Kikwete hajamjibu Lowassa - S. Kubenea | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete hajamjibu Lowassa - S. Kubenea

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Luteni, Jul 8, 2011.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Jul 8, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  RAIS Jakaya Kikwete, ama ameshindwa au amekataa kujibu tuhuma za swahiba wake, kwamba serikali yake inaumwa ugonjwa wa kutofanya maamuzi magumu, MwanaHALISI limeelezwa.

  Siku 13 tangu tuhuma hizo zirushwe bungeni, Kikwete amekaa kimya. Hata waziri mkuu, Mizengo Pinda aliyedaiwa kujibu tuhuma hizo wakati akijibu hoja za wabunge kuhusu makadirio ya wizara yake, "aliishia kudodosa tu," wachambuzi wa siasa wanasema.

  Edward Lowassa, waziri mkuu aliyejiuzulu kwa kashifa ya Richmond, alimshukia Kikwete na serikali yake wiki mbili zilizopita na kudai serikali ya swahiba wake ina ugonjwa wa kutotoa maamuzi magumu.

  Lowassa alikuwa akichangia hotuba ya bajeti ya ofisi ya waziri mkuu kwa mwaka wa fedha 2011/2012.

  Lowassa alisema, "…hivi sasa kuna ugonjwa umezuka nchini wa viongozi wa serikali kushindwa kutoa maamuzi magumu kwa maslahi ya taifa." Alisema "Bora kuhukumiwa kwa kutoa maamuzi magumu, kuliko kuogopa kuyatoa."

  Wachambuzi wa mambo wanasema hatua ya Kikwete kushindwa kumjibu Lowassa inaweza kuwa imetokana na viongozi hao wawili kuishi kama "watu walionyonya ziwa moja," jambo ambalo limewafanya kufahamiana vema na kulindana "kwa gharama yoyote ile."

  Uchunguzi umeonyesha kuwa wengi waliomsikia Lowassa, wiki mbili zilizopita, akihutubia bunge kwa mara ya kwanza tangu alipojiuzulu wadhifa wa waziri mkuu, Februari 2008, walitarajia Rais Kikwete angetia neno hima. Hajafanya hivyo.

  Lowassa ndiye alikuwa mwenyekiti wa mtandao uliofanya kazi kubwa ya kumuingiza Kikwete ikulu mwaka 2005. Pamoja na mambo mengine, kazi kubwa ya genge hilo ilikuwa kumlinda, kumkinga na kumg'arisha Kikwete; huku likichafua kila aliyeonekana mgombea tishio.

  "Lowassa anajua mengi. Wamefanya mengi pamoja. Inawezekana kabisa ndiyo sababu Kikwete ameshidwa kujibu," ameeleza mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya CCM.

  Amesema, "Lowassa anafahamu nani alichangia kampeni za Jakaya (Rais Kikwete) mwaka 2005. Anafahamu ametoa kiasi gani na amekabidhiwa nani. Anafahamu hata mapato ya hao waliochangia, kwamba wengine hayakulingana na fedha walizotoa. Hivyo hatua yeyote ya kumjibu ingesababisha mengi ikiwamo kuumbuana."

  Alipoulizwa iwapo Lowassa wakati akitoa kauli hiyo alilenga kueleza hayo; hasa ukitilia maanani kwamba ndani ya chama chake kuna vuguvugu la kumtaka kuondoka katika uongozi, kwanza alicheka na kisha akasema, "Inawezekana. Wakati mwingine siasa ni kuviziana."

  Kwa takribani miaka mitano sasa, Rais Kikwete amekuwa akilaumiwa na viongozi wastaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na serikali, viongozi wa vyama vya upinzani, asasi za kijamii na watu binafsi, kwa kutochukua hatua mwafaka pale zinapohitajika.

  Tuhuma za Lowassa ziliibua hisia mbalimbali huku wengine wakisema amelipuka kwa kuwa ameona wanataka "kumfukuza katika chama." Lowassa, Rostam Aziz na Andrew Chenge walitajwa na chama chao, miezi miwili iliyopita, kuwa "mafisadi wanaochafua chama" na wanaostahili kung'olewa uongozini.

  Alikuwa katibu mwenezi wa CCM, Nape Nnauye aliyesema, siku tatu baada ya "mpasuko" wa Lowassa kwamba, serikali imechukua maamuzi magumu na kwamba wananchi wasubiri maamuzi yatakayochukuliwa dhidi ya walioambiwa kujiondoa kwenye uongozi lakini bado hawajafanya hivyo.

  Kauli hiyo ilikuwa ikilenga moja kwa moja kwa Lowassa, Rostam na Chenge, ambao chama chao kimesema kimewapa siku 120 wawe "wamejifukuza."

  Ni tafsiri hii ya viongozi wa juu CCM ambayo inadaiwa kufanya Lowassa kuchukua hatua ya kujihami kabla hajachukuliwa hatua.

