Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
Unajua tatizo moja la kupenda kuzungusha watendaji (recycling) ni kuwa unaweza ukafika mahali ukakuta hauna watu wa kuwazungusha tena. Sasa inabidi utegee tu. Kuna katabia ambako kamekubalika kuwa nafasi fulani za juu bado ni za kundi fulani la watu na hivyo ni hao hao watazungushwa kiasi kwamba wale makada wa ngazi ya kati ni vigumu kwela kupasua paa hilo la nafasi za juu.
Matokeo yake Mkurugenzi wa taasisi moja kubwa anahamishwa na kuwa Mkurugenzi wa taasisi nyingine na vivyo hivyo hadi inafika mahali wanapofika wakati wa kustaafu hatuko tayari wastaafu kwa sababu hatuna watu wengine wa kuingia katika nafasi hizo. Matokeo yake waliostaafu wanaoengezewa muda zaidi si kwa sababu wanahitajika sana la hasha; kwa sababu "hakuna" watu wa kuchukua nafasi zao.
Lakini hili pia linaelezea matokeo ya tatizo jingine ambalo naweza kusema ni sehemu ya "gharama ya ufisadi". Unapokuwa na mfumo wa kiutawala wa ufisadi (MUK) waliomafisadi na makuwadi wao ni wengi sana kwenye system kiasi kwamba ikitokea nafasi nyeti ya kujaza ni vigumu mno kwa sababu wale wote ambao unafikiria wajaze nafasi hizo tayari wana harufu ya ufisadi fisadi.
Pia ni dalili ya mfumo mbaya ambapo hata wakurugenzi wa makampuni ambayo hayahusiani na utendaji wa serikali moja kwa moja wanateuliwa na Rais! Kwanini mtendaji wa Shirika la Bima ateuliwa na Rais? Kwanini mtendaji wa Shirika la Tanesco ateuliwe na Rais? Vipi mtendaji wa ATCL ateuliwe na Rais na wakati huo huo Rais anatakiwa ateue Mkuu wa Usalama wa Taifa n.k ?
Kama wabunge wetu wangeamua kufikiri kidogo wangeondoa mzigo huu wa uteuzi kwenye makampuni yafanyayo biashara ili wakurugenzi wake waingie kwa kushindanishwa (kuomba) na kuteuliwa na Bodi ya Wakurugenzi ambayo nayo iundwe na wadau siyo na wanasiasa.
Matokeo yake Mtawala anaamua Kusettle; yaani kuteua mtu yule ambaye aidha ni fisadi "mdebe mdebe" (mdogo) au fisadi asiyejulikana sana. Na hili linaweza kuelezea kwanini hadi leohii Rais Kikwete anapata shida ya kuachia watu wastaafu na kuteu watendaji wengine.
Hebu angalia taarifa hii kutoka katoto ka "nzi"...

Mkuu Mwanakijiji;
...
Ndege moja ya Aribus ambayo sisis tulikuwa tunakodi(iliyotimika) bei yake ikiwa mpya ni dola million 50 ba inachukua muda wa miaka mitatu mpaka unakabidhiwa ndege yao;Jiulize serikali ilikuwa inakodi kwa bei gani?mara mbili zaidi ya bei ya kununulia
tatu,Mpaka leo mashirika haya pamoja na interview kufanyika na faili kupelekwa kwa mkuu ila hajateua watendaji wa mashirika haya;sijui muungwana anafanya kazi gani
1.Mkurugenzi wa Consolidated Holdings Corporation(miaka miwili)
2.Mkurugenzi wa National Insurance Corporation(NIC)
3.Mkurugenzi wa TANESCO
4.Mkurugenzi wa TTCL
5.Mkurugenzi wa ATCL
Hao wote nafasi zao ziko acted kwa muda mrefu na hakuna maamuzi yoyote yanayofanyika;watu hawahoji kwanini inachukua muda mrefu ila hii yote ni kwasasabu tunapenda mapmbo mepesi mepesi
Shirika la NBC tunatakiwa kuteua Mwenyekiti wa Bodi ila mpaka sasa yule Mpungwe anakaimu ;matokeo yake kunakuwa na maamuzi mabovu sana katika kufanikisha
Hapo bado kuna mambo mengi yanakwama tu ukiangalia hata Luhanjo muda wake umeisha ila naye sijui nani kamuongezea muda wa kukaa pale ila anatakiwa kustaafu;
suala la mambo mepesi mepesi limenikumbusha haya