Kikwete atwishwa mzigo

Kikwete atwishwa mzigo

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,037
Reaction score
34,741
Wasomi wahoji, ni binafsi au msimamo wa serikali

PindaMizengo(7).jpg

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda

Kauli ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kutaka polisi kuwapiga raia wasiotii amri halali ya jeshi hilo, sasa suala hilo limeelekezwa kwa Rais Jakaya Kikwete.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema Rais Kikwete, akiwa Amiri Jeshi Mkuu, anapaswa kueleza tamko la Pinda ni kauli binafsi ama msimamo wa serikali yake.

Chadema inatajwa na `kunyooshewa kidole', kwamba inahusika katika kuandaa mikutano na maandamano yanayotawanywa na polisi kwa kile kinachodaiwa kufanyika kinyume cha sheria.

Kwa hali hiyo, Chadema kupiti Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika, kimesema kinatilia shaka tamko la Pinda bungeni, kikisema huenda ikawa ‘nyuma ya mashambulizi' yanayodaiwa kufanywa na polisi kwa nyakati tofauti dhidi ya raia wasiokuwa na hatia.

Hata hivyo, akifafanua kuhusu tamko lake bungeni, Pinda, alisema wanaoistahili adhabu ya kupigwa ni raia wanaoshindwa kutii amri ya polisi, inayotolewa kwa lengo la kuepusha vurugu nchini.

Lakini taarifa ya Mnyika iliyosambazwa na Afisa Habari wa Chadema, Tumaini Mekene, ilisema kuwa majibu ya Pinda bungeni yanatilia shaka kuhusu matukio yanayotajwa kuwahusisha polisi kuwa na mkono wa serikali.

Mnyika alitoa mfano wa maeneo ambayo vyombo vya dola vimetumika na kuwanyima wananchi haki ya kuishi kwa kusababisha mauaji ni pamoja na Mwanza, Ruvuma, Mbeya, Mtwara na Mara.

DK. BANA: PINDA AMEKOSA UVUMILIVU

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk. Benson Bana, alisema kauli ya Pinda inaonyesha ni jinsi gani alivyoshindwa kuvumilia jambo zito linalohitaji ufumbuzi wa kudumu.

"Pinda hakutoa kauli nzuri bungeni, lazima aangalie jambo zito na alichukuliaje kama kiongozi…si vyema kuruhusu vyombo vya dola viwapige watu kwa kukiuka amri, je, kama hawajakiuka na wamepigwa, itakuwaje," alihoji.

Akijibu swali la Mbunge wa Kilwa Kaskazini (CCM), Murtaza Mangungu, Pinda alisema ikiwa serikali (kupitia polisi) itatoa amri au maagizo ili yafuatwe, lakini ikatokea mtu ama watu kukaidi katika hali inayoashiria vurugu, hapatakuwa na namna nyingine zaidi ya kupigwa.

Mbunge huyo alitaka kusikia kauli ya serikali kuhusu vurugu zilizoambatana na raia kupigwa mabomu katika mikoa ya Arusha na Mtwara.

AVIKOSOA CHADEMA, CCM
Dk. Bana alisema kauli zilizotolewa kwa nyakati tofauti na Chadema na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuhusu vurugu za Arusha, hazikuwa za kiungwana.

Alisema kitendo cha Chadema kulalamika moja kwa moja kuhusiana na ulipukaji wa bomu katika mkutano wao na kumhusisha polisi, pamoja na CCM kudai chama hicho (Chadema) wamejilipua ni za uchochezi.
"Hizi ni kauli za uchochezi na za kukurupuka kwa viongozi wa Chadema na CCM, lakini pia Waziri Mkuu ametoa kauli nzito sana juzi na kushindwa kuangalia jambo zito lichukuliwaje," alisema Dk. Bana.

Kuhusu mlipuko wa bomu kwenye mkutano wa Chadema mjini Arusha, Dk Bana, aliiasa jamii kutambua kwamba ni mapema kujua asili na kusudio lake.

"Lakini suala hilo linaweza likawa la kigaidi ama jinai, na hivyo wanasiasa wasiingilie na kulibeba wakati vyombo vya ulinzi na usalama vinalifanyia uchunguzi," alisema.

Dk. Bana alisema tukio la kwanza la kulipuka kwa bomu katika Kanisa Katoliki, Parokia ya Olasiti Jimbo Kuu la Arusha, polisi waliachiwa kufanya uchunguzi, lakini hali haipo hivyo kwa upande wa ilivyotokea kwa Chadema.

"Wakati Chadema wakizungumza kuhusu tukio hilo, Nape naye anakurupuka na kudai chama hicho kinafanya kile wanachotaka…sasa vyombo vya usalama vinafanya kazi gani," alihoji.
Aidha, alisema iwapo Chadema hakiamini vyombo vya dola hata kupeleka ushahidi polisi, basi wanatakiwa kujenga hoja bungeni kutokuwa na imani na polisi na busara zifanyike ili chombo hicho kifanye kazi yake.

