchukua nafasi zao.
Lakini hili pia linaelezea matokeo ya tatizo jingine ambalo naweza kusema ni sehemu ya "gharama ya ufisadi". Unapokuwa na mfumo wa kiutawala wa ufisadi (MUK) waliomafisadi na makuwadi wao ni wengi sana kwenye system kiasi kwamba ikitokea nafasi nyeti ya kujaza ni vigumu mno kwa sababu wale wote ambao unafikiria wajaze nafasi hizo tayari wana harufu ya ufisadi fisadi.
Pia ni dalili ya mfumo mbaya ambapo hata wakurugenzi wa makampuni ambayo hayahusiani na utendaji wa serikali moja kwa moja wanateuliwa na Rais! Kwanini mtendaji wa Shirika la Bima ateuliwa na Rais? Kwanini mtendaji wa Shirika la Tanesco ateuliwe na Rais? Vipi mtendaji wa ATCL ateuliwe na Rais na wakati huo huo Rais anatakiwa ateue Mkuu wa Usalama wa Taifa n.k ?
Kama wabunge wetu wangeamua kufikiri kidogo wangeondoa mzigo huu wa uteuzi kwenye makampuni yafanyayo biashara ili wakurugenzi wake waingie kwa kushindanishwa (kuomba) na kuteuliwa na Bodi ya Wakurugenzi ambayo nayo iundwe na wadau siyo na wanasiasa.
Matokeo yake Mtawala anaamua Kusettle; yaani kuteua mtu yule ambaye aidha ni fisadi "mdebe mdebe" (mdogo) au fisadi asiyejulikana sana. Na hili linaweza kuelezea kwanini hadi leohii Rais Kikwete anapata shida ya kuachia watu wastaafu na kuteu watendaji wengine.
Hebu angalia taarifa hii kutoka katoto ka "nzi"...
Wa mwisho alikuwa yule mama Albino. Jina lake gumu kidogo. Jimbo la Ikulu nadhani imebaki nafasi moja.Yes wa mwisho alikuwa Mwang'onda bado 3
wa mwisho alikuwa yule mama albino. Jina lake gumu kidogo. Jimbo la ikulu nadhani imebaki nafasi moja.