Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,890
- 6,896
RAIS Jakaya Kikwete, anaelezwa kukwamisha vita dhidi ya ufisadi ndani na nje ya chama chake, Chama cha Mapinduzi (CCM), baada ya kuamua kumteua mtuhumiwa wa kashfa ya Richomond, Bashir Mrindoko, kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji. Tayari hatua hiyo imeanza kumgharimu kisiasa aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza kashfa hiyo, Dk. Harrisson Mwakyembe, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ujenzi.
Duru za siasa kutoka ndani ya CCM, zinasema kuwa uteuzi wa Mrindoko umewashtua wengi na kuibua hoja endapo Rais Kikwete ana dhamira ya dhati kupambana na ufisadi nchini. Ripoti ya kamati ya Mwakyembe ilitaka Mrindoko na wenzake wawajibishwe kwa ufisadi waliohusishwa nao katika zabuni ya Richmond, lakini badala ya kumuwajibisha, juzi Rais Kikwete amempa cheo cha kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji. Unaweza kujiuliza, kweli Rais ana dhamira ya kupambana na ufisadi? alihoji kada mmoja wa CCM.
Kada mmoja ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe, alihoji uhalali wa CCM kutaka kuwatimua kwenye chama wabunge wake Edward Lowassa, Rostam Aziz na Andrew Chenge kwa tuhuma za ufisadi wakati Rais, ambaye pia ni mwenyekiti wa chama hicho taifa, anamfumbia macho Mrindoko. Mimi simtetei Lowassa na wenzake, lakini katika hali ya kawaida, kama ndani ya chama Rais anaongoza vikao kuwafukuza Mapacha Watatu kwa tuhuma za ufisadi, kwa nini mtuhumiwa mwingine wa ufisadi (Mrindoko) aliyependekezwa awajibishwe anapewa cheo kingine? alihoji kada huyo. Mtuhumiwa wa ufisadi aliyepaswa kuchukuliwa hatua za kinidhamu na za kisheria leo amepewa cheo kipya cha kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji. Ni rahisi kwa ngamia kuingia kwenye tundu la sindano kuliko CCM kuachana na mafisadi, alisema.
Kada huyo ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), alimlaumu Rais Kikwete kuwa anavuruga vita dhidi ya ufisadi kwa kushindwa kuchukua maamuzi magumu ya kuwatosa watuhumiwa wa ufisadi. Alisema uteuzi huo unazidi kulipa taifa ushahidi jinsi Rais Kikwete na chama chake wanavyoendelea kukumbatia ufisadi licha ya kujidai kujivua gamba hivi karibuni.
Katika mapendekezo yake, Kamati ya Mwakyembe ilimtaja Mrindoko na wenzake kuwa walihusika katika kuibeba kampuni ya Richamond na kuipa kazi ya kufua umeme wa dharura wakati haikustahili. Wengine waliotakiwa kuwajibishwa kwa kuliingiza taifa kwa makusudi kwenye kashfa ya Richmond na kusababisha hasara kubwa ni pamoja na Waziri wa Nishati na Madini wakati huo, Dk. Ibrahim Msabaha; aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Arthur Mwakapugi; na Bashir Mrindoko. Watendaji hao walidaiwa kushindwa kumshauri Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Nishati na Madini kuhusu udhaifu wa Richmond Development Company LLC ambao ulijulikana dhahiri toka mwaka 2004 kwenye Mkataba wa Bomba la Mafuta.
Mrindoko ndiye aliyeiandikia barua kampuni ya Richmond kusitisha mkataba wake na serikali mwezi mmoja tu kabla ya mchakato wa zabuni ya umeme wa dharura haujaanza. Kwa upande wa aliyekuwa Waziri Mkuu, Lowassa, Kamati ya Mwakyembe ilipendekeza kuwa kwa kuzingatia umuhimu wa nafasi aliyonayo katika uendeshaji wa shughuli za serikali na uongozi wa nchi kwa ujumla, ni wajibu wake mwenyewe kupima uzito wa matokeo ya uchunguzi huu na wajibu wake kikatiba ndani na nje ya Bunge. Vile vile ilisema ni wajibu wa Bunge ambalo linathibitisha uteuzi wake kwa mujibu wa Ibara ya 51 103 inayothibitisha uteuzi wake.