Mhadhiri huyo alivitaka vyama vya siasa kujenga mazingira ya kuaminiana na kuwa na imani kwa vyombo vya ulinzi na usalama.
Naye Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mukandala, alisema ili kufikia mustakabali mzuri wa

taifa, lazima kujenga mazingira ya kuheshimiana, kuvumiliana na kujenga ushindani kwa njia ya hoja na upendo.
Alisema kila chama lazima kitafakari wanachokifanya kutokana na ukweli kwamba, vyote vinalenga kuwaongoza Watanzania.
"Tukio la Arusha linalaaniwa na kila mtu, lakini kwanza tuache vyombo husika vifanye kazi yake," alisema Profesa Mukandala.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

Huyu bana asizingue, asitake kujikosha, sasa hii ni kama vita vya chichi kati ya CCM na vyama pinzani, sasa inahitajika maamuzi ya wazi yenye utekelezaji haya mamba ya kaeni chini muongee hayatazaidia sana, mambo mangapi machafu yameisha fanya na CCM, na hawa wanaojiita wasomi wamuwa wakikemea kinafiki.
siasa sasa basi maana damu za ndugu zetu zinaendekea kumwagika bila kosa lolote. kisha anakuja bwana mmja juha, mambae yeye anajidhahia ni mwerevu anadai polisi wapigeni sana
 
Kwa kweli Pinda amechemka sana,huyu si kiongozi hata kidogo,ni dickteta lililojificha ndani ya ngozi ya kondoo!
 
Bana mdomo kunuka anatukera aache kujifanya neutral wakati ukisoma kwa makini unakuta ameegemea CCM mzoroteshaji wa demokrasia mkubwa.
 
"mada inasema KIKWETE ATWISHWA MZIGO halaf maelezo yaliyomo kwenye mada hii na huo mzigo aliotwishwa bwana kikwete sjajua ni mzigo gani aliotwishwa.............au hili suala la kumtaka ajibu kuwa ni tamko la SERIKALI au la PINDA,NIMEJILAZIMISHA TU KUELEWA YALIYOMO ILA SIDHANI KAMA YALIYOMO YAMO..."
 
Akili za pinda zimepinda kama jina lake!! Hata aibu hana,akibanwa hapa anaanza kulialia kutafuta public sympath.
 
Kiongozi kama pinda kulia mbele ya watu wake ni aibu ya taifa na ilidhihilisha kuwa kuwa hana kitu. Nafasi yake siyo ya kulia bali niyakutafuta ufumbuzi. Sasa yeye akilia na wananchi wakalia nani atamtia moyo mwenzie. Hii siyo hoja ya uzi huu, ila nimelileta kuwaonyesha kuwa anakasoro katika kufikiri na kufanya maamuzi kwa masula mazito. Kiongozi wa nafasi kama yake hawezi kuwaambia wanachi ngoja muipate hata kama kwa ndani unajihisi kusema hivyo. Hafai.
 
Wasomi wahoji, ni binafsi au msimamo wa serikali

PindaMizengo(7).jpg

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda

Kauli ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kutaka polisi kuwapiga raia wasiotii amri halali ya jeshi hilo, sasa suala hilo limeelekezwa kwa Rais Jakaya Kikwete.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema Rais Kikwete, akiwa Amiri Jeshi Mkuu, anapaswa kueleza tamko la Pinda ni kauli binafsi ama msimamo wa serikali yake.

Chadema inatajwa na `kunyooshewa kidole', kwamba inahusika katika kuandaa mikutano na maandamano yanayotawanywa na polisi kwa kile kinachodaiwa kufanyika kinyume cha sheria.

Kwa hali hiyo, Chadema kupiti Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika, kimesema kinatilia shaka tamko la Pinda bungeni, kikisema huenda ikawa ‘nyuma ya mashambulizi' yanayodaiwa kufanywa na polisi kwa nyakati tofauti dhidi ya raia wasiokuwa na hatia.

Hata hivyo, akifafanua kuhusu tamko lake bungeni, Pinda, alisema wanaoistahili adhabu ya kupigwa ni raia wanaoshindwa kutii amri ya polisi, inayotolewa kwa lengo la kuepusha vurugu nchini.

Lakini taarifa ya Mnyika iliyosambazwa na Afisa Habari wa Chadema, Tumaini Mekene, ilisema kuwa majibu ya Pinda bungeni yanatilia shaka kuhusu matukio yanayotajwa kuwahusisha polisi kuwa na mkono wa serikali.

Mnyika alitoa mfano wa maeneo ambayo vyombo vya dola vimetumika na kuwanyima wananchi haki ya kuishi kwa kusababisha mauaji ni pamoja na Mwanza, Ruvuma, Mbeya, Mtwara na Mara.

