Kikwete: Kiongozi bora au mbabaishaji? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete: Kiongozi bora au mbabaishaji?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kidudu Mtu, Dec 10, 2009.

 1. Kidudu Mtu

  Kidudu Mtu Member

  #1
  Dec 10, 2009
  Joined: Nov 7, 2009
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kumekuwa na kauli tata kutoka kwa viongozi mbalimbali kuhusiana na uongozi wa Rais Kikwete. Kuna wanaomsifu na kuna wanaomkosoa.

  Tukiweka ushabiki wa kisiasa pembeni na kuweka uzalendo mbele, je Rais Kikwete ni kiongozi bora au mbabaishaji? Jadili ukiweka bayana yanayokufanya useme hivyo.
   
 2. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #2
  Dec 10, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Kiongozi bora ni yule anayetimiza yote anayoahidi, ni shupavu na asimwogopa wala kumwonea mtu, ni mwadilifu, anayeona mbali, nk! Tukija kwa Rais Kikwete: Alitoa ahadi nyingi ambazo kama ametekeleza sijui ni zipi! Amekuwa mwoga wa kuwakemea watu wanaojihusisha na ufisadi, tena wengine bado wana nyadhifa nzito kwenye chama ambacho yeye ni Mwenyekiti! Katika uongozi wake nchi imekumbwa na migawanyiko ambayo haijawahi kutokea: Kijiografia-Zanzibar ni nchi au la? Kidini, mambo ya Kadhi, OIC, Mahakama za Kadhi, Waraka, Mwongozo, Ilani, nk! Kiuchumi: Walio nacho na wasio nacho: siku hizi kama mfuko wako hausomeki sahau kabisa fomu ya kugombea uongozi, maisha bora kwa kila mtz ni ndoto under JK!
   
 3. T

  Tongue blister JF-Expert Member

  #3
  Dec 10, 2009
  Joined: Jun 19, 2009
  Messages: 361
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sasa Kidudu Mtu kwanini tusianzie kwako Mkuu wangu ? Wewe maoni yako yana sema je ?
   
 4. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #4
  Dec 10, 2009
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Ni bola kiongozi
   
 5. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #5
  Dec 10, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  kikwete sio kiongozi bora. Watu walimchagua si kwa uongozi bora bali ni kwa jinsi alivyo mkarimu.mtu akiwa mkarimu haimaanishi utakuwa kiongozi mzuri na ndio kosa la watanzania katika kumchagua kikwete.kinachofanyika sasa ni weakness zake zinaonekana.na yeye kwa vile yeye hana sifa za kuwa kiongozi ndio maana alivyopata uraisi akaendelea kuwakumbatia marafiki zake bila kuja huwezo wao wa kutumikia taifa au maovu yao yaliopita.


  kikwete kuchaguliwa kuwa kiongozi inanikumbusha shule ya msingi watu walikuwa wanapenda mtu mpole hawe monita darasani manake wanajua tatizo au watu wakipiga makelele akija kuulizwa majina waliofanya fujo yako wapi hana kwa vile anaogopa.
   
 6. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #6
  Dec 10, 2009
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,068
  Likes Received: 3,999
  Trophy Points: 280
  nathani jibu unalo anaonewa wivu na nchi yake!
   
 7. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #7
  Dec 10, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Kumuita Kikwete mbabaishaji ni kumkweza.

  Mana ili mtu kuwa mbabaishaji inabidi awe anaelewa angalau the basics, lakini hawezi kufanya mambo vizuri, anababaisha babaisha na kubahatisha bahatisha, hii ni bora kuliko Kikwete.

  Kikwete ni chini ya mbabaishaji, huyu anaitwa "bora liende", yaani yeye mwenyewe hajui kazi (fine, hata Mwinyi hakujua kazi, lakini alichagua watu wakamfanyia kazi to an extent)

  Sasa huyu Kikwete yeye kazi hajui, hata kuchagua watu watakaomfanyia kazi nako hajui, unaenda kuchagua PM Pinda, sijui Sophia Simba, Makamba, Mkullo aibu aibu aibu.

