Kikwete bado anajifunza kuongoza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete bado anajifunza kuongoza

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Inkognito, Mar 28, 2011.

 1. I

  Inkognito Member

  #1
  Mar 28, 2011
  Joined: Feb 13, 2011
  Messages: 73
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Kati ya mambo ambayo yalivuta hisia za wengi katika mwaka 2009 ni kitendo cha ofisi ya kikwete kutangaza kuwa Kikwete ataongea na wananchi moja kwa moja kupitia vyombo vyetu vya habari tofauti na ule utaratibu wa kurekodiwa kwa hotuba zake na kurushwa hewani kupitia vyombo vya habari.

  Wengi walikuwa na shauku ya kutaka kusikia na kuona utaratibu huo mpya utakaomwezesha kikwete kuwasiliana na wananchi moja kwa moja, naomba kwanza tujikumbushe kabla sijaenda katika hoja za msingi kwa kusoma taarifa ifuatayo;-
  DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
  UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
  Telephone: 255-22-2114512, 2116898
  E-mail: press@ikulu.go.tz
  Fax: 255-22-2113425
  PRESIDENTÂ’S OFFICE,
  THE STATE HOUSE,
  P.O. BOX 9120,
  DAR ES SALAAM.
  Tanzania.


  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI​
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, kesho, Jumatano, Septemba 9, 2009, atazungumza moja kwa moja na wananchi kupitia Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) na vyombo vingine vya utangazaji nchini kuanzia saa mbili na nusu usiku. Mbali na TBC, televisheni nyingine za ITV, TVZ, Mlimani TV, Tumaini TV na Channel Ten zinatarajia kuonyesha mazungumzo hayo.

  Rais atatumia aina mpya ya kuwasiliana na wananchi kwa kusikiliza hoja zao, kwa kujibu maswali yao, kusikiliza ushauri wao na kupata maoni juu ya mambo yanayohusu mustakabali wa nchi yetu, Serikali yetu na maendeleo yetu.
  Aidha, Rais atasikiliza matarajio ya wananchi katika jitihada zao za kuboresha maisha yao kwa kujiletea maendeleo.

  Mazungumzo hayo yatakayochukua muda wa dakika 90 kuanzia saa mbili unusu usiku (saa 2:30 usiku) hadi saa nne kamili usiku.

  Aidha mazungumzo hayo yatatangazwa kwenye redio za TBC-Taifa, Sauti ya Tanzania, Zanzibar, Radio Mlimani, Radio Clouds, Radio Tumaini, na Radio Uhuru.
  Maswali, maoni, hoja, ushauri utapokelewa moja kwa moja na TBC kupitia simu nambari +255-22-2772448, +255-22-2772452 na +255-22-2772454.

  Aidha, maswali, maoni, hoja ama ushauri unaweza kutumwa moja kwa moja TBC kupitia ujumbe mfupi wa SMS kwenye nambari 0788-500019, 0714-591589 na 0764-807683 ama kupitia kwenye barua pepe swalikwarais@yahoo.com kuanzia leo.
  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais inawashauri wananchi kutumia kikamilifu nafasi hiyo ya kuwasiliana moja kwa moja na Rais wao.
  Imetolewa na:

  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
  Ikulu,
  DAR ES SALAAM .
  08 Septemba, 2009

  Baada ya kusoma taarifa hiyo nimegundua mambo yafuatayo:
  1. Kikwete na washauri wake walitaka kutushawishi kuwa njia pekee ya kuwavuta watanzania ni kupitia utaratibu huo mpya wsa kuongea na kusikika moja kwa moja kwenye vyombo vya habari
  2. Kwamba Kikwete na washauri wake walitaka kuwaaminisha watanzania walio wengi kuwa yuko karibu zaidi na watanzania katika kuwasikiliza na kubadilishana mawazo kuliko utaratibu wa mwanzo uliozoeleka kwa wengi
  Pamoja na utaratibu huo mpya uliobuniwa na washauri wake, utaratibu huo ulikuwa wa kukurupuka kutokana na sababu zifutazo ambazo pamoja nyingine nyingine utakazoweza kuziongezea nazieleza kwa kifupi tu kama ifuatavyo;
  1. Utaratibu huo sio endelevu, ulikuwa wa kitambo na ndio maana tangu kuanzishwa kwa utaratibu huo na kufanyika mara moja tu mpaka leo haujafanyika tena
  2. Vyanzo kutoka ikulu vinabainisha kuwa hakukuwa na utaratibu wowote uliopangwa kuonesha ni kwa muda gani rais atakuwa anaongea kwa kutumia njia hiyo mpya
  3. Ikulu inabainisha kuwa washauri wake waligundua kuwa njia ya kuongea moja kwa moja ingeweza kushusha kiwango na mvuto wa Rais kwa kuwa njia hiyo ingeibua maswali na changamoto ambazo kwa uwezo wa JK ingekuwa vigumu kuzikabili
  4. Ikulu iligundua kuwa njia hiyo mpya haikuwa na maandalizi ya kutosha hivyo kufanya hata siku ile alipoongea moja kwa moja wafanye utaratibu wa kuwapanga watu kutoka ofisi yake kupiga simu, kutuma email na kuuliza maswali
  5. Njia hiyo mpya ingezidi kumpa Rais JK wakati mgumu wa kukariri maswali na majibu jambo ambalo lingekuwa ni kazi kubwa kwa Rais kama Kikwete ambaye muda mwingi anakuwa safarini kupata muda wa kujiandaa
  Kwa kifupi tu, hii ni moja ya mambo ambayo bado yanathibitisha kauli ya JK mwenye kuwa katika kipindi cha miaka mitano ya mwanzo alikuwa anajifunza kuongoza, viongozi wengi aina ya kikwete bado wana dhana ya kuongoza mambo ya nchi kama wanavyoongoza familia zao.
  Kubuniwa na kuanzishwa kwa utaratibu huo mpya wa kuongea na watanzania ni mfano mmoja tu wa namna Kikwete anavyojifunza kuongoza watanzania

  Naomba kuwasilisha
   
Loading...