  Taarifa kutoka Dodoma zinasema Lowassa amekwenda ofisi ya kuweka rekodi za nyaraka za bunge (Hansard), kuchukua nukuu sahihi ya aliyosema bungeni na kumpelekea katibu mkuu wa CCM, Wilson Mukama.

  Mtoa taarifa anamnukuu Lowassa akimwambia Mukama kuwa asitafsiriwe au hata kueleweka vibaya; "mambo niliyosema ni haya hapa," huku akimkabidhi nakala ya hansard. Juhudi za kumpata Lowassa kuthibitisha haya zilikwama kutokana na simu yake kuita bila kupokelewa.

  Tangu alipotoa kauli ya kutuhumu bungeni, Lowassa amekuwa akifikiriwa kuwa sasa ameamua "kupambana na rafiki yake Kikwete ambaye aliwahi kusema ‘hatukukutana njiani tu,'" ameeleza mtoa taarifa.

  "Ingekuwa hivyo, hata ikulu pangekuwa hapatoshi. Wanaofahamiana sana wangekuwa wameumbuana sana na kuachana uchi. Kwa manufaa ya nani, lakini?" ameuliza mjumbe huyo wa CC.

  Miongoni mwa tuhuma ambazo Rais Kikwete amebebeshwa, ni pamoja na kushindwa kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wa wizi wa fedha za umma kupitia Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Taifa (BoT).

  Imekuwa ikidaiwa kuwa sehemu kubwa ya mamilioni yaliyochotwa BoT, ilitumika kuwaingiza madarakani Kikwete na wenzake. CCM imeshindwa kujinasua kwenye tuhuma hizi zinazoibuka mara kwa mara
  .
  Kwa mfano, mtoa taarifa wa gazeti hili amesema karibu kiasi cha dola za Marekani 15 milioni, zilizoibwa kutoka BoT kwa jina la Kagoda Agriculture Limited, zilitumika katika kampeni za Kikwete.

  Anasema Rostam na Lowassa wanafahamu hilo na kwamba Kikwete analijua pia. "Hatua yoyote ya kuingia mzozo, hakika itawalipua wote, hata kama taarifa hizi zimetajwa mara nyingi."

  Rostam ndiye amekuwa akitajwa kuhusika katika mpango wa kufanikisha wizi wa Kagoda, jambo ambalo wachambuzi wanasema "limemfanya Kikwete kushindwa kufanya maamuzi magumu ya kuwafikisha watuhumiwa mahakamani."

  Ukimya wa Rais Kikwete umemhenyesha waziri mkuu Mizengo Pinda. Akifunga mjadala wa bajeti juu ya ofisi yake, Pinda alisema Bungeni wiki iliyopita kuwa serikali imefanya maamuzi mengi magumu; likiwamo lile la kuvunja baraza la mawaziri.

  Kauli ta Pinda ndiyo ilichochea hatua ya Lowassa ya kutafuta hansard na kuipeleka kwa Mukama, ikisindikizwa na barua na maelezo kuwa "nisije kusingiziwa uwongo."

  Taarifa zinasema katika barua yake kwa Mukama, Lowassa ameambatanisha ushahidi, ikiwamo hansard ya Bunge inayoonyesha alichokisema wakati akichangia bajeti ya ofisi ya waziri mkuu.

  Lowassa anasema katika barua yake, "Nilichosema kuhusu maamuzi magumu, si kulenga mambo ya kisiasa. Nimelenga ujenzi wa reli na kutafuta fedha kwa kutumia dhamana za ndani," kimeeleza chanzo cha gazeti hili ndani ya CCM.

  Wiki tatu zilizopita, Spika Anna Makinda alijipa fursa ya kumsemea waziri mkuu Pinda wakati wa kikao cha maswali na majibu. Alimzuia kujibu maswali akidai hoja zake zilikuwa mahakamani.

  Naye Pinda, wiki iliyopita, alimsemea Rais Kikwete katika juhudi zake za "kumjibu" Lowassa aliyedai serikali inashindwa kufanya maamuzi magumu.

  Mtoa taarifa mwingine ambaye yuko karibu na Kikwete anasema, mbali na madai kwamba Kikwete anashindwa kuchukua maamuzi magumu ya kupeleka watuhumiwa mahakamani kwa sababu ya wizi wa fedha za EPA, simu yake ya mkononi ni kikwazo kingine cha kufanikisha majukumu yake.

  Anasema rais amekuwa "bize" kujibu ujumbe mfupi wa simu yake ya mkononi, jambo ambalo limesababishwa na uamuzi wake wa kugawa namba yake ya simu kila anakopita.

  Kiongozi huyo wa nchi, mtoa taarifa anasema, ana simu tatu za mkononi ambazo anatembea nazo kila anakopita; jambo linalomfanya kupokea umbea kutoka kwa wasaidizi na maswahiba wake.