Hivi karibuni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimemtaka Dk. Mwakyembe ajiuzulu serikalini, kwani kuteuliwa kwa Mrindoko kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji ni kinyume na ripoti ya kamati yake aliyoiongoza. Katika hatua nyingine, CCM inakusudia kutumia mikanda ya video kuwaonyesha wajumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) na Kamati Kuu (CC) wanaopinga kwamba hakukuwa na majina ya wabunge watatu waliotajwa kuhusishwa na ufisadi na kutakiwa kujiuzulu. Wabunge wanaodaiwa kutajwa kuhusika na ufisadi na kutakiwa kujiuzulu ni pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa (Monduli), Rostam Aziz (Igunga) na Andrew Chenge (Bariadi Magharibi).
Habari ambazo Tanzania Daima Jumatano imezipata, zilisema kuwa chama hicho kinakusudia kuonyesha mikanda hiyo ya video ili kubaini ukweli wa suala hilo. Hadi sasa suala la wabunge hao kutakiwa kujiondoa au kutimuliwa kwenye chama, limeigawa CCM katika makundi mawili makubwa.
Kundi moja linadai kuwa suala la makada hao maarufu kama Mapacha Watatu, lilijadiliwa na kufikia maamuzi ya kuwataka wapime uzito na kuchukua hatua au watimuliwe wakati kundi lingine likipinga kwamba vikao vya CCM vilivyomalizika hivi karibuni mjini Dodoma, havikupitisha uamuzi huo wala kutaja majina yao. Mmoja wa makada wa CCM ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe, aliliambia gazeti hili kwamba mikanda hiyo itaonyeshwa katika kikao kijacho cha NEC kabla ya wajumbe kujadili yatokanayo na kikao kilichopita. Hakuna ubishi kwamba suala la ufisadi na maamuzi ya NEC iliyopita, limekigawa chama. Wapo wanaopinga akiwemo Katibu Mkuu mpya, Willson Mukama, kwamba hakuna majina yaliyotajwa, huku kundi lingine likisema majina ya kina Lowassa, Chenge na Rostam yalitajwa. Ili kukata mzizi wa fitna, tutalazimika kuangalia mkanda mzima uliorekodiwa kwenye vikao hivyo, alisema kada huyo.
Alipoulizwa na gazeti hili kuhusu sakata hilo, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, alisema kwa kawaida vikao vya CC na NEC hurekodiwa kwa sababu za kichama. Mimi naamini hatuna sababu ya kufikia kuonyesha mikanda ya vikao vilivyopita kwa sababu rekodi zipo. Ila ni kweli kwamba vikao hivyo huwa vinarekodiwa kwa sababu ya kuweka kumbukumbu za chama, alisema Nape. Alisisitiza kuwa maazimio ya NEC ni kuhakikisha watuhumiwa wa ufisadi wanatoka ndani ya chama na hilo lilisitizwa pia na Rais Kikwete wakati wa hotuba yake ya kufunga kikao cha NEC.
Tangu kumalizika kwa vikao hivyo, sekretarieti mpya wakiongozwa na Naibu Katibu Mkuu, Kapteni John Chiligati, na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nauye, katika mikutano yao ya kujitambulisha, wamekuwa wakidai kuwa NEC imepitisha uamuzi wa kuwatimua makada hao. Wanasema kwa nyakati tofauti kuwa makada hao wamepewa siku hadi kikao kijacho wawe wamejiengua vinginevyo watatimuliwa na chama. Hata hivyo hivi karibuni Katibu Mkuu, Mukama katika mkutano wake na wahariri wa vyombo vya habari alisema kuwa katika maamuzi ya NEC, hakuna majina yaliyotajwa.
Tanzania Daima