Hiyo siyo nadharia yako ila mwl nyerere..alisema hayo kwenye maongezi yake...kama amekuwa yahaya na yeye sijui!
Hata ikiwa hivyo wewe mtanganyika inakuhusu nini? ombeni na nyinyi kusitokee mwanza zone and kilimanjaro zone damn!
Kidole kimoja hakivunji chawa.Umoja ni Nguvu na Utengano ni dhaifu. Wazanzibari wanashangilia kufa kwa muungano lakini hawajui baada ya hilo fungate ni mateso. Yani hawa jamaa wananifananisha na wakati wa Musa na Waisraeli kule jangwani. Kwamba bora usultani kuliko kwenda nchi ya maziwa na asali. Tumaini naona unajiandaa kurudi kwenye zama za makuli na kufuta dhana ya Shafi Adamu Shari kwenye kitabu chake cha KULI.
Muungano ulipigiwa kura na Bunge la Tanganyika na Baraza la Wawakilishi wa Zanzibar. Pande zote mbili zilijadili (najua wengi hawajui historia hiyo). Nyerere alileta hoja Bungeni na kuwaelewa wabunge wetu kwanini mataifa mawili haya yataungana. Wabunge wakaridhia na ni baada ya hapo ndio Muungano ukafanyika.
Hivyo ni Muungano halali na ni jukumu la kila Mtanzania kuulinda. Katika kuulinda huko ni jukumu letu kuwapinga pasipo kuwapepesea macho wale wote wanaotaka Muungano uvunjike kwa sababu hawataki kufanya maamuzi magumu au kuzungumzia mambo yanayoleta utata katika Muungano. Wapo watu wa bara ambao kwa kawaida hatupendi sana migongano, tunapenda vitu lelemama kiasi kwamba tumekuwa kama tumedekezwa hivi!
Serikali ikisema "hawa wanaleta mgawanyiko katika jamii" basi kama watoto tunakubali na kuwakimbia wenzetu kwa sababu "serikali imesema"; Serikali ikija na kusema wapinzani wanataka kuligawa taifa basi tunakimbia kama watoto huku tumenyanyua mikono tubebwe huku tunaonesha vidole "yule anataka kuligawa taifa mama!".
Hatutaki kugonganisha mawazo na matokeo yake hata kwenye vikao vya kazi tumekuwa hivi hivi tu. Mtu anayebisha sana anaonekana "mbishi tu"; mtu anayetaka maelezo zaidi anaonekana kama anataka kujipendekeza. Tunataka mambo ya upole upole na taratibu.
Ndio maana utaona watu wengi wa bara wanaotaka Muungano uvunjike wanafanya hivyo kwa sababu utaondoa "migongano" na kubishana bishana. Tunataka "utulivu, amani, na mshikamano" wa uongo. Ndio maana watu wa bara wanaona kama Zanzibar ni wakorofi kweli kumbe kule Zanzibar wao wameshazoea zile siasa za kujibizana, kubishana na serikali, na kutunishiana misuli.
Ninaamini athari kubwa sana ya ukoloni katika psyche ya watu wa bara ni unchecked docility ya ajabu sana. Na watawala wetu wanatumia sana hii kuwatuliza watu wa bara.
Muungano tutaulinda na tutaudumisha na kuuboresha. Tutawapinga watu wa bara wanaotaka kuuvunja kwa sababu hawataki kubishana na kulumbana na kugongana kifikra na tutawapinga watu wa visiwani wanaotaka kuuvunja kwa sababu wanaogopa kukubali ukweli wa umuhimu wa muungano.
Tutawaunga mkono wale wote majasiri ambao watasimama na kutoa hoja za jinsi ya kuudumisha, watakaokuwa tayari kutoa mapendekezo ya jinsi ya kuuboresha na wale watakaonesha uongozi wa kuboresha muungano wetu kwa uwazi na ukweli na ujasiri usio kikomo.
Natumaini hatutawafumbia macho wala kuwaonea haya kuwashughulikia pasipo kuwabembeleza watu wanaofanya njama za kuuvunja muungano wetu.
Muungano daima!
JK hana power ya kuvunja Muungano....
of course hana; lakini ana uwezo wa kuwazuia wengine wasivunje?
Sometimes men are masters of their own fate! Nafikiri Zenj wameshafanya due diligence ya kutosha ya consequences za kuuvunja muungano.Si ndio wanafuata wanatumia kikao cha wawakilishi kilicho halali kikatiba kuomba kibadilishwe ili kiwafae watu na mahitaji yao...
tatizo kwanini watu wa bara wanataka kuwahadaa wazenj wasitumie fursa hiyo kubadilisha katiba?
Pamoja na makosa kadhaa ndani ya muungano, pia muungano huu umeyasitiri mengi. Ngoja tuone nini kitajiri baada ya kujivua nguo hii ya muungano.
Lakini wakati huo huo, uongozi imara hauonekani wakati wa kushangilia stars ikicheza na Msumbiji au Ghana...unaonekana katika umahili wa kutatua matatizo yaliyopo mezani wakati huo. All the best kwenu leaders!!!
of course hana; lakini ana uwezo wa kuwazuia wengine wasivunje?
karibu CCJ - Chama cha Jamii
Wewe unaunga muungano kwasababu gani? au kwa vile kasema nyerere?
@Kuchanganya Mchanga
Mchanga uliochanganywa ni wa Tanganyika tuu...naye ni Nyerere pekee ndie aliechanganya mchanga huo wa mikoa tofauti kutoka Bara.
Ukitizama hii picha, utaona Karume hajagusa mchanganya huo..kwasababu si mchanga wa visiwani.
@Mwanakijiji
Ukitizama nyaraka ya muungano ni saini za Nyerere tuu na Msekwa hakuna saini ya Baraza au bunge la Zanzibar.Sasa huu msimamo wako kuwa Zanzibar walipitisha na kukubali muungano ulitokea wapi?Lete ushahidi kama huna basi unazungumza pumba tupu...
Nyaraka ya muungano iliyopo kwenye public http://www.scribd.com/full/24823426?access_key=key-1dlp0tnzt4n91utuby5c
Duuh hii kali, na kiwanja chenyewe ni hicho kisiwa cha zbar!Inachanganya kidogo kwamba Karume anatia saini lakini haionekani kwenye mkataba...naona picha hii imepigwa wakiuziana kiwanja sio muungano.
Kama ingelikuwa muungano basi hiyo saini ya Karume ni lazima ionekane kwenye mkataba.
@Mwanakijiji
Ukitizama nyaraka ya muungano ni saini za Nyerere tuu na Msekwa hakuna saini ya Baraza au bunge la Zanzibar.Sasa huu msimamo wako kuwa Zanzibar walipitisha na kukubali muungano ulitokea wapi?Lete ushahidi kama huna basi unazungumza pumba tupu...
Nyaraka ya muungano iliyopo kwenye public http://www.scribd.com/full/24823426?access_key=key-1dlp0tnzt4n91utuby5c