  "Hata Mkapa (rais mstaafu Benjamin Mkapa) alikuwa na simu ya mkononi. Lakini simu ya Mkapa ilikuwa ya kupiga tu. Ilikuwa huwezi kumpata Mkapa kwenye simu yake ya mkononi, hadi yeye akupigie," anaeleza kigogo mmoja wa ikulu ambaye alikuwa karibu na Mkapa.

  Anasema, "Hata mawaziri wake walikuwa hawawezi kuongea naye kupitia simu yake ya mkononi. Simu ya Mkapa ilikuwa kwa mawasiliano ya watu wasiozidi sita wakiwamo watoto wake wawili na mkewe."

  Anasema hadi sasa, Mkapa anamiliki simu ya mkononi, lakini huwezi kumpata hadi yeye akupigie. Ile ni simu ya yeye kukupigia, si wewe kumpigia. Ni tofauti na Kikwete. Huyu bwana amegawa namba yake ya simu kwa watu ambao wengine wanaitumia kumpelekea umbeya," anaeleza.

  Anasema simu ya Rais Kikwete inapokea ujumbe wa kila mmoja na kuna wakati yeye hujibu ujumbe aliotumiwa usiku wa manane. Anahoji, "Sasa katika mazingira hayo, rais anapata wapi muda wa kupumzika na kusoma nyaraka?"

  Gazeti hili liliwahi kuchapisha ujumbe wa simu uliodaiwa kutoka kwa Rais Kikwete kwenda kwa aliyekuwa mbunge wa Viti Maalum, Amina Chifupa aliyekuwa ameomba ushauri wa kisiasa kwa rais Kikwete.

  Amina aliusambaza ujumbe uliotoka kwa rais kwa watu mbalimbali akiwamo Zitto Kabwe na Emmanuel Nchimbi.
   
 2. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #2
  Jul 8, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mimi nafikiri kujibu kila kitu kutamchosha Rais. Huyu mtoa tuhuma hataishia hapa, kwani ndiyo kwanza ameanza na atakuwa akitoa tuhumua kila wakati ili kurejesha nuru yake ya kisiasa. Kumkalia kimya nayo ni namna nzuri ya kumpuuza na kupuuza madai yake.
   
 3. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #3
  Jul 8, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Namna nynigne ni kumjibu kirejareja kama mzee Sitta alivyofanya.
   
 4. s

  saggy Senior Member

  #4
  Jul 8, 2011
  Joined: Nov 12, 2008
  Messages: 153
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kubenea ndugu yangu na mwandishi maarufu wa habari na unayeheshimika na Jamii ya Watanzania na hata mimi mwenyewe nimejifunza mengi kutoka katika Makala zako,nakupongeza kwa Kugundua kwamba EL anaweza kusaidia kuongeza Manunuzi ya GAZETI lenu ndio maana kila siku hamchoki kuandika Habai zake kana kwamba hakuna watu wengine,Hongera sanaaaa Kubenea kwa Ubunifu mkubwa wa Kibishara,EL ni jina kubwa la Kuuzia Gazeti lako!
   
 5. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #5
  Jul 8, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Raisi Kikwete hana historia ya kujibu tuhuma zozote. Mara nyingi Kikwete hujibiwa na wa chini wake kuanzia kwenye chama hadi press secretary wake, mawaziri na waziri mkuu. Ni nadra sana Kikwete kutoa ufafanuzi wa jambo tata na hili linatokana na ukweli kwamba Kikwete anaogopa kwa sasa kutoa majibu yasiyo popular. Mnaotegemea JK atajibu tuhuma fuatilia historia ya utawala wake na ni mara ngapi amekua proactive katika kujibu important issues.
   
 6. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #6
  Jul 8, 2011
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,316
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Atatoa majibu yatakayoshtua wengi baada ya kikao cha NEC ya magamba!
   
 7. Mvua Ya Kiangaz

  Mvua Ya Kiangaz JF-Expert Member

  #7
  Jul 8, 2011
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 305
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 33
  .......Amjibu ili iweje???............................Kubenea njaa tu,anakwenda kwenye mlo tu........siyo kila kitu kinajibiwa tu.........roma locuta,causa finita:
   
 8. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #8
  Jul 8, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Na huo ndiyo wakati muafaka. Wakati huo jamaa akiwa chaliii!
   
 9. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #9
  Jul 8, 2011
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  ssa atajibu kitu gan wakati ameshikwa na butwaa anajua huyu ni mchafu mwenzie sasa anapoanza kuhoji anashtushwa kuwa hayumkini mwenzi wake kaanza kutakata!
   
 10. M

  Mnyakatari JF-Expert Member

  #10
  Jul 9, 2011
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 1,557
  Likes Received: 488
  Trophy Points: 180
  Huwa sipendi pale mwanahalisi wanapoandika 'ameeleza mjumbe wa kamati kuu 'CC' ya ccm'.Kwanini wasitaje jina lake?Hii husababisha nione kuwa ni mawazo binafsi ya mwandishi.Mtazamo tu.Not necessary true!
   
Loading...