  Kuna a famous physicist alikuwa anaitwa Wolfgang Pauli, aliletewa arguments za physicist mwingine, akaambiwa aseme kama ziko right or wrong, Pauli akasema "This is not even wrong" yaani arguments na constructs ziko so off base hata kuziita wrong itakuwa ni kuzi elevate.

  Ndiyo Kikwete huyo, he is not even wrong, hata si mbabaishaji.

  Kikwete ni bora liende, kama dege liko katika autopilot, halina pilot, rais hatuna.

  Autopilot dege likiwa hewani unaweza hata usijue.

  Tatizo huwezi kutua na autopilot, inabidi uwe na pilot.

  I dread to think of how Kikwete will handle a crisis that require his immediate attention and calculations, hapo ndipo tutajua hatuna rais.
   
 8. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #8
  Dec 10, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Jibaba,

  Unataka kusema kuna "Kiongozi bora" na "Bora kiongozi" ?
   
 9. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #9
  Dec 10, 2009
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Siyo kiongozi bali ni MTAWALA
   
 10. Z

  Zungu Pule JF-Expert Member

  #10
  Dec 10, 2009
  Joined: Mar 7, 2008
  Messages: 2,139
  Likes Received: 682
  Trophy Points: 280
  He is useless!
   
 11. T

  Tongue blister JF-Expert Member

  #11
  Dec 11, 2009
  Joined: Jun 19, 2009
  Messages: 361
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa mtazamo wangu kuna vitu ambavyo naweza kuvitazama kabla ya kutoa maamuzi ya ubora wake au la !!!


  1) Rais wetu amekuwa na dream vision ambazo naweza kusema huwa ni za kuwalaghai watanzania.
  2) Rais Bora anatakiwa ku
  inspire watu ili wajiunge kwenye chama chake.
  3) Rais bora ni yule ambaye yupo clear and directly face the strengths pamoja na weaknesses, Unaliona je kwa Rais wetu hili ? Je anatingishika kweli ?
  4) Rais bora ni yule ambaye yupo bottom-line oriented and extraordinarily committed katika matokeo.
  5) Rais bora mara nyingi huwa ana achieve vitu ambavyo amevi set out to kuvifanya kabla ya ku launching new initiatives.
  6) Rais bora lazima awe motiv by persuasion rather than intimidation.
  7) Rais bora ni lazima aonyeshe high degrees of emotional intelligence, and thrive on finesse na wakati huo huo awe likeability.
  Rais bora lazima awe Decisive:" wanasema "In any moment of decision, the best thing you can do is the right thing, the next best thing is the wrong thing, na katika hayo the worst thing you can do is nothing."
  9) Rais bora ni yule ambaye yupo direct and straightforward katika shughuli zake . Na huwa ana set clear performance expectations and hold people accountable.
  10) Rais bora ni yule ambaye yupo open and dedicated to lifelong learning. Hujaribu kutafuta taarifa about their performance through direct conversations pamoja na objective tools

  Kutokana na Maoni yangu hayo sijaona hata kimoja ambacho naweza kupa 50pts. Na kama atapata vi points itakuwa ni wale wenye kupenda ushabiki..!!

  KWAHIYO MIMI MAONI YANGU RAIS KIKWETE SIO RAIS BORA BALI NI BORA RAIS !!!!

  Mungu ibariki Tanzania !!!

   
 12. Serendipity

  Serendipity JF-Expert Member

  #12
  Dec 11, 2009
  Joined: Jan 24, 2009
  Messages: 475
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Kuna aina nne au tano za viongozi!
  Yeye ni leizer fair!
   
 13. T

  Tongue blister JF-Expert Member

  #13
  Dec 11, 2009
  Joined: Jun 19, 2009
  Messages: 361
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Zungu unanifanya ni cheke sana !!! Umegundua hilo kumbe !!!
   
Loading...