DK. BANA: PINDA AMEKOSA UVUMILIVU

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk. Benson Bana, alisema kauli ya Pinda inaonyesha ni jinsi gani alivyoshindwa kuvumilia jambo zito linalohitaji ufumbuzi wa kudumu.

"Pinda hakutoa kauli nzuri bungeni, lazima aangalie jambo zito na alichukuliaje kama kiongozi…si vyema kuruhusu vyombo vya dola viwapige watu kwa kukiuka amri, je, kama hawajakiuka na wamepigwa, itakuwaje," alihoji.

Akijibu swali la Mbunge wa Kilwa Kaskazini (CCM), Murtaza Mangungu, Pinda alisema ikiwa serikali (kupitia polisi) itatoa amri au maagizo ili yafuatwe, lakini ikatokea mtu ama watu kukaidi katika hali inayoashiria vurugu, hapatakuwa na namna nyingine zaidi ya kupigwa.

Mbunge huyo alitaka kusikia kauli ya serikali kuhusu vurugu zilizoambatana na raia kupigwa mabomu katika mikoa ya Arusha na Mtwara.

AVIKOSOA CHADEMA, CCM
Dk. Bana alisema kauli zilizotolewa kwa nyakati tofauti na Chadema na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuhusu vurugu za Arusha, hazikuwa za kiungwana.

Alisema kitendo cha Chadema kulalamika moja kwa moja kuhusiana na ulipukaji wa bomu katika mkutano wao na kumhusisha polisi, pamoja na CCM kudai chama hicho (Chadema) wamejilipua ni za uchochezi.
"Hizi ni kauli za uchochezi na za kukurupuka kwa viongozi wa Chadema na CCM, lakini pia Waziri Mkuu ametoa kauli nzito sana juzi na kushindwa kuangalia jambo zito lichukuliwaje," alisema Dk. Bana.

Kuhusu mlipuko wa bomu kwenye mkutano wa Chadema mjini Arusha, Dk Bana, aliiasa jamii kutambua kwamba ni mapema kujua asili na kusudio lake.

"Lakini suala hilo linaweza likawa la kigaidi ama jinai, na hivyo wanasiasa wasiingilie na kulibeba wakati vyombo vya ulinzi na usalama vinalifanyia uchunguzi," alisema.

Dk. Bana alisema tukio la kwanza la kulipuka kwa bomu katika Kanisa Katoliki, Parokia ya Olasiti Jimbo Kuu la Arusha, polisi waliachiwa kufanya uchunguzi, lakini hali haipo hivyo kwa upande wa ilivyotokea kwa Chadema.

"Wakati Chadema wakizungumza kuhusu tukio hilo, Nape naye anakurupuka na kudai chama hicho kinafanya kile wanachotaka…sasa vyombo vya usalama vinafanya kazi gani," alihoji.
Aidha, alisema iwapo Chadema hakiamini vyombo vya dola hata kupeleka ushahidi polisi, basi wanatakiwa kujenga hoja bungeni kutokuwa na imani na polisi na busara zifanyike ili chombo hicho kifanye kazi yake.

Mhadhiri huyo alivitaka vyama vya siasa kujenga mazingira ya kuaminiana na kuwa na imani kwa vyombo vya ulinzi na usalama.
Naye Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mukandala, alisema ili kufikia mustakabali mzuri wa

taifa, lazima kujenga mazingira ya kuheshimiana, kuvumiliana na kujenga ushindani kwa njia ya hoja na upendo.
Alisema kila chama lazima kitafakari wanachokifanya kutokana na ukweli kwamba, vyote vinalenga kuwaongoza Watanzania.
"Tukio la Arusha linalaaniwa na kila mtu, lakini kwanza tuache vyombo husika vifanye kazi yake," alisema Profesa Mukandala.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

hii ndo hali inayoendelea mtwara so mizengo pinda kathibitisha tu
1001149_272324819575683_1317479769_n.jpg
 
Sitashangaa kama Kikwete na huyu kenge wakaja kutofautiana katika hili kwani si mara ya kwanza kufanya hivyo.
 
Mzigo mzito kajitwisha mwenyewe,angeamua kuwaambia Mwigulu & co sasa basi imetosha ,mauaji ya raia yasingekuwepo.
Na sababu Urais ni wa kwake na familia yake haya yote yapo juu yake na familia yake.
 
Hapa kweli huyu mzee wa kifipa kachemka. kama mtu akivunja sheria zilizowekwa na serikali inapaswa achukuliwe hatua inayofaa kulingana na vifungo vya sheria vilivyopo. Na katika sheria zetu ya nchi hatuna sheria inayosema mtu akivunja sheria anastahili achukue kibano. Kweli Chadema wanawapeleka puta CCM
 
Mzigo upi wakati hilo alilipanga kulifanya strategically na hakuna la kushangaa.
 
Back
Top Bottom